Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Rais Barack Obama wa Marekani amesema wamarekani wote wanapaswa kuguswa na tukio la kuuawa kwa kufyatuliwa risasi watu wawili weusi wiki hii nchini humo. Obama ambaye yuko nchini Poland kuhudhuria mkutano wa kilele wa jumuiya ya kujihami ya NATO amesema kuna haja ya kufanyika mageuzi katika jeshi la polisi nchini humo.
Jumatano wiki hii mtu aliyetambuliwa kwa jina la Philando Castile mwenye umri wa miaka 32 aliuawa kwa kupigwa risasi katika jimbo la Minnesota ambapo rafiki wa kike wa mtu huyo aliyeuawa aliyekuwa naye katika gari alituma picha za tukio hilo katika mitandao ya kijamii.
Siku moja kabla mtu mwingine aliyetambulika kwa jina la Alton Sterling mwenye umri wa miaka 37 aliuawa baada ya kufyatuliwa risasi na polisi katika mji wa Baton Rouge ulioko katika jimbo la Lousiana.
Chanzo : DW