OCD Ajigamba Kumkamata Salum Mwalimu

OCD Ajigamba Kumkamata Salum Mwalimu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
OCD AJIGAMBA KUMKAMATA SALUM MWALIM Naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar Salum Mwalim anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kuzidisha muda kwenye mkutano wake uliofanyika katika viwanja vya mashujaa mjini Mafinga

Mwalimu aliyefika katika viwanja hivyo majira ya saa 11 na dakika 48 alipanda jukwaani saa 11:55 alihutubia mkutano huo hadi saa 12:20 huku jeshi la polisi likiwa limeshaimarisha ulinzi katika eneo la uwanja wa mkutano na kumtaka naibu katibu mkuu huyo kuelekea kituo cha polisi

baada ya maelekezo ya hapa na pale yaliyochukua zaidi ya nusu saa,naibu katibu mkuu huyo alienda kituoni alikohojiwa huku OCD akijigamba kuwa yeye ni kiboko Kwa sababu amewahi kumkamata Mbowe na Tundu Lissu
 
Pole zake OCD huyo. Akitaka ammwangosi kabisa apande cheo kabla ya Oktoba. Kumbe hawajasikia ushauri wa Mzee Lowasa?? Mafuriko kama hayazuiliki kwa mikono sembuse Nguvu ya umma??
 
Mwanahabari Huru

Miezi 4 ijayo huyo ocd atakuwa chini ya utawala wa CHADEMA/UKAWA hivyo serikali makini itaweka mfumo utakaowafanya polisi kutenda majukumu yao kwa Weledi mkubwa na kuacha ushabiki wa kisiasa unaoweza kuleta machafuko.
Huyu ocd ni zao la mfumo mbovu wa ccm unaowafanya polisi kuwa mawakala wa chama tawala
 
Last edited by a moderator:
Ajue Mwezi Nov tunamtimua kazi na kumshitaki kwa kuvunja katiba Nchi mwehu zake huyo
 
Huyo OCD hana cha kujigamba, manake hana tofauti na Mbwa, mwenye mbwa akimwambia mbwa abweke atabweka tu......

Kuikomboa Tanzania tuitakayo hatuna budi kukumbana na vituko kama hivyo!

Hapo umenena Mkuu Mungi acha wamuongezee ujasiri Kamanda Salum Mwalim maana kuelekea oktoba kiengo cha ccm Polisi kitajaribu kuzuia nguvu ya umma japokuwa wanajua hawataweza kupambana na sauti ya Mungu.
 
Huyo OCD hana cha kujigamba, manake hana tofauti na Mbwa, mwenye mbwa akimwambia mbwa abweke atabweka tu......

Kuikomboa Tanzania tuitakayo hatuna budi kukumbana na vituko kama hivyo!

Kumbe mbwa kama hawa bado wapo? Wenzao wanapochinjwa mbona huwa wanaufyata?
 
Mwanahabari Huru

YAAN watanzania tunijisifia mambo ya kipumbav
Sasa kumkamata huyo mwaimu kuna faida gani kwa mustakabali wa taifa?
 
Last edited by a moderator:
Hawa ndio wanaosababisha Tanzania ionekane nchi inayotawaliwa kibabe wakati hata Kikwete mwenyewe hajui kabisa mambo hayo na wala asingetoa amri ya jambo hilo kufanyika. Nadhani hawa wanatafuta vyeo vya kisiasa kwani kuna wakati Tibaigana alipoacha upolisi akawa anatafuta ubunge kupitia CCM.
 
Kumbe mbwa kama hawa bado wapo? Wenzao wanapochinjwa mbona huwa wanaufyata?

Yapo, na yamefikia sifa kama zile za mbwa koko waliozagaa mitaani wanavyofyatuliwa risasi...
 
Double standard ya kipuuzi sana hii,jana kinana mpaka saa 4 usiku.
 
Aonyeshe kweli kama ni kiboko, kwa kumkamata Kinana anayehutubia mpaka saa 4 usiku! Polisi mnatafuta vyeo kwa kuwashughulikia wapinzani! Ovyoooooooooooo!!!!! Poleni, vyeo vya kuhongwa hivyo, vimekwisha, vimebaki vya kuhenyea kihalali!
 
Miezi 4 ijayo huyo ocd atakuwa chini ya utawala wa CHADEMA/UKAWA hivyo serikali makini itaweka mfumo utakaowafanya polisi kutenda majukumu yao kwa Weledi mkubwa na kuacha ushabiki wa kisiasa unaoweza kuleta machafuko.
Huyu ocd ni zao la mfumo mbovu wa ccm unaowafanya polisi kuwa mawakala wa chama tawala
Na akitaka kuthibitisha maneno yako, na awaulize polisi wa Nigeria.
 
Huyo atakuwa mdogo wake Kamuhanda ... R.I.P Mwangosi ... Octoba damu yako itawakomboa watanzania ...

Mwanahabari Huru
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom