Ndiyo chaguzi za Afrika, Kenya enzi za Moi marehemu wengi sana walimpigia kura, ni mpaka yeye mwenyewe aliporidhia kuondoka madarakani lakini hakuondolewa kwa sandukuwla kura.
Ujue unapoiga jambo ni lazima utalizidisha au utalipunguza,yaani kama Frelimo wamejifunza kufanya figisu kutoka CCM basi naweza amini wamewapita.
Mwaka 2017 ilifanyika sensa ya Taifa kuna jimbo linaitwa Gaza hii ndio ngome ya Frelimo,Frelimo kupitia Tume ya uchaguzi ikaongeza idadi ya wapiga kura ili kupata wabunge wengi zaidi,hawa watu wa sensa wakaikataa idadi ya tume ya uchaguzi kwa kusema idadi hiyo itapatikana kuanzia 2040 kwa kuwa wakazi wengi wana umri chini ya miaka 18,hii yule mwenyekiti wa sensa akajiuzulu kwa kuipinga idadi hii ya tume ya Taifa ya uchaguzi na msaidizi wake akauliwa wakati wa kampeni.
Na hapa ndipo wapinzani walipokosea kwa kuamua kwenda kwenye uchaguzi wakati figisu wameziona live bila chenga na hapo ndipo kukatokea tena kutoaminiana wanachama ndani ya Renamo,wapo waliomuona Ossufo Momade ni msaliti na kitengo cha askari wa Renamo kikiongozwa na Mariano Nhongo kuasi na kutomtambua kiongozi wao.
Hii nayo inataka kutokea Tanzania ambapo Rais kashatangaza kuwa wapinzani wasitangazwe washindi,sasa sijui wanashiriki uchaguzi wa kazi gani😇
Nchini Msumbiji uchaguzi wa wabunge,huwa kinachaguliwa chama na sio mtu,yaani iko hivi mtagombania wenyewe ndani ya chama chenu na atakayepata kura nyingi ndiye atakuwa mbunge (mfano: ccm ndani ya chama wanaogombania jimbo la Ubungo na matokeo ni hivi
1.Edward Simjui 1000
2.Filomena Ndimu 880
3.Abdala Miyeyusho 610
Cuf nao wakafanya uchaguzi wao wa ndani na mshindi namba
1.John Tindo 1000
2.James Fungo 879
3.Mwanaidi Nyau 617
Chadema wakafanya uchaguzi wao wa ndani na washindi wakawa hivi
1.Eliza Shayo 1000
2.Kasim Mwanakwetu 86
3.Asha Ndalandefu 69
Tuchukulie ccm ndio kashinda kwenye jimbo la Ubungo ina maana
Edward Simjui ndiye anakuwa mbunge na ikitokea kwa namna yoyote akaacha kuwa mbunge basi ina maana namba 2 bi
Filomena Ndimu ndiye atakayechukua nafasi yake,hapa hata mbunge akiamua kuunga mkono juhudi basi chama hakipotezi mbunge wala diwani kwa kuwa uchaguzi hautorudiwa.
Uchaguzi pekee utakaorudiwa ni Rais au meya. Meya atakapoacha umeya kwasababu yoyote ile mtu kutoka chama chake ndiye atakayekaimu nafasi na baadae kutajwa tena kwa siku uchaguzi,style yao ni nzuri kwenye kupunguza pesa za kufanya uchaguzi wa marudio,hawataki kusikia mara mtu kupita bila kupingwa na figisu nyenginezo.
Nalog off