Rais wa Marekani Barack Obama amekubali kwamba alifanya kosa kuhusu uteuzi wa baraza lake la mawaziri .
Wawili kati ya wanasiasa aliowateua kutoka chama chake cha Democratic, walitiliwa mashaka kuhusu uaminifu wao binafsi katika ulipaji kodi.
Hatimaye Wanasiasa hao wawili; Seneta Tom na Bibi Nancy, waliamua kukataa kupokea nyadhifa walizopewa kutokana na tuhuma za kutokuwa waaminifu katika ulipaji kodi zinazowahusu wao binafsi.
Tunajifunza nini kwa nchi zetu za Afrika?