Obama atenga mabiioni kutaka mashoga watambuliwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Obama atenga mabiioni kutaka mashoga watambuliwe

Discussion in 'International Forum' started by sir.JAPHET, Aug 9, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [​IMG]Rais Barack Obama

  Mwandishi Wetu
  MAREKANI imeungana na Uingereza kushinikiza kutambuliwa kwa haki za mashoga, ikitumia rungu la misaada yake inayotoa kwa nchi mbalimbali duniani, huku ikitenga Dola za Marekani 3 milioni sawa na Sh5.1bilioni, kwa ajili ya kufanikisha mkakati huo.

  Shinikizo hilo la Marekani ambalo ni taifa kubwa kiuchumi duniani, linazidi kuchochea mjadala ulioibuliwa na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, ambaye alitangaza katika mkutano wa Jumuiya ya Madola uliofanyika Uswis hivi karibuni kwamba, nchi yake itasitisha misaada kwa nchi zote duniani ambazo hazitambui haki za mashoga.

  Baada ya Cameron, Rais Barack Obama wa Marekani naye juzi alitangaza kwamba, taifa hilo kubwa litatumia uwezo wake wote ikiwamo misaada inayotoa kwa nchi mbalimbali kuhakikisha haki za mashoga zinatambuliwa na kuthaminiwa duniani.

  Rais Obama alitoa msimamo huo jijini Washington katika hafla ambayo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hiyo , Hillary Clinton ambaye ndiye alikuwa mzungumzaji mkuu.

  "Wengine wanasema kuwa haki za mashoga na haki za binaadamu ni vitu tofauti na havifanani, lakini ukweli ni kwamba ni kitu kimoja na chenye usawa,"alisema Clinton wakati akisoma taarifa hiyo maalumu yenye baraka za Obama.

  Clinton alisema, "Tayari tumetenga kiasi cha Dola za Marekani 3 Milioni kwa ajili ya programu ya kutangaza haki za mashoga ili kuondokana na ubaguzi na unyanyasaji dhidi yao."

  Waziri huyo wa mambo ya nje, alisema mpango huo unazitaka nchi ambazo sheria zake bado hazitambui haki za mashoga na kubadilisha sheria hizo ili jamii hiyo ya watu ianze kutambulika.

  "Kwa nchi ambazo watu wanafungwa, kupigwa kutokana na kuwa mashoga ni muhimu viongozi wa nchi hizo, kuangalia jinsi gani wanaweza kukiangalia kikundi hicho cha watu. Si kwamba mashoga hawafanyi makosa, wanaweza kufanya au kutokufanya kama watu wa kawaida, lakini isiwe ni kosa la jinai mtu kuwa shoga,"alisema.
  Kwa mujibu wa Clinton, haki za mashoga ni haki za kimataifa. "Hazina tofauti na haki za binadamu zilizotambuliwa na nchi 48 lililotolewa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

  Naibu Msemaji wa Baraza la Usalama la Marekani, Caitlin Hayden alisema Serikali ya nchi hiyo si kwamba itapunguza au kuzuia misaada yake ya kimataifa ili kubadilisha utamadini wa nchi nyingine, bali inataka kuhakikisha haki za mashoga zinapewa pia kipaumbele.

  Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Obama kujitokeza hadharani na kutetea haki za mashoga, lakini aliwahi kupitisha sera iitwayo " don't ask, don't tell" ikimaanisha "usiulize, usiseme" ambayo inawazuia mashoga kujiunga na kufanya kazi za jeshi kwa uwazi.

  Mmoja wa viongozi wa Republican ambaye atawania nafasi ya Urais, Gavana Rick Perry alisema Obama kwa mara nyingine amewakosea Wamarekani kwa aina tofauti ya maisha yao kwa kuingiza aina hiyo ya maisha kitu ambacho mtu kama yeye Perry hawezi kukifanya.

  Kauli hiyo ya viongozi wa Marekani inaonekana kuungana na ile iliyotolewa na Cameron aliyesema, "Hii ni moja ya vitu vinavyoongoza sera yetu ya misaada kwa mataifa mbalimbali na tayari tumeanza kuitekeleza katika maeneo kadhaa.
  MIMI SITAAAKI TABIA MBAYAA IJE BONGO,, TAFADHALIIIII SISI SIO MALAWIII NI WATANZANIA USHOGA NA USAGAJI MARUFUUKUUUKU,, FULL STOP
   
 2. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  If they support democracy in different countries, it is time to vote for homosexual acceptance in the country. If a large number of people will vote for homosexuality, they can impose what they are saying. Otherwise, they are contradicting themselves about democracy and their interests.So far, a large number of Africans do not want homosexuality, why are they forcing us?. We need better hosipitals, better schools, better infrastructure, etc, which can be boosted with these 3 millions dollars instead of emphasizing and encouraging sins and biological hammering to people with physiological problems. Homosexual is a physiological issues which need only guidance and counseling to sort it out. Why are these people forcing us?
   
 3. S

  Sessy Senior Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tumekwisha sisi omba omba ....huyu raisi ambae kila siku mguu na njia usa kuomba atakataha hili sijui .....mungu atusaidie
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Huyu Obama lazima kuna wadudu wanamtekenya kwenye makalio siyo bure!
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,200
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Sasa Yule mwenyekiti wa Chama cha mabwepande akienda marekani lazima ajiandae na zana za kuvaa
   
 6. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Msimamo wetu uko wazi. Wazipeleke Malawi ambako wanahitaji na hata watu wake kupata kuoana. Sisi tulishaweka wazi msimamo wetu na hatutageuka nyuma.
   
 7. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  not easy as u think.......unaijuwa sunami ww?? haizuiliki
   
 8. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  nadhani pia lazima atakuwa mke wa mtu huyo, sio bure.
   
Loading...