Elitwege
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 5,154
- 10,809
Kama unaishi nyumba za kupanga zenye masharti lukuki hii inakuhusu sana, wataalamu wa afya ya akili na wanasaikolojia wameonya kuwa masharti hayo ni moja ya kichocheo cha mtu kukumbwa na magonjwa ya afya ya akili ikiwemo sonona.
Takwimu za magonjwa ya afya ya akili kwa mwaka jana kutoka Wizara ya Afya zinaonyesha Watanzania milioni saba wana matatizo ya afya ya akili, huku Mkoa wa Dar es Salaam ukionekana kinara na idadi kubwa ya watu wenye matatizo hayo.
Kauli ya wataalamu hao inakuja wakati Debora Maiko mkazi wa Mbezi Afrikana Dar es Salaam, akisimulia mama mwenye nyumba wake kumkataza kuamka alfajiri kabla yake na wakati mwingine haruhusiwi kutoka ndani hadi mama huyo amwage maji barazani.
Akizungumza hivi karibuni na Mwananchi Debora alisema jambo la ajabu katika mkataba mama huyo hakuainisha masharti hayo, pia hakuna mpangaji anayeruhusiwa kupiga nyimbo za dini au kutoka nje kabla ya mama huyo kuamka.
Alisema kunapotokea hali ya kukiuka utaratibu huo, mwenye nyumba hutishia kusitisha mkataba kwa madai kuwa mtenda tukio anamuharibia mambo yake.
Kauli ya Debora ianungwa mkono na Sophia Urasa mkazi wa Mabibo anayeshangazwa na masharti ya jirani yao asiyepangisha vijana waliooa ndani ya nyumba yake au familia yenye mtoto mchanga kuishi kwake.
Daktari Idara ya Afya ya Akili, kutoka Hospitali Rufani Kanda ya Mbeya, Dk Raymond Mgeni alisema vitisho na masharti kandamizi anayotoa mmiliki wa nyumba kwa mpangaji wake humsababishia mpangaji kupata msongo wa mawazo ambao huchangia mtu kuingia katika kundi la magonjwa ya akili ikiwemo sonona.
“Mwenye nyumba anapoweka masharti magumu bila kufahamu aina ya watu anaowapangisha aidha ni wanafunzi, mtu mwenye kipato chenye kutia shaka, anayepitia changamoto ya mahusiano au kodi kwa pamoja vinamuingiza mtu huyo katika sonona,’’ alisema.
Nyumba za kupanga zinavyoharibu akili | Mwananchi - Nyumba za kupanga zinavyoharibu akili