Uko sahihi kabisa, risasi haipigi kona, gurudumu lipo mbele na kiti kipo nyuma. Alyepiga risasi yu nyuma ya aliyepigwa risasi.
Itawezekana vipi risasi ipige gurudumu halafu irudi tena kumpiga mtu makalioni!
nakubaliana nawe. mgongaji kakimbia. afisa polisi anamfukuza kwa nyuma nae yuko garini. kafyatua risasi 1 tu. hiyo risasi imepiga gurudumu la mbele. kisha ikamrudia dereva aliyekaa nyuma ya hilo gurudumu! jamani hata lies inabidi viwe na mantiki kidogo, vinginevyo mnajidhalilisha!
Tunaomba kuazima kazi za wapelelezi, labda risasi iliikosa tairi ikaenda kupiga engo ya gari karibu na makalio ya dereva! Kazi wanayo wapelelezi!
:grouphug::mod::A S-rose:Hongera OCD huo ndiyo uzalendo,hata kama siyo kituo chako cha kazi,ukiona uhalifu chukua hatua mtuhumiwa akiresist use reasonable force hiyo ndiyo falsafa ya usalama ,hata ungeua hakuna shaka kuliko kuacha mtuhumiwa aende untouched:A S-rose:
Hata mimi najiuliza mara mbilimbili sipati jibu, namna gani risasi ipasue tairi then iende makalioni.... mmh!how come risasi itoke kwenye tairi hadi makalioni? Huyo kamanda alikuwa kwenye engo gani alipokuwa akipiga hiyo risasi?
Mimi pia hapa sijapaelewa, tairi ya mbele na makalio!
habari hii ina walakini sana, kwanza sua wenyewe wanakanusha lecturer wao kupigwa risasi, pili sua hawana kitengo cha sanaa, sasa huyo mtu anahusishwa vipi na sua. by the way inasemekana ma-ocd wote wapo moro kwa semina.
morogoro ulivyo mji mdogo,angechukua namba ya gari tu isingetosha?akili matope,si ajabu victim aliachwa hapo akafukuzia gari!ndo akili za polisi wetu,angeweza kuua wapita njia 3 wakati anamlipua huyo prof wa watu!
:grouphug::mod::A S-rose:Hongera OCD huo ndiyo uzalendo,hata kama siyo kituo chako cha kazi,ukiona uhalifu chukua hatua mtuhumiwa akiresist use reasonable force hiyo ndiyo falsafa ya usalama ,hata ungeua hakuna shaka kuliko kuacha mtuhumiwa aende untouched:A S-rose:
OCD ni mtu wa usalama, huyo jamaa hakupaswa kukimbia! Hii stori imekaa kimtego sana, na maelezo tunayoyapata humu ni ya hearsay, mpaka hapo tutaposikia kauli ya huyo mwalimu na OCD mwenyewe (mahakamani). Huenda ticha ni mkosaji na OCD ni mwanausalama hivyo hapaswi kufuma macho mhalifu anatimua, ama huenda kuna ishu nyingine pasono kati ya wawili hawa!
hiyo ni falsafa ya usalama wa nchi gani? ninavojua mimi, polisi hatakiwi kutumia nguvu kubwa kupita kiasi ili kumdhibiti mtuhumiwa, huyo polisi alifanya vizuri kumfatilia mtuhumiwa lakini kufyatua risasi alifanya kosa, it's unproffessional! jaribu kufikiria kama lile gari lililogonga lingekuwa ni taxi na wewe ni abiria halafu dereva anakimbia baada ya ajali halafu polisi anafyatulia gari risasi kwa kulenga tairi la mbele na gari
linapinduka na wewe abiria unajeruhiwa au kufa kwa ajili ya upumbavu wa huyu polisi, itakuwa ni busara hiyo? hata kama mwenye baiskeli naye afe baada ya ajali bado kitendo cha polisi huyo kitakuwa ni cha kipumbavu, na vipi ikiwa mwenye baiskeli akinusurika huku wewe abiria ufe au dereva wa taxi afe au wote! ni upumbavu tu! na una uhakika gani kama sababu ya ajali ni uzembe wa dereva wa gari au ni makosa ya mwendesha baiskeli yaliyoshidwa kuepukika? it's a traffic case! madereva wengine huwa wanakimbia baada ya ajali kwa kusalimisha maisha yao kutoka kwa wananchi wanaochukua sheria mkononi na baadae huenda kuripoti polisi.kupiga risasi ya 'maajabu' iliyopasua tairi la mbele na halafu ikamwingia dereva matakoni ni makosa na ni vigumu kuamini!
Yaani huyu lecturer kamgonga mfanyakazi wa hospitali ambayo baadaye ilimuadmit kwa matibabu.
Mi nadhani amestahili kutiwa risasi ya matakoni kwa sababu hakuwa muungwana baada ya kumgonga mpanda baiskeli.