Ofa za wanaume zimebeba mengi!

vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
165
Kwa huku kwetu ni wanaume wachache sana wanaomsaidia mwanamke bila lengo la kumpata mwanamke huyo. Hata hivyo sio wanawake wengi wanaokubali kulipa fadhila kwa njia hiyo, lakini wanaume wengi hutumia misaada au ofa kama chambo cha kuwanasia wanawake.

Kwa wanawake kusaidiwa ni kusaidiwa tu huwa hakufungwi na kutakiwa kimapenzi, lakini kwa wanaume kusaidia huwa kunafungwa pamoja na mapenzi.

Je sababu ni nini?

Wanaume wamelelewa na kufanywa kuamini kwamba wanatakiwa kuonesha sifa fulani kwa wanawake kabla hawajawatongoza. Kwa hiyo mwanaume kabla hajatongoza huanza kujisifu kwanza, ili mwanamke amuone kama mtu anayeweza, hivyo mwanaume anapotoa msaada kwa mwanamke kuna mawili kama sio matatu, ama anataka kusifiwa au anamtaka mwanamke huyo, au vyote.

Lakini pia wanaume wengi huamini kwamba kwa kutoa ofa, mwanamke atajua kwamba anamtaka, hivyo kwa wanaume hao ofa ndio kutongoza kwenyewe. Kwa hiyo mwanume kama huyu anapotoa msaada kwa mwanamke anatarajia kumpata kimapenzi mwanamke huyo.

Kwa mijini kwa mfano mwanamke anayepewa lifti ni yule mzuri kwa sura na umbo, ukweli ni kwamba hakuna msaada hapo bali mwanaume anaanza kununua penzi ambalo hajalipata. Mwanaume akimpa lifti mwanamke na kumtongoza, na mwanamke huyo akakataa, basi huo msaada unafutwa mara moja.

Kwenye baa, mwanaume anaweza kumtuma mhudumu ampe pombe mwanamke fulani. Hajui mwanamke huyo kaja hapo baa na nani na anafanya kitu gani. hiyo ofa sio ya urafiki bali ni ombi la mwili wa mwanamke huyo, kwani hiyo ni hatua ya awali ya kuwa karibu nae.

Kuna idadi kubwa ya wanaume ambao hujitolea kuwasomesha, kuwapa au kuwatafutia ajira wanawake, lakini nyuma ya kujitolea huko, kuna agenda ya kuutaka mwili wa huyo mwanamke. Mara nyingi mwanamke anakuwa hajui kwamba misaada mingi ya wanaume imefungwa pamoja na mapenzi. Ni wanaume wachache sana waliolelewa tofauti wasiofanya hivyo.

Ukweli ni kwamba wanawake wengi wamekuwa wahanga wa misaada. Utakuta mwanaume anamsaidia mwanamke, mwanamke anapokea misaada hiyo akijua ni ya kibinadamu, kumbe akilini mwa mwanaume ni kwamba amewekeza. kwa hiyo anapokuja kumtongoza mwanamke huyo akakataa basi vita huanza.

Mwanaume anaweza kukumbushia misaada aliyotoa. na katika hali ya kushangaza mwanamke huyo hushikwa na butwaa. kwani hakujua kwamba alikuwa anapewa misaada ili atoe mwili wake. Kuna wanaume wengi tu ambao wanaweza kumpa mwanamke soda kama taarifa kwamba amempenda, na mwanamke anaweza kupokea soda hiyo akijua kwamba ni ofa ya kawaida, lakini baadae hushangaa akija kutongozwa, na akikataa, anadaiwa soda aliyokunywa.

Nawasihi wanawake wenzangu wawe makini na ofa za wanaume kwani nyingi zimejaa utata mkubwa.

snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
17,388
22,839
vukani vipi mamii na hawa viumbe wanaotupa raha ya dunia!?
 
Last edited by a moderator:

vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
165
vukani vipi mamii na hawa viumbe wanaotupa raha ya dunia!?

Ah dada wee, ujue tuna mabinti, na siku hizi na malezi ya watoto wa kike sio kama ya zamani, kuna mafisadi wa mapenzi ka nini ni vyema kuvunja ukimya
 
bhikola

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,130
1,654
wakati mwingine tatizo ni wanawake wenyewe bana, unakuta demu yuko tight robo uwanja unaamua kurescure hali, na unamtoa kweli kweli, mwisho wa siku anataka akulipe in kind aaaaaaaaaaaahhhhhh!!!!!!!!!
au mwingine anakuja na story ya kukopa, unajua mimi nina shida na nini na vile unasema ok poa isiwe ishu bana, unamrekebishia ishu zake, mwisho wa siku ukinaza kudai au kutaka atimize makubaliano anaanza kukuletea za kuleta na kulegeza macho na sauti kwingi, kisa anataka akulipe in-kind
Acheni kupenda ofa na kuomba omba ovyo baaaaaaaaaaaaaaasssssssssssss, otherwise muwe wepesi kutimiza ahadi zenu na siyo kujilengesha
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
44,441
51,157
Kama ushayajua hayo basi kataa offer on the spot ukikubali offer basi unakubali chochote kitakachotokeaa naungana na Kongosho ukitaka kula shurti nawe uliwe........By J.M Kikwete
 
Last edited by a moderator:

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,872
4,536
Inawezekana mwanangu una hoja ingawa haina utafiti. Kama umefanyiwa hivyo basi amini si wote. Nadhani hali ya kutakana au la inategemea na wahusika. Ni muhimu kusema kuanzia mwanzo kuwa msaada ulio mzuri haupaswi kuwa na masharti. Hata hivyo sioni kama watoa misaada wanalazimisha kupewa malipo. Kwa sisi wa kizazi cha zamani kutoa msaada kuliishia kwenye msaada. Ukimsaidia mwanamke sana sana anakuwa ndugu au rafiki lakini si mpenzi. Nimewahi kusomesha msichana mmoja lakini baada ya kufanya hivyo nilimchukulia kama dada yangu au binti yangu ingawa wakati ule nilikuwa single. Kuna watu hata walinijia wakitaka nimuoe nikawajibu kuwa kama ningefanya hivyo thamani ya msaada wangu kwake ingetoweka. Kwangu thamani ya msaada ilikuwa muhimu kuliko maslahi yangu binafsi.
 
mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
24,214
34,360
kwa huku kwetu ni wanaume wachache sana wanaomsaidia mwanamke bila lengo la kumpata mwanamke huyo. Hata hivyo sio wanawake wengi wanaokubali kulipa fadhila kwa njia hiyo, lakini wanaume wengi hutumia misaada au ofa kama chambo cha kuwanasia wanawake.

Kwa wanawake kusaidiwa ni kusaidiwa tu huwa hakufungwi na kutakiwa kimapenzi, lakini kwa wanaume kusaidia huwa kunafungwa pamoja na mapenzi.

Je sababu ni nini?

Wanaume wamelelewa na kufanywa kuamini kwamba wanatakiwa kuonesha sifa fulani kwa wanawake kabla hawajawatongoza. Kwa hiyo mwanaume kabla hajatongoza huanza kujisifu kwanza, ili mwanamke amuone kama mtu anayeweza, hivyo mwanaume anapotoa msaada kwa mwanamke kuna mawili kama sio matatu, ama anataka kusifiwa au anamtaka mwanamke huyo, au vyote.

Lakini pia wanaume wengi huamini kwamba kwa kutoa ofa, mwanamke atajua kwamba anamtaka, hivyo kwa wanaume hao ofa ndio kutongoza kwenyewe. Kwa hiyo mwanume kama huyu anapotoa msaada kwa mwanamke anatarajia kumpata kimapenzi mwanamke huyo.

Kwa mijini kwa mfano mwanamke anayepewa lifti ni yule mzuri kwa sura na umbo, ukweli ni kwamba hakuna msaada hapo bali mwanaume anaanza kununua penzi ambalo hajalipata. Mwanaume akimpa lifti mwanamke na kumtongoza, na mwanamke huyo akakataa, basi huo msaada unafutwa mara moja.

Kwenye baa, mwanaume anaweza kumtuma mhudumu ampe pombe mwanamke fulani. Hajui mwanamke huyo kaja hapo baa na nani na anafanya kitu gani. Hiyo ofa sio ya urafiki bali ni ombi la mwili wa mwanamke huyo, kwani hiyo ni hatua ya awali ya kuwa karibu nae.

Kuna idadi kubwa ya wanaume ambao hujitolea kuwasomesha, kuwapa au kuwatafutia ajira wanawake, lakini nyuma ya kujitolea huko, kuna agenda ya kuutaka mwili wa huyo mwanamke. Mara nyingi mwanamke anakuwa hajui kwamba misaada mingi ya wanaume imefungwa pamoja na mapenzi. Ni wanaume wachache sana waliolelewa tofauti wasiofanya hivyo.

Ukweli ni kwamba wanawake wengi wamekuwa wahanga wa misaada. Utakuta mwanaume anamsaidia mwanamke, mwanamke anapokea misaada hiyo akijua ni ya kibinadamu, kumbe akilini mwa mwanaume ni kwamba amewekeza. Kwa hiyo anapokuja kumtongoza mwanamke huyo akakataa basi vita huanza.

Mwanaume anaweza kukumbushia misaada aliyotoa. Na katika hali ya kushangaza mwanamke huyo hushikwa na butwaa. Kwani hakujua kwamba alikuwa anapewa misaada ili atoe mwili wake. Kuna wanaume wengi tu ambao wanaweza kumpa mwanamke soda kama taarifa kwamba amempenda, na mwanamke anaweza kupokea soda hiyo akijua kwamba ni ofa ya kawaida, lakini baadae hushangaa akija kutongozwa, na akikataa, anadaiwa soda aliyokunywa.

Nawasihi wanawake wenzangu wawe makini na ofa za wanaume kwani nyingi zimejaa utata mkubwa.

ofa yoyote ya mwanaume wa ukweli lazima uilipie kwa pumegwa papuchi!!! Wanaume tunahangaika kusaka pesa mjini humu alafu wewe ule ofa zetu bure bure weeeee!!! Lazima upanue miguu
 
Tized

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
4,023
5,897
Asante Fadher, barikiwa sana. Nadhani pia kuna nadharia mbaya iliojengeka miongoni mwa wadada kuwa ukimcare/kumsaidia lazima utakuwa umempenda au unamtaka, ilishanitokea mara kadhaa kwa wachache niliweza kuwasaidia au kuwakopesha kwa namna moja au nyingine, so wakti mwingine unajikuta unafanya kazi kisaikolojia kumuonesha kuwa anavyofikiri sivyo n.k

Naamini mtu ukitumia shida ya mtu mwingine kama kigezo cha kumpata, japo utafanikiwa lakini ni kama unachuma laana flani ivi..... Mbaya sana. ''Nadhani huu itakuwa sio msaada, labda tuuite ni HONGO kwa sababu unatolewa in favour of something''

Inawezekana mwanangu una hoja ingawa haina utafiti. Kama umefanyiwa hivyo basi amini si wote. Nadhani hali ya kutakana au la inategemea na wahusika. Ni muhimu kusema kuanzia mwanzo kuwa msaada ulio mzuri haupaswi kuwa na masharti. Hata hivyo sioni kama watoa misaada wanalazimisha kupewa malipo. Kwa sisi wa kizazi cha zamani kutoa msaada kuliishia kwenye msaada. Ukimsaidia mwanamke sana sana anakuwa ndugu au rafiki lakini si mpenzi. Nimewahi kusomesha msichana mmoja lakini baada ya kufanya hivyo nilimchukulia kama dada yangu au binti yangu ingawa wakati ule nilikuwa single. Kuna watu hata walinijia wakitaka nimuoe nikawajibu kuwa kama ningefanya hivyo thamani ya msaada wangu kwake ingetoweka. Kwangu thamani ya msaada ilikuwa muhimu kuliko maslahi yangu binafsi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom