Ofa ya pasaka kwa wateja wa airtel

UKIONGEZA SALIO UTAWEZA KUPATA
Dakika za bure;message 100 na MB200
kuangalia dk bonyeza *102*05# ok;
kuangalia message bonyeza *102*15#;
kuangalia salio la data bonyeza *102*06# ok.

Offer hiyo inaanza kutumika saa sita usiku hadi kumi na mbili hasubuhi

HAMIA AIRTEL

nilikuwa nimeweka laini yangu kando kidogo.Mpaka uongeze salio ndio unapata hiyo zawadi ya pasaka?
 
Hivi jamani leo ndio mnagundua kuwa airtel ni wezi na wanyonyaji wakubwa matangazo yao mengi na hizo offer nyingi ni za uongo nimekwishachoka nao
 
Eti ofa!!!!!!!. Hamjui kuwa makampuni haya ni firms which try to make profit???????......................We unafikiri kwanini ofa zao zoooote ni za usiku wa manane,,,,,,,,,,,Kama ni kutoa ofa si bora wangejitosa kwenye elimu ili kuwafadhili wasio na uwezo?
Ofa ya kuwasiliana usiku itakusaidiaje wewe mtanzania wa leo unayeishi katika ulimwengu wa ushindani???????
Nahisi ofa zingine ni za kuidumaza jamii tu na kwenda kinyume na maadili kwa kulala mchana ili ukeshe usiku kufaidi ofa zao.:blah:
 
Mkuu tunashukuru kwa tangazo hili la ofa..mkuu kama hii ofa ni kunufaisha watumiaji kwanin imeletwa kwa masharti makali mkuu..saa sita usiku naamini walio wengi wanaojishughulisha na shughuli zao za kujikwamua kimaisha watakuwa wamepumzika na hawatoweza kupata huo muda wa kuifurahia ofa hii ya airtel. lakin wangeipewa muda mwingine ukiwa mchana wangeweza kuifaidi vizuri kuliko usiku wa mnane halafu inaisha tuu wanapoamka kujiandaa kwenda kwenye shughuli mbalimbali. kwa mtazamo wangu hii ofa ingetolewa ule muda watu bado wanaendelea na shughuli zako na sio ule muda ambao watakuwa kitandani..hata yule atakae kuwa macho kuisubiri, atakaekuwa anataka kuwasiliana nae atakuwa usingizin na kumuamsha kwa ajili ya ofa ya airtel itakuwa ni kero nyiingine. hizi ofa zinatolewa kwa masharti ya kupiga simu saa 6 usiku hazina mantiki kwa kunufaisha watumiaji wake..bali kero kwa watumiaji. ni kuwaridhisha kuwa ofa pia zipo.
UKIONGEZA SALIO UTAWEZA KUPATA
Dakika za bure;message 100 na MB200
kuangalia dk bonyeza *102*05# ok;
kuangalia message bonyeza *102*15#;
kuangalia salio la data bonyeza *102*06# ok.

Offer hiyo inaanza kutumika saa sita usiku hadi kumi na mbili hasubuhi

HAMIA AIRTEL
 
Back
Top Bottom