kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,943
- 17,359
Hakika chama cha Republican (GOP) kimeshikwa pabaya huko marekani baada ya kushindindwa kwa juhudi zake za kuzuia utoaji wa bima ya afya kwa walalahoi maarufu kama ObamaCare kwa kuzuia bajeti. Chama cha Republican ni chama cha mabepari ambao bei kubwa ya huduma za afya kwa walalahoi ilikuwa miongoni mwa mitaji yao ya kuwafanya walalahoi waende wakafanye kazi kwa mabepari hata kwa bei ndogo ili wapate hela za matibabu ambayo ni ghari sana. Kuwapatia walalahoi wa Marekani (ambao ni wengi) bima ya matibabu (ujamaa) ni kitendo cha kuvunja nguvu za mabepari kwa kuwapunguzia faida nono ya kufa mtu. Hii itawafanya walalahoi wasilazimike kufanya kazi zisizo na maslahi kwa mabepari kwasababu tu ya kutafuta hela za matibabu ghali kwenye hospitali na maduka ya dawa ya mabepari. Hata makampuni ya bima ya mabepari yatapata pigo kubwa kwasababu watu hawatalazimika kujiunga na makampuni yao ambayo ni ghari sana lakini huduma za afya duni. Dawa na huduma za bei rahisi zitaanzishwa ambazo walalahoi watazimudu. Kama mkakati huu wa Obama utakuwa ndiyo sera ya chama cha Democrat katika kupata wapiga kura, basi kuna kila dalili kuwa chama cha republican kikakosa uungwaji mkono na walalahoi na kusababisha kushindwa kwenye chaguzi mbalimbali zijazo, na huo utakuwa mwisho wa Republican kuiongoza Marekani na mwanzo wa kuanguka kwa ubepari mkali huko Marekani. Hivyo Obama atakuwa ameujeluhi ubepari huko Marekani kama vile Gorbachev alivyoujeluhi ucommunist huko USSR (Urusi).
Siku moja mfumo wa Ubepari utakufa na kutoweka kabisa duniani
Siku moja mfumo wa Ubepari utakufa na kutoweka kabisa duniani