Sokoro waito
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 2,200
- 2,603
Hamjambo wana MMU,
Migogoro ya ndoa inaongezeka kwa kasi sana maana maarifa mbalimbali yanaongezeka kwa kasi kubwa.
Ndivyo mwanamme pia unahitaji maarifa ya kutosha angalau uanze kutengeneza familia imara kwa ajili ya ustawi wa taifa letu.
Tukubaliane tu kwamba Mola alipotuumba alituwekea karama mbalimbali katika nafsi zetu za kutusaidia kuishi vizuri na watu au kukabiliana na mazingira yanayotuzunguka.
Mwanamme yeyote anasisitizwa kuishi na mke wake kwa AKILI. Akili inayozungumziwa hapa siyo elimu wala ubongo, bali ni uwezo wa kutambua jinsi ya kuishi na mke uliyenaye kulingana na jinsi alivyo kwa kumsaidia kuacha yanayokukera pasipo kukwaruzana mara kwa mara.
Kwa mfano: AKILI YA KUHUDUMIA NA KUTUNZA FAMILIA.
Kama mwanamme unajua kabisa uwezo wako wa kiakili katika kutunza na kuhudumia familia ni mdogo sana haijalishi umesoma hadi kidato gani, sasa unaoa mwanamke wa nini? Wakati hata kuhudumia mkeo roho inauma!
Unaoa halafu nani akutunze kama mwanamme unajua kabisa uwezo wako wa kiakili katika kutunza na kuhudumia familia ni mdogo sana haijalishi umesoma hadi kidato gani, sasa unaoa mwanamke wa nini? Wakati hata kuhudumia mkeo roho inauma! Unaoa halafu nani akutunzie?
Ukweli tu ni kwamba akili anayotumia mwanamme fulani kuishi na mkewe ni tofauti na akili atakayotumia mwanamme mwingine kuishi na mkewe haijalishi hao wake zao wote wamezaliwa tumbo moja ama wana elimu inayofanana au wote hawana elimu.
Mfano wa pili:
Mwanamme unajua kabisa uwezo wako wa kiakili ni mdogo au IQ yako ni ndogo sana kuishi na mwanamke fulani ambaye ktk uchumba umegundua siyo wa mchezo mchezo, ana akili ambayo itakufanya ujidharau kila mara na kujiona dhaifu au hufai kuwa baba wa familia.
Unamuoa wa nini? Mwachie aolewe na mwanamme mwenye akili ya kuishi na wanawake wenye akili kubwa.
Tafadhali tafuta size yako, acha kujifurahisha kwenye hamna.
Chagua saizi yako kulingana na AKILI YAKO.