Nyumba za nssf bei ya chini millioni 200

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,058
2,000
NYUMBA 215 zilizojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kuwauzia wanachama wake kwa bei nafuu eneo la Kijichi Dar es Salaam hazikamatiki baada ya gharama halisi anayotakiwa kulipa mwanachama kuwa kati ya Sh200 milioni na Sh260 milioni.
Benki ya Commercial Bank Of Afrika (CBA) ilidokeza hayo jana ilipokuwa ikitoa utaratibu wa kupata mkopo wa kununua nyumba hizo kupitia benki hiyo baada ya kuteuliwa na NSSF kuwasaidia mikopo wanachama waliotimiza masharti ya wali kununua nyumba hizo.

Ofisa wa CBA (jina lake linahifadhiwa) alimweleza mwanachama wa NSSF aliyefika kujua utaratibu wa kupata mkopo wa kununua nyumba hizo kwamba pamoja na NSSF kuwaeleza wanachama wake kwamba nyumba zitauzwa kati ya Sh90 milioni na Sh118 milioni, ukweli ni kwamba gharama halisi ni kati ya Sh200 milioni na Sh260,000 kulingana na hadhi ya nyumba.

“Kwa mfano nyumba za 3A-3 zenye vyumba vitatu ambazo NSSF ilisema inahitaji Sh90 milioni, gharama halisi ni Sh214,500,000 zinazojumuisha gharama mbalimbali za mkopo utakaolipwa kwa miaka 20,’’ alisema ofisa huyo.

Alisema utaratibu wa kupata mkopo ni kwamba CBA inatoa asilimia 90 ya bei halisi na kwamba riba ni asilimia 19.5 huku mkopaji akitakiwa kukatwa asilimia 45 ya mapato ya mkopaji kila mwezi.

“Ukitaka nyumba ambayo NSSF inataka irudishiwe Sh90 milioni, basi utakuwa ukikatwa Sh1.45 milioni kila mwezi ili kurudisha mkopo kwa muda wa miaka 20,’’ alisema.
Mbali ya gharama ya riba kufikia Sh214.5 milioni katika kununua nyumba hiyo, lakini mteja pia atatakiwa kugharimia masuala ya kisheria, uthamini wa nyumba, uwezeshaji, na kuingia kwenye bima.
 

omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,322
2,000
nimemuona Mchechu wa NHC anasema pale Mchikichini, Ilala wanajenga nyumba za watu wenye kipato cha chini (wanyonge wa Tanzania) na bei yake ni Tsh. 100,000,000/- (milioni mia moja za Kitz na sio za Zimbabwe au Somalia).
Mimi sikuwa na taarifa kuwa status ya wanyonge sasa ni million hizo zote, sijui ndio ukuuaji wa uchumi wanaousema ulio uplift equity ya Mtz!!
Hizi nyumba zaidi ya 95% inabidi tuwaachie mafisadi wazinunue kwa majina yetu alafu waje kutupangisha
 

Gerad2008

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
583
500
Hizo za wahindi. Watanzania sio wajinga kiasi hicho kwani ukiwa na mil.200 hapa arusha unapata kiwanja sehemu nzuri kwa tshs 50mil. Na unajenga nyuma ya kisasa kubwa mara mbili ya hizo fake za nssf pamoja na sehemu kubwa ya parking ya magari 5 na ya kulima mboga.
 

kiparah

JF-Expert Member
Sep 7, 2010
1,173
0
Tanzania kuna wakati inanifurahisha mno. Eti nyumba za walala hoi milioni 100!!! Hivi huyo mlalahoi ni nani vile??? Kama mlalahoi anaweza kuwa na kiasi hicho cha fedha neno MLALAHOI halina maana, labda itafutiwe maana nyingine!!!
 

omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,322
2,000
Hizo za wahindi. Watanzania sio wajinga kiasi hicho kwani ukiwa na mil.200 hapa arusha unapata kiwanja sehemu nzuri kwa tshs 50mil. Na unajenga nyuma ya kisasa kubwa mara mbili ya hizo fake za nssf pamoja na sehemu kubwa ya parking ya magari 5 na ya kulima mboga.
Mzee Mtikila alisema "saa ya ukombozi ni sasa" na ilikuwa zaidi ya miaka 15 iliyopita na wengi either walimpuuza lakini kwa hakika mawazo kama yako mkuu yanaonyesha wazi kuwa ukombozi ulio muhimu zaidi ambao ni wa kifikra unaanza kusaambaa kwa wengi. Asante kwa ufafanuzi mzuri
 

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,058
2,000
tatizo liko wapi?

mkuu ujaona tatizo? wanasema wamejenga nyumba za wanyonge,kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kumiliki nyumba,na hio bei unaona zinaendana? je kweli nyumba za wanyonge,au wanyongaji !!
 

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,908
2,000
Tanzania ni nchi bepari!!! Hivi ni nani huyo descent employee mwenye kuweza kununua nyumba cash at 100m or mkopo wa kukunyonyoa manyoya? Inasikitisha sana.
 

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,058
2,000
Tanzania kuna wakati inanifurahisha mno. Eti nyumba za walala hoi milioni 100!!! Hivi huyo mlalahoi ni nani vile??? Kama mlalahoi anaweza kuwa na kiasi hicho cha fedha neno MLALAHOI halina maana, labda itafutiwe maana nyingine!!!

inaonekana tanzania hakuna walalahoi,kwa mtindo huu wananchi wa tanzania wana uwezo sana,kama mlalahoi anaweza afford nyumba ya million 100-200 je wenyewe wanyongaji aka wenye nchi
 

Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
9,380
2,000
Millioni 100! Mmmh...walalahoi hatuna chetu,inadhihirisha ni jinsi gani mafisadi wanavyokumbukana wenyewe,ina maana kweli wameshindwa kujenga nyumba nafuu kwa mtanzania wa kawaida? Hatutaki mbwembwe nyumba ya kawaida tu ambayo angalau na sisi tutasema katika yale mahitaji muhimu,hili la sehemu ya kulala angalau!
 

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,058
2,000
Millioni 100! Mmmh...walalahoi hatuna chetu,inadhihirisha ni jinsi gani mafisadi wanavyokumbukana wenyewe,ina maana kweli wameshindwa kujenga nyumba nafuu kwa mtanzania wa kawaida? Hatutaki mbwembwe nyumba ya kawaida tu ambayo angalau na sisi tutasema katika yale mahitaji muhimu,hili la sehemu ya kulala angalau!

mlalahoi na million 100-200 ni kama ndoto anaota,kwake ni miujiza,sasa sijui wametumia vigezo gani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom