Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,016
- 9,885
Mteja wa Vodacom, Enock Akeyo alipokea ujumbe kutoka vodacom mwaka 2018 ukisema "Pesa ni Mpesa tunakupa MB 100 BURE kuperuzi intaneti kwa saa 24 ukiongeza salio la TZS 500 au zaidi kwa Mpesa leo."
Enock aliongeza salio na akapokea sms iliyoonesha amepewa MB100 za kuperuzi. Hata hivyo baada ya dk 8 akashangaa salio lake lote limeisha. Alipowapigia aliambiwa hakujiunga na kifurushi ndio sababu ya hela yake kutumika
Enock alienda Kamati ya Malalamiko ya TCRA ili kufikisha kesi hiyo na kudai fidia ya Tsh. 5,000,000 kwa sababu ya usumbufu na kupewa ahadi ya uongo wa ofa ya Mb.
Hata hivyo, vodacom walithibitisha kuwa mteja wao alipata MB100 lakini alizitumia kwa sekunde moja na zikaisha zote.Yaani aliwasha data majira ya saa mbili na dakika 22 na sekunde 51, na muda huohuo MB100 ziliisha.
Mbali na kuwa inaonesha ukakasi lakini kamati ya malalamiko ya TCRA ilikubali hoja za Vodacom hivyo Enock alishindwa kupata fidia mbali na kusema ilimletea shida.
Kwa maelezo ya Enock ni kuwa alipowasha data alisoma emails chache na kuingia JamiiForums kuperuzi akapata taarifa salio lake ni Tsh 0.00