nyumba ya kupanga tegeta nyaishozi

candygrapez

Member
Jul 21, 2009
12
2
Habari wana jamii forum, nina nyumba yangu mitaa ya tegeta nyaishozi haiko barabarani,unaingia ndani kama mwendo wa dakika 10 kwa mguu toka barabara kuu,ninayohitaji kuipangisha ,ila tatizo niko mkoani Shinyanga ambako ndiko ninaishi kwa sasa,na sina uzoefu na upangaji/upangishwaji wa nyumba kwa mji wa Dar, ninachoomba kuuliza ni nyumba kama hii ina master bedroom kubwa tu ya kutosha,vyumba viwili vya kulala na choo,jiko,na stoo ndogo,uwanja wa wastani pamoja na fensi na geti,furniture ananunua mpangaji kwa mitaa hiyo naweza nikaambulia kama pango la shilingi ngapi kwa mwezi/mwaka?
na madalali wa uhakika naweza nikawapata wapi?
Ahsante.
 
Naishi maeneo ya Nyamachabes, kupata wapangaji huku ni kazi sana na hata ukipata mpangaji atakuambia akupe laki 3 kwa mwezi, sababu ni mbali sana na mjini napia kuna msongo mkubwa wa foleni
 
Naishi maeneo ya Nyamachabes, kupata wapangaji huku ni kazi sana na hata ukipata mpangaji atakuambia akupe laki 3 kwa mwezi, sababu ni mbali sana na mjini napia kuna msongo mkubwa wa foleni
ahsante ndugu kwa insight,na madalali wa kuaminika kwa maeneo hayo nitawapata wapi?
 
Back
Top Bottom