Ofa kwa Wanaopenda Kupanda Mlima Kilimanjaro

Ofa kwa Wanaopenda Kupanda Mlima Kilimanjaro

Filipo Lubua

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2011
Posts
339
Reaction score
579
Umeianza safari, kwa nyingi mbwembwe bashasha
Na mkeo mwasafiri, Ki’manjaro kupandisha
Utambue ni hatari, tamaa kumkatisha
Mwapanda Kilimanjaro, vyema mfike pamoja

Mnapopanda mlima, sikiliza nikweleze
Muoneane huruma, ndo safari ipendeze
Mtembee kwa kudema, haraka siendekeze
Mlima Kilimanjaro, pupa kamwe hautaki

Mmeianza pamoja, safari yenye furaha
Kwa hatua mojamoja, mtembee kwa staha
Umaridhawa ni tija, ipunguzeni mizaha
Kufika Kibo ni lengo, ila mfike pamoja

Kukwea mlima huu, si kwepesi nakwambia
Pamoja kufika juu, liwe lengo la kwanzia
Kamwe usije sahau, Hawa pole atembea
Mtembeze taratibu, safari siharakishe

Kwani haraka ya nini, wapi unakimbilia?
Mwenzio wamwacha chini, kilele wafukuzia
Nyote mko safarini, kasi waing’ang’ania
Kile kilele cha Kibo, raha kufika pamoja

Ufikapo kileleni, kabla mwenzio kufika
Soga tapiga na nani, uzuri kuajabika
Taratibu tembeeni, acha kuleta dhihaka
Raha kufika pamoja, kilele kukifikia

Wewe juu umefika, yeye bado atembea
Wamwacha kwenye kichaka, pek’yake ajihemea
Aweza ng’atwa na nyoka, nani tamsaidia?
Tembeeni polepole, hadi kilele kufika

Wafurahia theluji, kileleni ilojaa
Yeye bado yu dibaji, safari akazania
Moyoni mwake ahoji, hujui kuhudumia?
Subiri nyote mfike, uzuri wote kuwona

Nimeona nishauri, wale wapanda milima
Najua mmekariri, mwadhani mwapiga ngoma
Mlima kuuabiri, kwataka nyingi hekima
Kupanda Kilimanjaro, kwataka mwingi weledi

Wengine mnashangaa, eti naandika nini
Umalenga si sanaa, ni kutia watu nuruni
Mimi nimemalizia, usibaki ujingani
Mnapopanda mlima, kilele fikeni wote


© Filipo Lubua, 23 Machi 2014
 
Mhhhhh nilivokuja spidi sasa....bado najichanga ,i wanna climb the kilimanjaro this year...yani dah,umenikata stimu..enewei sio mbaya
 
542280_269083626535292_1763545302_n.jpg
 
Mhhhhh nilivokuja spidi sasa....bado najichanga ,i wanna climb the kilimanjaro this year...yani dah,umenikata stimu..enewei sio mbaya
Pole sana mkuu. Niko kwenye kozi ya uandishi wa habari. Najifunza kuandika habari zisizo na vichwa vinavyofanana na habari yenyewe. Kama ingekuwa gazeti hapo si ungeshanunua? naomba radhi lakini, ikiwa wewe sio mpenzi wa mashairi na kupanda mlima Kilimanjaro kama shairi lizungumziavyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom