Nyumba ya mil. 89/- yamtatiza DC

Nyumba ya mil. 89/- yamtatiza DC

lidoda

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2008
Posts
641
Reaction score
576
View attachment 195418

Nyumba ya mil. 89/-MIRADI ya ujenzi katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imeghubikwa na tuhuma za ufisadi, ambapo hivi karibuni imekabidhiwa nyumba ya mwalimu yenye vyumba viwili vya kulala na sebule, ikitajwa kugharimu sh. milioni 89, jamba ambalo limeibua utata na kumlazimu Mkuu wa wilaya hiyo, Elibariki Kingu kuingilia kati.

Gharama ya ujenzi wa nyumba hiyo katika shule ya sekondari Ichama kata ya Chabutwa ni sehemu ya matumizi ya kiasi cha sh. milioni 219 zilizotolewa na Serikali kuu kupitia mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumatano, umebaini kuwa mbali na kiasi hicho pia katika muendelezo wa matumizi ya fedha hizo, sh. milioni 8.6, zimetumiwa kwa ajili ya kujenga tanki la kuvunia maji ya mvua katika nyumba hiyo, hali inaibua maswali kwa wakazi wa Chabutwa kutokana na ubora wa nyumba yenyewe na gharama zinazotajwa kutumika.

Kutokana na utata huo, tayari mkuu wa wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu, ameingilia kati na kutaka malipo ya mradi huo yasitishwe huku akiagiza wataalam wa halmashauri kufanya tathmini upya kuthibitisha kama thamani ya fedha inalingana na ubora wa nyumba.

Oktoba 8 mwaka huu, wakati kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Rache Kasanda akiikagua nyumba hiyo ya mwalimu baada ya kuifunga, alisikika akisifia kuwa ni bora kwa kile alichoeleza kuwa haina dalili yoyote ya nyufa.

Gazeti hili lilipomhoji juu ya gharama zilizotajwa katika taarifa ya halmashauri kama zinarandana na ubora wa nyumba, Kasanda alisema wahusika walimueleza kuwa gharama zilizoandikwa katika taarifa zilikuwa zimekosewa na kwamba nyumba imegharimu sh. milioni 38 na si 89 iliyosoma kwake.

"Wasaidizi wangu ulioongea nao awali waliniambia juu ya hilo na nikafuatilia na mkurugenzi ameniambia walikosea katika kuandika na kwamba gharama zake ni sh. milioni 38," alisema Kasanda akiwa katika kata ya Simbo.

Nyumba hiyo ina vyumba viwili vya kulala visivyokuwa na vyoo vya ndani, sebule moja pamoja na madirisha manne yaliyowekwa nondo na nyavu, huku sakafu yake ikiwa ya kawaida ya saruji na kuezekwa kwa bati.

Kwa mujibu wa taarifa fupi ya ujenzi iliyosomwa kwa kiongozi wa mbio za mwenge, mbali na sh milioni 89 gharama za nyumba hiyo, pia zimetumika sh .milioni 58.5 kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha maabara, sh. milioni 38.8 kwa ajili ya vyumba viwili vya madarasa na sh. milioni 23.9 kwa ununuzi wa samani.

Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya ukandarasi ya Elisha & Son Ltd ya mjini Igunga, iliyopewa kazi ya ujenzi wa majengo hayo, alipoulizwa gharama za nyumba ya mwalimu alisema hazizidi sh. milioni 50 na si chini ya milioni 40.

"Kama wanasema ni sh. milioni 89 sasa unanifumbua macho labda kuna mkataba unaotuhusu sisi na ule unaohusu taarifa zao mbele ya umma lakini hizo gharama za nyumba hazifiki huko," alisema.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Igunga, Rustruka Turuka alipoulizwa gharama halisi ya jengo hilo, alielekeza swali hilo kwa Afisa Elimu Sekondari, Aloyce Kaziyareli ambaye alisema gharama zilizosomwa siku ya uzinduzi ndizo zinapaswa kufuatwa.

"Gharama ni hizo hata hiyo nyumba ndiyo gharama yake, sasa ukitaka kujua zimefikaje hayo ni maswali ya Mkandarasi," alisema Kaziyareli.

Jana, mkuu wa wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu, alizungumza na gazeti hili na kukiri kuwaita badhi ya maofisa wa halmashauri katika ofisi yake kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa ubora wa mradi huo na fedha zilizotumika.

Alisema baada ya kuongea nao aliwaagiza kusitisha malipo kwa mkandarasi na kisha mthamini wa ujenzi wa halmashauri awasilishe taarifa yake ya kukubali jengo hilo la walimu kuwa na thamani ya sh. milioni 89.

Kwa mujibu wa Kingu, baada ya hatua hiyo wataalam mbali mbali wataenda kufanya tathmini upya kuthibitisha kama nyumba iliyojengwa ina thamani ya fedha iliyotajwa.

Huyu aliyepitisha BOQ ya fedha hizo tunamtaka ajieleze kwa kuwa jengo halilingani na thamani ya fedha iliyotajwa," alisema Kingu.


Chanzo: Tanzania Daima
 
Kwani kabla ya siku hiyo hakuwa anajua nini kinaendelea hapo????
Hivi kama mbio za mwenge zinahusisha kuzindua miradi je huwa kuna wataalamu wa fani husika au ndio hao wanatafuta nyufa tu??!!
 
Wakuu,
Miradi ya Ujenzi katika Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, imeghubikwa na tuhuma za ufisadi, ambapo hivi karibuni imekabidhiwa nyumba ya Mwalimu yenye Vyumba viwili vya kulala na sebule, ikitajwa kugharimu sh. milioni 89, jambo ambalo limeibua utata na kumlazimu Mkuu wa Wilaya hiyo, Elibariki Kingu kuingilia kati.

Gharama ya ujenzi wa nyumba hiyo katika Shule ya Sekondari Ichana Kata ya Chabutwa ni sehemu ya Matumizi ya Milioni 219 zilizotolewa na Serikali kuu kupitia mpango wa maendeleo ya Elimu ya Sekondari[MMES] kwa ufadhili wa bank ya Dunia.

Wakuu naomba tujadili haya matumizi. Nimejaribu kuweka picha kutoka Gazeti la Tanzania daima la Leo.

attachment.php


Mia
 

Attachments

  • nyumba.jpg
    nyumba.jpg
    27.5 KB · Views: 4,793
labda ndani wameweka vito vya thamani ya pesa kubwa!, si wana mpango wa kuweka mazingira mazuri ili walimu wasikimbie kwenye vituo vya kazi zao?
 
Ndani ya serikali ya CCM yote hayo yanawezekana...

Hapana Mkuu, yote hayawezekani kumbuka maisha Bora kwa kila Mtanzania yameshindikana, yapo mengi tu yameshindikana hasa ya jamii mfano kupiga marufuku Uvaaji wa hovyo hovyo (mlegezo) watu kuvaa suruali chini ya makalio wadada kuvaa vinguo vya ajabu, kwenye Maadili wamefeli, isipokuwa kwenye Uchakachuaji hawana Mpinzani Duniani.
 
Namwamini sana Elibariki Kingu, Mkuu wa wilaya ya Igunga, nadhani atasimamia hilo vyema.
 
Kwa magamba kila kitu kinawezekana. Hata mil. 15 haifiki. Hizo hela zingeweza kujenga zingine 6
 
labda ndani wameweka vito vya thamani ya pesa kubwa!, si wana mpango wa kuweka mazingira mazuri ili walimu wasikimbie kwenye vituo vya kazi zao?

Ndani kuna AC 12, Thamani za ndani zote zimenakishiwa kwa madini ya Alumas na Dhahabu,chezea wajanja weweee.....
 
Ama kweli tunahangaika kumtafuta alieye turaga kumbe huyo mganga na mchawi ndo tunawafuga sisi wenyewe
 
Hiyo nyumba hata Tsh. 25,000,000 haizidi. Wizi mtupu! EPA kila mahali.

Hapo ndipo ninapowapendea watu wa serikalini, na huyo mkuu wa wilaya Mr Kingu hawezi fanya kitu kwani naye wenzie wanajua anavyopiga deal zake,

Uzuri wa nyumba ya panya wapangaji wote ni mapacha wanafanana kama Kulwa na Dotto
 
Hiyo pesa inaweza kujenga nyumba10 kama hizo kwa pale igunga. No wonder ndo zao magamba.
 
Kwa magamba kila kitu kinawezekana. Hata mil. 15 haifiki. Hizo hela zingeweza kujenga zingine 6

Mkuu si kila kitu kinawezekana ! Vingi vimewashinda mfano Maisha Bora kwa kila Mtanzania na maadili kwenye Uvaaji nguo hivi sasa kila kijana anavaa suruali chini ya Makalio ( Mlegezo) si Rais wala Waziri Mkuu, au Waziri au hata Mkuu wa mkoa au wilaya hata kijiji anathubutu kukemea Uvaaji wa hovyo hovyo.
 
Kwa uzoefu wangu na kwa mtazamo wa haraka, kama watakuwa amenunua kiwanja basi, nyumba hiyo inaweza kuwa imegharimu 39 milion. ila kama kiwanja hakija nunuliwa nyumba hiyo itakuwa imegharimu 35milion za uhakika. hivyo milioni 50 zitakuwa zimewekwa kibindoni!!
 
Back
Top Bottom