Nyumba za kupanga ni degree tosha

ZINDAGI

JF-Expert Member
Dec 5, 2015
1,117
1,424
Ili kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu" Baba Ushakua, Jitegemee" nilienda kupanga chumba huku maeneo ya Tandale.

Nyumba ina vyumba 16, vinane nyumba kubwa na 8 mabanda ya uani, choo kimoja cha uani na hakijaezekwa, mlango wa bati

Nakumbuka siku moja wakati nipo chooni, mvua kubwa ikanyesha, ikabidi nibaki humo nalowa tuu maana sikuweza kutoka kwa wingi wa mvua.

Matukio ni mengi mno kiasi kwamba unajifunza mengi kutoka kwa watu mbali mbali ambayo kwa kweli yanakukomaza akili.

Je wewe yapi umeyapitia?

Kula kulala huruhusiwi kuchangia
 
Kuna nyumba nilipanga mmiliki alikua Mmama mswahili kupitiliza na alikua anaishi hapo na anategemea hiyo nyumba kwa maisha yake. Sasa ole wako ucheleweshe kodi hata wiki hapo utaujua mdomo wa mndengereko. Akikukuta unakunywa biere halafu usimpe ofa utamjua mndengereko.
 
Back
Top Bottom