Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,098
- 34,914
Rais Barrack Obama
Rais Barrack Obama amesema kuwa ushahidi unaonyesha kwamba ndege ya Malaysia Airline iliokuwa ikisafiri kutoka Amstaderm kuelekea Kuala Lumpur ilitunguliwa na
kombora lililorushwa kutoka eneo linalodhibitiwa na waasi wanaounga mkono Urusi.
Rais Obama amesema kuwa kitendo hicho kinatia hasira na kwamba waasi hao wamekuwa
wakipokea usaidizi kutoka kwa Urusi ikiwemo makombora ya kuangusha ndege.
Obama ametaka usitishwaji wa vita nchini Ukraine ili kutoa fursa ya shirika huru la kimataifa kuchunguza kilichojiri. Chanzo.BBC