Obama kumbe uchawi wake upo kwenye rangi ya nguo

Obama kumbe uchawi wake upo kwenye rangi ya nguo

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,091
Reaction score
34,899


Stori: Mwandishi wetu




UCHAGUZI wa rais nchini Marekani umemalizika, mgombea wa Democrat, Barack Hussein Obama ameibuka kidedea baada ya kumbwaga wa Republican, Mitt Romney.

Rais Barack Hussein Obama akiwa amemkubatia mkewe Michelle Obama
​
Duru za kisiasa nchini humo zinasema kuwa mke wa Rais Obama, Michelle La Vaughn Robinson ni ‘uchawi’ tosha kwa kuwa alichangia ushindi wa mumewe kwa kile kinachotajwa kuwa nyota yake inang’ara ukilinganisha na ilivyokuwa kwa mke wa Romney aitwaye Ann.
attachment.php




...akiwa na familia yake
​
Imeelezwa na mitandao mbalimbali kuwa wakati wa kampeni katika majimbo tofauti, Michelle alishangiliwa zaidi na wapiga kura ikilinganishwa na Ann.
Wataalamu wa mambo ya utabiri walisema nguo alizokuwa akivaa Michelle walizozipa jina la election’s purple power dress (nguo za uchaguzi za rangi ya pinki yenye nguvu) zilikuwa zikisaidia kumfanya mumewe, Obama kuwa na mvuto katika uchaguzi huo.

Wachunguzi hao wanasema hasa nguo ya rangi hiyo ya pinki ambayo Michelle alikuwa akipendelea kuivaa, kiutabiri ilikuwa ikiongeza kung’aa kwa nyota ya Obama katika uchaguzi huo.


Hata hivyo, wananchi walikuwa wakisema wazi kuwa mke wa Obama alikuwa anavaa mavazi ya kilalahoi ukilinganisha na zile za Ann na hata siku ya kutangazwa matokeo alivaa ile ya rangi ya pinki.


Michelle aliwashangaza watu katika moja ya midahalo ya wagombea urais ambapo ‘alivunja sheria’ kwa kumzaba kakofi mumewe, kitendo kilichofanya wasikilizaji kumuiga hali iliyomduwaza mwendeshaji wa mdahalo, Candy Crowley.


Aidha, Obama anatajwa kuwa rais anayeongoza Marekani kwa kumpiga mabusu mkewe mara kwa mara tena hadharani.

Suala la nguo liliibuka tena walipokuwa Chuo Kikuu cha Lynn ambapo mavazi aliyovaa Michelle yalikuwa ya kawaida na

kushangiliwa na watu hasa wanawake ambao inaaminika kuwa ndiyo waliompa kura nyingi Obama.

Obama baada ya kutangazwa mshindi saa 12:30 Jumatano iliyopita aliingia rasmi tena Ikulu ya White House, jijini Washington DC akiwa amefuatana na mkewe Michelle pamoja na watoto wao Malia (12) na Sasha (9) ambapo wataishi kwa miaka mingine minne.
 

Attachments

  • ...akiwa na familia yake.jpg
    ...akiwa na familia yake.jpg
    34.4 KB · Views: 627
Tangu lini rangi purple ikatafsiriwa kuwa pinki kwa kiswahili ? Haya magazeti ya vichochoroni bwana? :madgrin: Hata division zero ni waandishi! purple kwa kiswahili ni zambarau au udhurungi au urujuani! wakati pink ni waridi! Kha, kuna vitu vinakera jamani....
 
Tangu lini rangi purple ikatafsiriwa kuwa pinki kwa kiswahili? Haya magazeti ya vichochoroni bwana? :madgrin: Hata division zero ni waandishi! purple kwa kiswahili ni zambarau! kuna vitu vinakera jamani....

Shule ndugu yangu, wanaweza kupiga picha za akina Weama tu hawaa.....
 
Dahhh magazeti ya bongo jamani ..
Kwa nini mnapenda kusema ama kutumia neno uchawi kupita kiasi ?
 
it seems namba ya watu wanaoamini haya magazeti ya umbea umbea inaongezeka kila kukicha
 
Ni vigumu sana kuwatenganisha baadhi ya watanzania na uchwawi.
 
ujinga ni kushabikia ujinga ukijua kuwa na ujinga na usikemee ujinga
 
Back
Top Bottom