Official: Serikali ya JK Imeshindwa Kudeliver | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Official: Serikali ya JK Imeshindwa Kudeliver

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Uswe, Jan 22, 2011.

 1. U

  Uswe JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  JK ana degree ya Uchumi. JK ukimuuliza rate ya inflation tanzania anakwambia 5.5% kwa mwaka, tena anatongeza na vijimajigambo kwamba ilikua above tena lakini jitihada za serikali yake zimeishusha, lakini twende mtaaani


  MAFUTA: (yakipanda bei hakuna ambacho hakipandi) over the last 12 months or so yamepanda kwa asilimia ngapi? ryt now petrol ni kati ya 1750 - 1880 kwa lita


  UMEME: kitu ambacho tunakihitaji sana kwa uzalishaji sio tu viwandani hata kwenye huduma nyingine za jamii, sio tu umepanda bei haupatikani kabisa, unarudi usiku tu ili muweze kuwasha feni ziwapepee wakati mmelala


  RUSHWA: nenda polisi au mahakamani uone hilo balaa, nilikua sijui ukubwa wa hili jambo mpaka ndugu yangu alipopata matatizo, ni serikali tu yenye uwezo wa kukomesha rushwa, lakini ya JK imefeli vibaya kwenye hili.


  AJIRA: hivi katika kampeni 2005 aliahidi kuongeza ajira eeeh? ameongeza za walimu


  MAFUTA, UMEME, RUSHWA na AJIRA serikali ya JK imefeli kabisa, kama ni ranking 2/10 na kinachozingua zaidi sio tu imefeli hakuna jitihada za kujikwamua ndo ndo kwanza jamaa karudi ikulu we have another four or smthing years to deal with it. . . .TUTAKOMA!
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Haya bana, naona umemaliza kila kitu so hatuna cha kuchangia. Angalizo: serikali haiwezi kutatua tatizo la umeme kwani wenye serikali ya JK ndo wanauza genereta na mafuta yake, serikali haiwezi kutatua tatizo la ajira kwani mwajiri mkuu bado ni serikali na kwa sasa serikali haina fedha ya kuajiri japo deficit ya watumishi katika nyanja kubwa kama elimu, afya na ulinzi ni kubwa hii ni kwa sababu . Tazama mpaka sasa ktk nusu ya kwanza ya mwaka huu wa fedha serikali tayari ina nakshi ya bajeti inayofikia takriban trilion 7. So serikali ya JK haiwezi kudeliver ila yeye ataendela ku-smile na kujenga mahekalu pale msoga. Ciao.
   
 3. B

  Bull JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama umuamini JK kwamaba uchumi wa Tanzania haukui na inflation haiko down basi GOOGLE mwenyewe utapata data za world bank na IMF ndi utaamini kuwa kikwete hajafeli
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Uta deliver vipi kama na wewe ukiwa unawaabudu mafisadi
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Yote uliyoyataja yanatokea duniani kote UK prices of goods are rsing, employment at fall, US usiseme? next?
   
Loading...