Nyumba ya kiongozi wa CCM Igunga yachomwa Moto; CUF waungana na CCM,Chadema waruka

Waungwana tujadili...jana Mzindakaya kasaini Mkataba Wa Mchuchuma kuhusu kuzalisha MW 600 za umeme..jambo la kusikitisha nikwamba alishauriwa na mwanasheria mkuu wa serikali asubirii kable hajasaini waweke comments zao..lakini kwa simu mzee wa watu kaanguka...kisa keshapewa dilii kuwa watachukua kimeo chake cha SAAFI
 
Hivi kumbe kuku anaweza kuungua kirahisi sana kuliko karatasi. Ama hiyo karatasi ilikuja chomekwa wakati moto ushazimika. Na kama alikuwa na wasiwasi anawindwa na CDM, kwanini aliposhindwa uzima moto alirudi kwenye nyumba ya kulala hadi kesho yake, hakuwa na wasiwasi maana alijua alichokifanya tayari. Kweli sasa najitoa rasmi CCM, maana tutaonekana wote wapuuzi.....
 
Mhuuuu yahani hii ndo nyumba? miaka 40 ya CCM madarakani? Kweli maisha bora ndo hayo angalieni mtaendelea kula majani kama ng'ombe ili rais asafiri



Wednesday, 21 September 2011 21:03





07ccmigu.jpg
Katibu mkuu wa CCM, Wilson Mukama (mwenye miwani) akitoka kuangalia nyumba ya Katibu wa chama hicho kata ya Nyandekwa Jimbo la Igunga, Hamis Makala iliyochomwa moto usiku wa kuamkia juzi na watu wasiojulikana. Picha na Daniel Mjema


Daniel Mjema, Igunga

MATUKIO ya hujuma yanazidi kulitikisa Jimbo la Igunga safari hii watu wasiojulikana wamechoma moto nyumba ya Katibu wa CCM, Kata ya Nyandekwa usiku wa kuamkia juzi.Tukio hilo linahusishwa na wafuasi wa Chadema kutokana na ujumbe wa maandishi uliokutwa umechomekwa katika nyumba hiyo ukisomeka: “Chadema sisi ni wajanja”.Katibu huyo, Hamis Makala alimweleza Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama aliyemtembelea jana kumpa pole kuwa, kwa muda mrefu amekuwa akiwindwa na wafuasi hao wa Chadema.

Alidai kuwa sababu ya kuwindwa na wafuasi hao inatokana na kukasirishwa na kampeni anazozifanya katika kata hiyo zinazoifanya CCM ikubalike kwa wananchi na kukiacha Chadema kikikosa watu kinapokwenda kufanya mikutano ya hadhara. Nyumba iliyoteketezwa kwa moto ilikuwa ikitumiwa na katibu huyo kwa shughuli za jiko na kuhifadhia kuku.

“Niliposhtuka na kutoka nje nilikuta moto mkubwa unawaka nikapiga yowe kuomba msaada. Lakini majirani walishindwa kuuzima kwa kuwa ulikuwa umesambaa… kuku 15 kati ya 21 waliokuwamo ndani wamekufa,” alisema.

Alisema baada ya kushindwa kuuzima moto huo na nyumba hiyo kuteketea, aliamua kulala na asubuhi majirani walipofika tena kumjulia hali ndipo walipogundua karatasi ikiwa na ujumbe wa Chadema kuhusika.

Alidai kuwa mbali na ujumbe huo, upo mwingine wa maandishi ambao ulipenyezwa katika Ofisi ya CCM ya kata hiyo unaosisitiza kuwa Chadema hawahitaji bendera za CCM katika kata hiyo. Alisema kuwa karatasi zote hizo mbili zimechukuliwa na polisi.

Mukama alaani
Akizungumzia tukio hilo, Mukama amesema alisema ni lazima lilaaniwe na kila Mtanzania mpenda amani wakiwamo wananchi wa Igunga na akavitaka vyombo vya dola kuhakikisha vinawasaka na kuwakamata waliohusika.

“Ni lazima lilaaniwe kwa sababu halitoi taswira na maana halisi ya kuwa na vyama vingi ambavyo vinapaswa kushindana kwa ubora na sera… hatushindani kwa vitisho, uhuni na hata kumwagiana tindikali,” alisema.

Alisema ameshangazwa na mwenendo wa Chadema kuendesha siasa za chuki hususan katika Jimbo la Igunga na kutoa mfano wa Kenya ambako vyama vingi ni vya kikabila lakini hakuna matukio ya aina hiyo.

Alitumia fursa hiyo kupiga kampeni akisema matukio yanayotokea Igunga hivi sasa yanawasaidia Watanzania kukielewa Chadema ni chama cha aina gani na kuwataka Wana-Igunga kukiadhibu hicho kwa kukinyima kura Oktoba 2 ,mwaka huu.

“Demokrasia haiwezi kuanishwa kwa matukio ya kihuni na wale wanaotaka kuipa demokrasia taswira ya hovyo ni lazima waadhibiwe. Njia pekee ya kuwaadhibu watu wa aina hiyo ni kuwanyima kura,” alisema.

Katibu Mkuu huyo alimpa kiongozi huyo msaada wa Sh100,000 ili azitumie kuirejesha nyumba hiyo katika hali iliyokuwapo kabla ya tukio.

CUF waungana na CCM

Mwenyekiti wa CUF Kata ya Nyandekwa, Emmanuel Ezekiel ambaye alifika eneo la tukio mata tu baada ya Mkama na msafara wake kufika, alisema tukio hilo ni la kihuni na linapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote.

“Unajua kwenye mji unaweza kuwa na watoto watatu wa baba mmoja, mama mmoja lakini akatokea mmoja akawa kichaa msipomdhibiti atawaharibia ule mji,” alisema Ezekiel bila kufafanua kauli yake hiyo.

Mwenyekiti huyo alitahadharisha kuwa kampeni katika Jimbo hilo la Igunga ni za mwezi mmoja tu lakini, kama zisipofanyika kwa ustaarabu zinaweza kuzaa uhasama utakaodumu kwa miaka mingi.

Polisi wanena

Mkuu wa kitengo cha ufuatiliaji na tathmini kutoka makao makuu ya Polisi, Naibu Kamishna, Isaya Mngullu alisema polisi wanaendelea na upelelezi.

“Ni kweli hilo tukio lipo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia jana (juzi) na sisi tumeanzisha upelelezi, nipeni muda tukusanye taarifa halafu nitawaita (waandishi) niwapeni taarifa kamili,” alisema Mngullu.

Chadema waruka
Lakini Kamanda wa Operesheni za Kampeni wa Chadema, Benson Kijaila jana alikanusha chama chake kuhusika na tukio hilo na kukigeuzia kibao CCM kuwa wao ndicho kilichoshiriki katika tukio hilo.

“Matukio haya wanayapanga wao wenyewe halafu wanasingizia vijana wetu… kama ni kuchoma hiyo nyumba wameichoma wenyewe ni mpango wao huo,” alisema.

Kamanda huyo alisema hata tuhuma za tindikali zinazoelekezwa kwa Chadema ni mipango iliyosukwa na CCM na kwamba kama ni watu wenye tindikali, basi CCM ndiyo walionazo.

Tukio hilo la juzi la kuchomwa moto nyumba ya kada huyo wa CCM ni mwendelezo wa matukio ya kihalifu yanayotokea Igunga na wakati wote, matukio hayo yamehusishwa na wafuasi wa Chadema.

Mwanzoni mwa wiki hii, wabunge wawili na kada mmoja wa chama hicho walishtakiwa mahakamani kwa makosa manne likiwamo la kumdhalilisha na kumwibia Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario.

Septemba 9 mwaka huu, kijana mmoja anayedaiwa ni mwanachama wa CCM, Mussa Tesha (25) alimwagiwa tindikali usoni na watu anaodai kuwatambua kuwa ni wanachama wa Chadema.

 
hiyo ni janja ya ccm!!!! mtu anayechoma nyumba au anayefanya uhalifu anahaja ya kuacha ujumbe!!! jamani fungukeni hiyo ni janja ya ccm!
 
ccm wamefilisika kisiasa mpaka mbinu za kihujuma, yaani hata mtoto wa shule ya vidudu hawezi kukubali kuwa nyumba iungue moto halafu ujumbe(kama ulikuwa umeandikwa kwenye karatasi) ubaki salama labda kama ujumbe huo uliandikwa kwenye jiwe kama zile amri kumi alizopewa nabii Musa!
 
Tusipoteze muda katika hili, aliyechoma nyumba ile ni Mukama , ushahidi upo wazi kamlipa mweye banda lake tena hadharani, aibu kwenu CCM na mbinu zenu za kijuha , katika hili hamumpati mtu labda wajinga wajinga huko magamba
 
hiyo ni janja ya ccm!!!! mtu anayechoma nyumba au anayefanya uhalifu anahaja ya kuacha ujumbe!!! jamani fungukeni hiyo ni janja ya ccm!

na sio hilo tu kuna kitu kingine nimegundua hapa bongo kwa nini huwa kipindi cha chaguzi ndogo huwa kuna matatizo toka mwaka jana kule musoma hapa kazi ipo..
 
Yaani unachomewa banda kisha unarudi ndai kulala usiku huo huo, hao 'wachoji' watakuwa na akili za kiccm
 
hahaa hawa CCM wanaleta mambo ya kijinga na siasa wanazofanya ni za kitoto sana, ninajiuliza
1. Mukama katoa laki moja ya nini?
2.mwenye nyumba ilikuwaje aamuke apige yowe halafu arudi kulala mpaka asubuhi?
3. Karatsi ambayo ilikuwa na ujumbe unaosema CHADEMA NI WAJANJA kwanini haikuungua?
4. Kuku 15 wameeungua wakabaki 5. iweje hao wengine wasiuungue wakati inaonyesha nyumba imeteketea kabisa?
Angalizo na ushauri kwa mwenyekiti wa CCM asione haya kulikosa hili jimbo maana mbegu ya chuki inayopandikizwa na chama chake ina sumu mbaya kuliko hata ya chatu...
 
Waungwana tujadili...jana Mzindakaya kasaini Mkataba Wa Mchuchuma kuhusu kuzalisha MW 600 za umeme..jambo la kusikitisha nikwamba alishauriwa na mwanasheria mkuu wa serikali asubirii kable hajasaini waweke comments zao..lakini kwa simu mzee wa watu kaanguka...kisa keshapewa dilii kuwa watachukua kimeo chake cha SAAFI

....Mimi naona huyo mwanasheria mkuu ndio kilaza kabisa....sioni kama angekuwa na lolote la kuongeza zaidi ya kuweka na yeye cha juu........huu mkataba wa makaa ya mawe Liganga na chuma ...ni kati ya mikataba fair kwa nchi ..offcourse NDC watakuwa na share ..like 30% unlike barrick na kwingine ambako hatuja retain share ......hata 0.1% sasa mwanasheria mkuu ..angoje kupiga muhuri..washina nawaamini kwenye win - win.... unlike wazungu ...hawana maneno mengi ..pale miaka mitatu ijayo mradi utatoa megawatt 600 ..kufikia 2018 watafikisha megawatt 1,800 ...na zaidi itachochea uwekezaji kwenye heavy Iron industries kwenye ukanda wa mtwara na Lindi..kama gateway ya bahari.....na itapunguza vurugu za vyuma chakavu kwa ajili ya hii issue ya chuma kitakachozalishwa pale.......

So what to discuss here ..?? lets be fair ;pale ambako serikali inajitahidi ....hapa kwenye hili i can bank kuwa sio longo longo ..i saw minister Chami and Mzindakaya signing ...ni kati ya miradi mikubwa 3 billion usd!
 
Katika msafara wa Mamba, kenge nao wamo..
Leo nasimama upande wa pili ktk swala hili. Viongozi na wana Chadema mnatakiwa kulaani vitendo kama hivi badala ya kuendelea kutetea dhamira chafu kama hizi. Na inasikitisha sana kuwasoma watu wakiendelea kuchochea vitendo kama hivi dhidi ya viongozi wa CCM kama ndio mwanzo wa mapinduzi na nguvu ya Umma lakini kwa unafiki wanajitenga kuhusika..Nani kweli atakuwa mkisiwa ktk janga kama hili?

Na ifike mahala wanaChadema mkubali kuonyesha sura zenu kwa sababu haiwezi kuingia akilini hata kidogo nyumba ya katibu wa CCM kuchomwa moto bila wanaChadema kuwa main suspects, hili lazima tulikubali na tuonyeshe ushahidi tosha wa kutohusika lakini sii kukataa wakati huo huo tukishangilia...Wahusika wakamatwe na kufikishwa mahakamani ili ukweli upatikane na waadhabishwe.

Tulipofikia ni mahala pabaya sana kwa usalama wa wananchi na viongozi wetu kwani zipo sehemu viongozi wa CCM wakipita kutupiwa mawe na wengine kuchaniwa nguo na kadhalika hali ambayo haiwezi kutafsirika zaidi ya kuwa ni uhalifu na hauwezi kutetewa na mtu yeyote mwanye akili timamu.
Binafsi sikubaliani na madai ya waislaam kuhusiana na dc kuvuliwa Hijab kuwa swala la kidini, lakini wakati huo huo sikubaliani na kitendo cha watu kumvamia DC bila kufuata taratibu za usalama iwe kwa huyo DC ama wahusika kwa sababu sheria zipo na vyombo vya usalama vipo kutekeleza wajibu ambao wamekabidhiwa ktk kulinda wananchi.

Matukio haya mawili yanaonyesha wazi kwamba sasa hivi wananchi wamepoteza nidhamu na kama hii ndio nguvu ya Umma basi Chadema na wanaChadema inawabidi mkubali kutumia nguvu hizi badala ya kukataa kuhusika wakati huo huo mkiunga na kushangilia habari hizi..Si rahisi yafanywayo na Kenge hawa kutofautishwa ktk msafara wa Mamba! -Ni jamii moja!
 
07ccmigu.jpg


Hii nyumba iko polini? au kwenye mahame maana sioni nyumba zingine kwa karibu.

Yaani Mukama anafanya mpango kuchoma nyumba ya mtu kwa laki!!, aliyefanya mpango, aliyechoma na aliyekubali nyumba yake kuchomwa kwa laki wote ni wapumbavu sana.
 
Ccm wote wanaakili mgando kweli

Hili jina lako limenichesha sana

Kwahali ilivyo Igunga kunaitajika jicho la tofauti, kuna mitegomitego mingi

CCM wanapenda kurudisha heshima, na CDM wanataka ku prove a point

Haya yangu macho
 
CCM naona mumeishiwa mbinu za kuwahadaa raia mpaka mmeamua kuitumia hii ya kitoto zaidi
Am sure kwa mwendo huu mtakuwa mnajipanga kuiba kura na kuyasindikiza mabox ya kura na JWTZ
 

....Mimi naona huyo mwanasheria mkuu ndio kilaza kabisa....sioni kama angekuwa na lolote la kuongeza zaidi ya kuweka na yeye cha juu........huu mkataba wa makaa ya mawe Liganga na chuma ...ni kati ya mikataba fair kwa nchi ..offcourse NDC watakuwa na share ..like 30% unlike barrick na kwingine ambako hatuja retain share ......hata 0.1% sasa mwanasheria mkuu ..angoje kupiga muhuri..washina nawaamini kwenye win - win.... unlike wazungu ...hawana maneno mengi ..pale miaka mitatu ijayo mradi utatoa megawatt 600 ..kufikia 2018 watafikisha megawatt 1,800 ...na zaidi itachochea uwekezaji kwenye heavy Iron industries kwenye ukanda wa mtwara na Lindi..kama gateway ya bahari.....na itapunguza vurugu za vyuma chakavu kwa ajili ya hii issue ya chuma kitakachozalishwa pale.......

So what to discuss here ..?? lets be fair ;pale ambako serikali inajitahidi ....hapa kwenye hili i can bank kuwa sio longo longo ..i saw minister Chami and Mzindakaya signing ...ni kati ya miradi mikubwa 3 billion usd!
Mkuu wangu kosa lazima lipo. katika mikataba kuna finelines ambazo ni mwanasheria tu anaweza kuzitafsiri na kama mwanasheria mkuu amesema SUBIRINI, basi ilibidi wasubiri!
 
ccm wamefilisika kisiasa mpaka mbinu za kihujuma, yaani hata mtoto wa shule ya vidudu hawezi kukubali kuwa nyumba iungue moto halafu ujumbe(kama ulikuwa umeandikwa kwenye karatasi) ubaki salama labda kama ujumbe huo uliandikwa kwenye jiwe kama zile amri kumi alizopewa nabii Musa!

Source ya hiyo picha na habari hiyo ni gazeti la Mwananchi la leo,ninalo hapa mkononi.Hiyo picha inavyoonekana kwenye gazeti na ilivyotolewa JF kuna tofauti kidogo,kwenye gazeti inaonekana kwa uzuri zaidi.Nimeiangalia kwa jicho la tatu nimegundua yafuatayo:

1.Hicho KIBANDA CHA KUKU (mwenye nacho ndo kakitambulisha hivyo,ingawa wenye malengo yao wanaiita NYUMBA) kinaonekana kiko mbali na nyumba nyingine,inaonekana ni nje ya kijiji hivi.Kwamba kimetafutwa kwa lengo hilo ili kikiteketezwa kisilete madhara.

2.Picha inayoonyesha tukio hilo iko moja tu kwenye gazeti la Mwananchi.Nimetafuta labda naweza ona picha zaidi za tukio hili kwenye magazeti mengine kama Mtanzania,Rai,Uhuru,Daily news,Habari leo,Majira na Jambo leo (nadhani mmenielewa kwa nini nimeyataja haya) sijaona chochote.

My take:

Hili tukio limetengenezwa kwa nia ile ile ya kuughiribu umma.Waliotangulia wameongelea Kikaratasi kutoungua,wahusika kujitaja kuwa ni wa chama fulani,mwenye kibanda kuwahisi wabaya wake na bado akarudi kulala kwenye nyumba yake wakati kibanda chake cha kuku kinateketea-inafikirisha sana.

Wahusika wametumia mbinu ya kitoto sana isiyokuwa na mashiko,kimsingi wanaendelea kujiaibisha.Nafikiri hali ni mbaya sana kwao na hizo ndo dalili za kushindwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom