Obama azuru eneo la mashambulizi 9/11 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Obama azuru eneo la mashambulizi 9/11

Discussion in 'International Forum' started by kilimasera, May 6, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Rais wa Marekani Barack Obama amezuru eneo ambalo mashambulizi ya 11 Septemba yalitokea mjini New York.

  Ziara hiyo inafanyika siku nne baada ya kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Al-Qaeda Osama Bin Laden, nchini Pakistan.

  Inaaminika Bin Laden ndiye aliyepanga mashambulizi hayo ya 9/11 mwaka wa 2001.

  Rais Obama aliweka shada la maua kuwakumbuka takriban watu 3000 waliofariki na pia kuzungumza na jamaa zao katika eneo hilo.

  Awali Obama aliwaambia maafisa wa kikosi cha kuzima moto kuwa: ''Wakati tunaposema hatuwezi tukasahau, tunamaanisha vivyo hivyo''.

  Ziara hiyo inakuja siku moja baada ya rais wa Marekani kusema hatachapisha picha ya mwili wa Osama Bin Laden.

  Kiongozi huyo wa Al-Qaeda aliuwawa na vikosi maalum vya jeshi la Marekani kaskazini mwa Pakistan siku ya Jumatatu.

  Baadaye mwili wake ulizikwa kwenye bahari kutoka kwa ndege ya Marekani iliyokuwa imembeba.

  Majeshi ya Pakistan yalikiri kushindwa kugundua alikojificha Bin Laden na kusema wataanzisha uchunguzi.

  Pakistan pia imedokeza kuwa itatizama upya ushirikiano kati yake na Marekani iwapo kutatokea uvamizi mwingine bila ya wao kufahamishwa kama ilivyofanyika na Osama bin Laden.

  BBC Swahili - Habari - Obama azuru eneo la mashambulizi 9/11
   
 2. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Huyu ni raisi Obama akiweka shada la mauwa kwenye viwanja vya jengo la Twin tower palipotokea shambulizi la 9/11.hapo jana.Hii ni siku nne tangu shambulio linaloelezwa lilimuuwa sheikh Osama huko Pakistan.
  Kwani siku hiyo ilikuwa na umuhimu gani mpaka itumike kuweka shada la mauwa?.Afadhali ingekuwa hiyo sept.11.
  Kilichotaka kuoneshwa ni kama tambiko la shukrani kwa kummaliza Osama aliyetajwa ndiye alieyeamrisha kupigwa kwa majengo hayo.
  Jee hii si ni sehemu ya sinema iliyotayarishwa kabla?.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tafakari utupe jibu lako!
   
 4. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni sehemu ya tafakari yangu,kama kuna kitu unapinga au unakubaliana nami sema...

   
 5. rifwima

  rifwima JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Umefikiria weeeeeeee, hilo ndo umeona jambo. Napita tu hapa...manake sioni, sipati wala sihisi mantiki ya ulichokiandika. Kila, kulala, au kuacha kufanya lolote mara nyingine are best options than showing thinking faults here JF. Chukua hatua.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  basi akili za punda
   
 7. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nimefikiria weeeeee,sijapata jibu raisi anapokuwa msanii na raisi anapokuwa fisadi ni yupi afadhali!.
  Yupi anaweza kuiangusha nchi haraka.


   
 8. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu mi nimekuelewa sana!
   
 9. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2011
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ami inaitwa "Closure".
   
 10. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ogopa kucheza mchezo na Amerika kwani mwishowe ni kifo bila huruma.Saddam ilikuwa lazima afe,Osama lazima afe hivyo hivyo na Ghadafi.
  Tatizo limekuja kwa Osama haikuwezekana kuuliwa kiuhalisia mpaka alipokufa mwenyewe popote pale pawapo.Baada uthibitisho kupatikana na Marekani imebidi mchezo wa kumuua ufanyike.Hii ina faida nyingi kwao kama nchi na faida kwa mtu binafsi kama Obama.
  Baada ya hilo kufanyika sasa marekani wanajitekenya na kujichekesha wenyewe.Ati mtandao wa Alqaida umethibitisha kuuwawa kwa Osama!.Wapi huo mtandao upo!.Huu mtandao ni wa mfukumi kama Richmond.
  Nakushauri soma hizi hapa chini uone tabu ya usanii kutetea jambo lolote lile.Unaposoma zingatia utambulisho ya wakazi ndani ya jumba lililoitwa la Osama.
  Osama Bin Laden's Abbottabad Neighbors Noticed Unusual Things
  BBC News - Who was the courier who led US to Osama Bin Laden?

  Mimi nilichokiona ni kuwa kuna mkanganyiko wa maelezo kuhusu tabia za wakazi wa jumba hilo na idadi yao.Wengine wanasema walikuwa hawashirikiani na mjirani,wengine walikuwa wakishirikiana.Inatajwa kulikuwa na watu 12 na mara 23 ni idadi ya watoto tu!.Kwanza ilitajwa vijana wawili waliokuwa wakimsaidia Osama ni watu malofa ndipo wakadhaniwa hawawezi kumiliki lile jumba.Sasa inatajwa humo ndani walikuwa wakitoka watu na SUV mpaka ikadhaniwa ni wafanyabiashara wakubwa wa magendo.
  Vyovyote iwavyo wale wakazi muhimu wameuliwa bila sababu kuficha ukweli na waliobaki watakuwa wafungwa daima kama alivyokuwa Osama mwenyewe.
   
 11. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Closure ndio nini?

   
 12. Wit

  Wit JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 417
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Shekhe wenu Osama aliyekuwa anaongoza jihad ni marehemu,pole Ami
   
 13. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nashukuru kwa pole yako,lakini Osama hakufa May 2.
  Angalia msanii wenu hapo chini,eti anapongeza kikosi kilichomuua Osama !.Mwambie alete picha za marehemu!.

  [​IMG]

  Huyu atapigwa na kufa na maiti ya Osama tu.
   
 14. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Pole Ami, wewe ni Islamist au Islam Fundamentalist? Yote yawavyo, majibu ya imani yako utayapata ahera ukiongezewa na maswali ya kujibu kwa nini hukuamini yaliyokuwa 'kweli' duniani.
   
Loading...