Nyumba za serikali zilizouzwa

wuhulo

Member
Feb 20, 2016
28
8
1. Ziliuzwa kwa bei ndogo sana ukilinganisha na thamani yake pamoja na kiwanja chake.

2. Hakukuwa na sababu ya msingi sana iliyopelekea nyumba zile ziuzwe.

3. Watumishi wenye sifa ya kuishi katika nyumba za serikali wamekosa fursa hiyo na hivo kuishi katika hotel kwa gharama ya serikali ambapo fedha nyingi zinatumika.

4. Gharama zinazotumika kwa watumishi hao kuishi hotelini zingeweza kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi wa vipato vya chini katika afya, elimu na maji.

5. Nyumba kama zilizokuwa za Polisi aafu zikauzwa, ziko karibu kabisa na vikosi vya polisi jamnbo ambalo ni hatari sana kwa usalama wa vituo hivyo.

6. Je, Hili siyo jipu? Nani wa kulitumbua sasa.
 
Usiandike vitu vya kubuni au fikra zako !! Fanya utafiti kwanza!!
Mfano hakuna hata nyumba moja ya polisi iliyouzwa, au usalama wa Taifa au za madaktari wa mikoa na wilaya!!
 
Usiandike vitu vya kubuni au fikra zako !! Fanya utafiti kwanza!!
Mfano hakuna hata nyumba moja ya polisi iliyouzwa, au usalama wa Taifa au za madaktari wa mikoa na wilaya!!
Mwambie huyo. Anaropoka tu mambo ambayo hayajui
 
Usiandike vitu vya kubuni au fikra zako !! Fanya utafiti kwanza!!
Mfano hakuna hata nyumba moja ya polisi iliyouzwa, au usalama wa Taifa au za madaktari wa mikoa na wilaya!!
Hahhhahahhaaaa hiyo ya mwisho nakataaa kwa nguvu zangu zote, nenda Lushoto pale nyumba za hospital zote za miaka ya nyuma wameuziana kwa bei ya kutupa
 
1. Ziliuzwa kwa bei ndogo sana ukilinganisha na thamani yake pamoja na kiwanja chake.

2. Hakukuwa na sababu ya msingi sana iliyopelekea nyumba zile ziuzwe.

3. Watumishi wenye sifa ya kuishi katika nyumba za serikali wamekosa fursa hiyo na hivo kuishi katika hotel kwa gharama ya serikali ambapo fedha nyingi zinatumika.

4. Gharama zinazotumika kwa watumishi hao kuishi hotelini zingeweza kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi wa vipato vya chini katika afya, elimu na maji.

5. Nyumba kama zilizokuwa za Polisi aafu zikauzwa, ziko karibu kabisa na vikosi vya polisi jamnbo ambalo ni hatari sana kwa usalama wa vituo hivyo.

6. Je, Hili siyo JIPU ? Nani wa kulitumbua sasa.
nashukuru nami niliambulia kaappatment kwa 6m na kwakuwa me wa mujini nimekapiga bei faster nikalamba 68m nikajenga yangu ya halali tena ya hajja uspime
 
Muulize Sumaye ambaye ndiye aliyefanya maamuzi ya kuuza hizo nyumba. Maelezo anayo ya kutosha. Kama ni jipu basi atumbuliwe yeye
CCM hii cheap labour yenu ya mtandaoni muipige chini na badala yake huyu mtu mpeni kazi ya kuosha magari ya chama na kufuta vumbi maofisini hapo Lumumba.Kwa hizi hoja ni wazi kazi hii imemshinda.
 
Usiandike vitu vya kubuni au fikra zako !! Fanya utafiti kwanza!!
Mfano hakuna hata nyumba moja ya polisi iliyouzwa, au usalama wa Taifa au za madaktari wa mikoa na wilaya!!
Wewe ndiye hufanyi utafiti, njoo Mpwapwa nyumba ya OCD kauziwa askofu Chiwanga na iko kwenye eneo la polisi unatoka tu unaenda hatua chache unaingia kituoni.
 
CCM hii cheap labour yenu ya mtandaoni muipige chini na badala yake huyu mtu mpeni kazi ya kuosha magari ya chama na kufuta vumbi maofisini hapo Lumumba.Kwa hizi hoja ni wazi kazi hii imemshinda.
Kwani wewe ulitaka nicomment vipi? Suala la uuzwaji wa nyumba lilishatolewa ufafanuzi na Sumaye. Hata wewe mburula wa Ufipa unajua hilo
 
Waliouziwa pia wamekiuka mikataba yao.
Akiwemo Apson Mwang'onda ambaye ameuza nyumba yake iliyopo Oysterbay mtaa wa Laiboni kwa bilioni 10 kuchangia harakati za Lowasa kwenda Ikulu. Imekula kwake. Nyumba kauza na alichokitafuta kakikosa
 
Hata ya kwangu nilitaka kuiuza lakini JPM alipoingia madarakani nimesitisha mpango huo.
 
lushoto mbali sana hapo DSTV nyuma watu wameuziwa nyumba mil7 miaka ya tisini,nyumba ina uwanya kama wa mpira,we acha tu
Hahahahaaaa halafu huyo jamaa hapo juu eti anakataaa, mi nakumbuka nillititwa nyumba huko maeneo ya Bahari beach ila nikaogopa aiseee.
 
Usiandike vitu vya kubuni au fikra zako !! Fanya utafiti kwanza!!
Mfano hakuna hata nyumba moja ya polisi iliyouzwa, au usalama wa Taifa au za madaktari wa mikoa na wilaya!!
Vipi ile nyumba wanayogombea Kova na yule Mkuu wa kikosi cha kupambana na dawa za kulevya pale Arusha ilikuwa ya idara gani? Wewe unakurupuka bila kuelewa chochote kwa kuwa tu unashabikia upuuzi.
 
Tutalalamika mengi sana WaTanzania, na majipu hayataisha! La msingi - tulijikwaa wapi? Na je kuna mwelekeo wa kusimama imara tena?
 
Usiandike vitu vya kubuni au fikra zako !! Fanya utafiti kwanza!!
Mfano hakuna hata nyumba moja ya polisi iliyouzwa, au usalama wa Taifa au za madaktari wa mikoa na wilaya!!
Shame upon you!Nyumba inayogombaniwa na Suleman Kova na mwenzake Pale high Court Arusha ni choo kile,inaoneka wewe hata habari huangalii,magazeti husomi?shame ! Za usalama wa Taifa pale moshi imeuzwa na mmiliki aliponunua akahamishiwaa manyara ,alipokuja Afisa mwengine ikabidi akae Hotelin,Kwa Dar ndo usiseme,heko JKikwete alikataa,Mstaafu kamishna wa magereza Komba kanunua nyumba ina hekari mbili pale Oysterbay ina swimming na uwanja wa basket wakati ye mwenyee alishajenga ya kustaafia!!Jaji Mwenzangu Kitusi kanunua moja Ipo Moshi inatazana na hospitali ya Moshi Arusha,Jaji Mchome kanunua ipo jirani na mkuu wa mkoa Kilimanjaro,Eeh Mungu hata kizazi na kizazi kipite ,hizo nyumba zitarudi tu!Yaani jaji anayepewa maslahi mpaka kufa kwake kwa mujibu wa sheria alaf anapewa nyumba kwa mil 5!Tena nikwambie kitu,Nyumba za oysterbay Komba aliinunua kwa Mil 20,baada ya hapo watu wanaotaka kwa Mil 800 na amekata ,Juzi kuna mdosi anaitwa Baghdad kapanda mpaka Bil 2 na bado hauzi,sasa kama serikali waliona hazina haja wangeuza kwenye open market
 
lushoto mbali sana hapo DSTV nyuma watu wameuziwa nyumba mil7 miaka ya tisini,nyumba ina uwanya kama wa mpira,we acha tu
Magufuli aweka kiporo uuzaji nyumba Mwandishi Wetu Toleo la 424 23 Sep 2015 MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, ameweka kiporo baadhi ya maswali likiwamo kuhusu uuzaji wa nyumba za serikali, kazi aliyoisimamia akiwa Waziri wa Ujenzi, katika Serikali ya Awamu ya Tatu. Magufuli aliweka kiporo kujibu maswali hayo yaliyoelekezwa kwake wakati wa mahojiano maalumu yaliyofanyika mjini Tabora, Septemba 15, mwaka huu. Mahojiano hayo yalichapishwa Jumatano wiki iliyopita, katika Gazeti la Raia Mwema. Mbali na swali kuhusu uuzaji wa nyumba za serikali, maswali mengine aliyoahirisha kuyajibu ni pamoja na kuhusu gharama kubwa za ujenzi wa barabara nchini ikilinganishwa na baadhi ya nchi, sambamba na ubora wa barabara hizo. Swali hilo la nyumba, ambalo ni sehemu ya maswali 11 kwake liliuliza; “Suala la uuzaji wa nyumba za serikali ambalo limetekelezwa katika wakati ambao ukiwa Waziri wa Ujenzi bado gumzo na limekera Watanzania wengi. Unasemaje kuhusu hili?” Kutokana na maswali hayo ambayo yalitangulizwa kwa Magufuli takriban wiki moja kabla ya mahojiano rasmi, maswali husika hayakujibiwa kwa maelezo kwamba yatajibiwa na Magufuli katika mahojiano yatakayopangwa wakati mwingine. Uuzaji wa nyumba za serikali ulitekelezwa katika uongozi wa Rais Benjamin Mkapa na nyumba zaidi ya 8,000 ziliuzwa, baadhi zikiwa zimejengwa katika maeneo nyeti. Inadaiwa kwamba katika uuzaji huo wa nyumba, Magufuli aliingilia mchakato wa uuzaji ambao unatajwa ulipaswa kusimamiwa moja kwa moja na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA). Katika uingiliaji huo, Magufuli anadaiwa kufanikisha uuzaji wa mojawapo ya nyumba hizo za kwa Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo anayedaiwa kuwa ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao. Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa serikali na si Waziri wa Ujenzi wa wakati huo. Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee TBA ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote. Kwa mujibu wa sheria hiyo, waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake. Katika mauzo hayo ya nyumba, serikali inatajwa kutarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00, lakini taarifa zilikuwa zikionyesha kwamba imepata shilingi 22,684,108,115.08. Miongoni mwa nyumba zinazomilikiwa na serikali kwa sasa ni 1,098 zinazosimamiwa na TBA, kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari. Katika bajeti ya mwaka 2010/2011, serikali, kupitia Wizara ya Ujenzi iliwasilisha bajeti yake bungeni mjini Dodoma na kueleza kwamba inataraji kutumia takriban Sh bilioni 5.7 kujenga nyumba mpya ili kuokoa mamilioni yanayotumika kuwalipia watumishi wanaolazimika kukaa hotelini kwa kukosa nyumba. Hata hivyo, kiasi hicho cha fedha kilichotengwa kwa wakati huo ni pungufu ikilinganishwa na kile kilichotengwa awali, katika bajeti iliyotangulia ya 2009/2010, Sh bilioni 11.4 kwa ajili ya ujenzi huo wa nyumba. - See more at: Raia Mwema - Magufuli aweka kiporo uuzaji nyumbaRaia Mwema - Magufuli aweka kiporo uuzaji nyumba
 
Back
Top Bottom