Nyumba ya miti na nyasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba ya miti na nyasi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by CHE GUEVARA-II, Sep 1, 2011.

 1. CHE GUEVARA-II

  CHE GUEVARA-II JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 531
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Hi, habari zenu?
  Ushauri wenu, maoni yenu ni muhimu kweli!!!!!!!!!!

  Nikitaka kujenga nyumbaya kuish mimi, mke wangu na mtoto wangu kama hii (AmazingPlans.com House Plan #1885C-SLM - 1885 Square Feet, 3 Bedrooms, 2 Full Bathrooms, Colonial, Contemporary, Country, Hillside, Ranch, Southern, Traditional, Victorian) kwa mbao na miti kama ile wanayojengea maukumbi ya starehe kama baa, pubs n.k, pia niifanye iwe thatched house (nyumba ya nyasi au makuti) na ile bonus house niijenge kwa mbao na miti pia, nayo iwe thatched. Sitaki kuweka ceiling board, nataka mapambo ya paa lenye nyasi yawe yanaonekana na pia nataka sakafu ya bonus room iwe ya mbao, siyo ya cement - itanigharimu sh. ngapi? Architects please, msaada wenu jamani. Mbao nitatoa huku maporini Liwale (niko Mtwara) na miti au nguzo nitanunua Dar au hata Iringa. Makuti yanapatikana huku kwa wamakonde.

  Nikishajua gharama na nikaona si mbaya sana, kama kuna mdau wa maufundi hayo (Archtect), nitaomba tuongee naye!

  Asanteni
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Unataka kutukoroga hapa. Ni kweli nyumba kana hizo za miti kama inayoonekana pichani ni nyumba mamilioni kwa mamilioni zilizojengwa nchi zilizoendelea kwa gharama nafuu, lakini kwao zina manufaa kutokana na hali ya hewa. Kwa usalama katika nchi zetu nyumba za aina hiyo si imara kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Wao hata nyumba ya 4-5 compartment apartments zaidi ya 200 hujenga kwa mbao lakini kwa nchi yetu si kitu cha kuiga. Yakitokea mafuriko au mvua za upepo utajutia kupoteza nyumba yako kwa sababu ya sasa unapofikiria kupunguza gharama za ujenzi. Tofali na blocks za cement na kuezekwa kwa bati inachukua muda kushika moto tofauti na iliyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa makuti.

  Kwenye mchoro wa nyumba uliyoonyeshwa haijaezekwa kwa nyasi bali ni kwa plastic iliyochanganyika na masalilia ya makaratasi na udongo fulani.
   
 3. CHE GUEVARA-II

  CHE GUEVARA-II JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 531
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Ingekuwa tunalipia kodi maneno tunayoongea, wengi tungekuwa mabubu (ingekuwa inakula kwetu)!

  Asante kwa ushauri!
   
 4. u

  ureni JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Tujuze mkuu ni kwa nini unataka kujenga nyumba ya mbao na miti na sio ya tofali na cement?
   
 5. CHE GUEVARA-II

  CHE GUEVARA-II JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 531
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Napenda vitu vya asili!
   
Loading...