Nyumba ya kiongozi wa CCM Igunga yachomwa Moto; CUF waungana na CCM,Chadema waruka


nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
81
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 81 145
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"][/TD]
[TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Wednesday, 21 September 2011 21:03[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
07ccmigu.jpg
Katibu mkuu wa CCM, Wilson Mukama (mwenye miwani) akitoka kuangalia nyumba ya Katibu wa chama hicho kata ya Nyandekwa Jimbo la Igunga, Hamis Makala iliyochomwa moto usiku wa kuamkia juzi na watu wasiojulikana. Picha na Daniel Mjema

Daniel Mjema, Igunga

MATUKIO ya hujuma yanazidi kulitikisa Jimbo la Igunga safari hii watu wasiojulikana wamechoma moto nyumba ya Katibu wa CCM, Kata ya Nyandekwa usiku wa kuamkia juzi.Tukio hilo linahusishwa na wafuasi wa Chadema kutokana na ujumbe wa maandishi uliokutwa umechomekwa katika nyumba hiyo ukisomeka: “Chadema sisi ni wajanja”.Katibu huyo, Hamis Makala alimweleza Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama aliyemtembelea jana kumpa pole kuwa, kwa muda mrefu amekuwa akiwindwa na wafuasi hao wa Chadema.

Alidai kuwa sababu ya kuwindwa na wafuasi hao inatokana na kukasirishwa na kampeni anazozifanya katika kata hiyo zinazoifanya CCM ikubalike kwa wananchi na kukiacha Chadema kikikosa watu kinapokwenda kufanya mikutano ya hadhara. Nyumba iliyoteketezwa kwa moto ilikuwa ikitumiwa na katibu huyo kwa shughuli za jiko na kuhifadhia kuku.

“Niliposhtuka na kutoka nje nilikuta moto mkubwa unawaka nikapiga yowe kuomba msaada. Lakini majirani walishindwa kuuzima kwa kuwa ulikuwa umesambaa… kuku 15 kati ya 21 waliokuwamo ndani wamekufa,” alisema.

Alisema baada ya kushindwa kuuzima moto huo na nyumba hiyo kuteketea, aliamua kulala na asubuhi majirani walipofika tena kumjulia hali ndipo walipogundua karatasi ikiwa na ujumbe wa Chadema kuhusika.

Alidai kuwa mbali na ujumbe huo, upo mwingine wa maandishi ambao ulipenyezwa katika Ofisi ya CCM ya kata hiyo unaosisitiza kuwa Chadema hawahitaji bendera za CCM katika kata hiyo. Alisema kuwa karatasi zote hizo mbili zimechukuliwa na polisi.

Mukama alaani
Akizungumzia tukio hilo, Mukama amesema alisema ni lazima lilaaniwe na kila Mtanzania mpenda amani wakiwamo wananchi wa Igunga na akavitaka vyombo vya dola kuhakikisha vinawasaka na kuwakamata waliohusika.

“Ni lazima lilaaniwe kwa sababu halitoi taswira na maana halisi ya kuwa na vyama vingi ambavyo vinapaswa kushindana kwa ubora na sera… hatushindani kwa vitisho, uhuni na hata kumwagiana tindikali,” alisema.

Alisema ameshangazwa na mwenendo wa Chadema kuendesha siasa za chuki hususan katika Jimbo la Igunga na kutoa mfano wa Kenya ambako vyama vingi ni vya kikabila lakini hakuna matukio ya aina hiyo.

Alitumia fursa hiyo kupiga kampeni akisema matukio yanayotokea Igunga hivi sasa yanawasaidia Watanzania kukielewa Chadema ni chama cha aina gani na kuwataka Wana-Igunga kukiadhibu hicho kwa kukinyima kura Oktoba 2 ,mwaka huu.

“Demokrasia haiwezi kuanishwa kwa matukio ya kihuni na wale wanaotaka kuipa demokrasia taswira ya hovyo ni lazima waadhibiwe. Njia pekee ya kuwaadhibu watu wa aina hiyo ni kuwanyima kura,” alisema.

Katibu Mkuu huyo alimpa kiongozi huyo msaada wa Sh100,000 ili azitumie kuirejesha nyumba hiyo katika hali iliyokuwapo kabla ya tukio.

CUF waungana na CCM

Mwenyekiti wa CUF Kata ya Nyandekwa, Emmanuel Ezekiel ambaye alifika eneo la tukio mata tu baada ya Mkama na msafara wake kufika, alisema tukio hilo ni la kihuni na linapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote.

“Unajua kwenye mji unaweza kuwa na watoto watatu wa baba mmoja, mama mmoja lakini akatokea mmoja akawa kichaa msipomdhibiti atawaharibia ule mji,” alisema Ezekiel bila kufafanua kauli yake hiyo.

Mwenyekiti huyo alitahadharisha kuwa kampeni katika Jimbo hilo la Igunga ni za mwezi mmoja tu lakini, kama zisipofanyika kwa ustaarabu zinaweza kuzaa uhasama utakaodumu kwa miaka mingi.

Polisi wanena

Mkuu wa kitengo cha ufuatiliaji na tathmini kutoka makao makuu ya Polisi, Naibu Kamishna, Isaya Mngullu alisema polisi wanaendelea na upelelezi.

“Ni kweli hilo tukio lipo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia jana (juzi) na sisi tumeanzisha upelelezi, nipeni muda tukusanye taarifa halafu nitawaita (waandishi) niwapeni taarifa kamili,” alisema Mngullu.

Chadema waruka
Lakini Kamanda wa Operesheni za Kampeni wa Chadema, Benson Kijaila jana alikanusha chama chake kuhusika na tukio hilo na kukigeuzia kibao CCM kuwa wao ndicho kilichoshiriki katika tukio hilo.

“Matukio haya wanayapanga wao wenyewe halafu wanasingizia vijana wetu… kama ni kuchoma hiyo nyumba wameichoma wenyewe ni mpango wao huo,” alisema.

Kamanda huyo alisema hata tuhuma za tindikali zinazoelekezwa kwa Chadema ni mipango iliyosukwa na CCM na kwamba kama ni watu wenye tindikali, basi CCM ndiyo walionazo.

Tukio hilo la juzi la kuchomwa moto nyumba ya kada huyo wa CCM ni mwendelezo wa matukio ya kihalifu yanayotokea Igunga na wakati wote, matukio hayo yamehusishwa na wafuasi wa Chadema.

Mwanzoni mwa wiki hii, wabunge wawili na kada mmoja wa chama hicho walishtakiwa mahakamani kwa makosa manne likiwamo la kumdhalilisha na kumwibia Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario.

Septemba 9 mwaka huu, kijana mmoja anayedaiwa ni mwanachama wa CCM, Mussa Tesha (25) alimwagiwa tindikali usoni na watu anaodai kuwatambua kuwa ni wanachama wa Chadema.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Blandes

Blandes

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2011
Messages
245
Likes
18
Points
35
Age
28
Blandes

Blandes

JF-Expert Member
Joined Sep 17, 2011
245 18 35
Mbinu chafu za ccm,mmesahau walivyoeneza suala la udin kwenye uchaguz mkuu?na ukabila?
 
tz1

tz1

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2011
Messages
2,128
Likes
42
Points
145
tz1

tz1

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2011
2,128 42 145
Hapa pana ulakini,they are cooking up things
 
Amoeba

Amoeba

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2009
Messages
3,328
Likes
122
Points
0
Amoeba

Amoeba

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2009
3,328 122 0
Things are falling apart!
 
C

Chupaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2008
Messages
1,078
Likes
189
Points
160
C

Chupaku

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2008
1,078 189 160
Inafurahisha sana. Kwanini Chadema hawakuchoma nyumba ya kulala wakachome kuku? Hahaaaa
 
Lukolo

Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
5,147
Likes
103
Points
160
Lukolo

Lukolo

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
5,147 103 160
Hao chadema ni wapumbavu kiasi gani wakachome kibanda cha kuku na wasichome nyumba anayoishi huyo kada wa CCM? Hawa magamba akili zao haziko timamu, mbona wanafanya michezo ambayo hata watoto wadogo hawawezi kuicheza?
 
Washawasha

Washawasha

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
9,909
Likes
1,473
Points
280
Washawasha

Washawasha

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
9,909 1,473 280
bora sie hajafa mtu. USA wao wanagonga majengo yao(WTC) wenyewe na wanatengeneza vimbunga(Tsunami) ili kuwaua raia wao wenyewe halafu kesi wanapewa Alqaeda
 
jouneGwalu

jouneGwalu

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
2,687
Likes
81
Points
145
jouneGwalu

jouneGwalu

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
2,687 81 145
Kwenye "game" ya Igunga.....
Mchezaji anayenifurahisha zaidi ni hyu anayekwenda kwa jina la "CUF"...!
CCM ni wanatia huruma tu wanavyotapatapa na siasa nyepesi
 
Kamakabuzi

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2007
Messages
1,535
Likes
96
Points
145
Kamakabuzi

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2007
1,535 96 145
Inatia mashaka mtu akachome nyumba kwa siri halafu aache ujumbe wa kujitambulisha! Kama alitaka ajulikane si angekuja mchana?
Kisa hiki kinanikumbusha tukio la wizi kwenye duka moja ambapo mwenye duka alidai kuokota picha iliyodondoshwa na wezi kwenye duka. Nilipofuatilia kwa makini nikagundua kuwa polisi walipofika kwa mtuhumiwa, kwa kuwa walikuwa hawamjui waliamua kuomba albam kwa mkewe na wakachomoa picha moja ambayo iklikuwa ikimuonyesha vizuri. Baada ya kukosa ushahidi, wakaamua kumpa picha hiyo mwenye duka aseme kuwa waliidondosha dukani wakati wa kuiba. Hakika hakimu mwenye busara alikataa kukubaliana na ushahidi huo kwani hakuona sababu ya mwizi kwenda kuiba akiwa na picha kama hiyo tena picha yenyewe ilionekana kupigwa wakati wa arusi yake.
Mimi nilimfuata mwenye duka na kumweleza kuwa kama kweli yeye ni muumini mzuri basi ukweli utakuja kukusuta hapa hapa duniani. Baada ya hakim kutilia mashaka ushahidi huo, jamaa hakuedelea na kesi!
 
tembeleh2

tembeleh2

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2010
Messages
767
Likes
4
Points
35
tembeleh2

tembeleh2

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2010
767 4 35
Historia ya maendeleo inaonyesha kwamba mabadiliko chanya lazima yatokee baada ya migongano/mitafaruku (contradictions) mikali baina ya pande mbili hasimu, kwa hiyo basi kwa sababu Tanzania tunaelekea kwenye mabadiliko chanya tutegemee kuona mengi sana kuliko haya.
 
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2010
Messages
12,556
Likes
2,368
Points
280
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined Feb 9, 2010
12,556 2,368 280
Sijawahi ona mkakati wa kitoto km huu ulofanywa na ccm!
 
T

Topical

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2010
Messages
5,175
Likes
11
Points
0
T

Topical

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2010
5,175 11 0
Hao chadema ni wapumbavu kiasi gani wakachome kibanda cha kuku na wasichome nyumba anayoishi huyo kada wa CCM? Hawa magamba akili zao haziko timamu, mbona wanafanya michezo ambayo hata watoto wadogo hawawezi kuicheza?
Hivi unafikir chadema wana akili? aise hawana kabisa
 
A

August

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2007
Messages
4,640
Likes
802
Points
280
A

August

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2007
4,640 802 280
hii ni aibu kwa huyu dr kafumu kushiri na kuwa kwenye chama chenye vitendo vya kitoto? sasa kwa sera kama hizi weli wana nia ya kuleta maendeleo hawa? naona magamba baada a kuwaleta heavy weight wao na dalili zina onyesha kushindwa ndio wameleta mkakati wa kuonewa huruma, maana kwenye kampeni watu wana enda kuangalia commedy na kuondoka
 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
81
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 81 145
Yaani CCM ina Vyombo Vyote Vya Kiulinzi na bado wanahujumiwa??

Nyumba ni ya Udongo, unajua ni vigumu kweli kuchoma nyumba ya Udongo; inabidi kutumia karibia lita 100 za mafuta na ni kijijini unahitaji watu zaidi ya kumi kubeba na kufanya kuunguza huo moto, sasa wenye nyumba na wenyeji walikuwa wapi mpaka jengo hilo likateketea kabisa?

Mmeona Picha? yaani imeungua mpaka imeisha ...

CCM wanajua hayo Madhara yanafanywa na nani...
 
M

MWananyati

Senior Member
Joined
Feb 3, 2011
Messages
158
Likes
13
Points
35
Age
43
M

MWananyati

Senior Member
Joined Feb 3, 2011
158 13 35
Mbona wakati wa kampeni za chaguzi ndogo, CCM huwa mnalia kua mnaonewa? karatasi kuwepo popote si kithibitisho cha mtu kukutwa na kosa. Hebu acheni kutafuta KURA ZA HURUMA. Kama yamewashinda mwaweza kujitoa

Mfukuzeni mzinzi huko igunga kwanza ili tuwaelewe
 
Power G

Power G

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Messages
3,912
Likes
93
Points
145
Power G

Power G

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2011
3,912 93 145
Hata ukimhadithia mtoto wa darasa la kwanza mkasa huu ataelewa wazi kwamba ni mpango wa ccm wenyewe. Siyo rahisi mtu wa CDM achome moto nyumba halafu aache ujumbe wa maandishi unaosema kwamba "Sisi Chadema ni wajanja".
 

Forum statistics

Threads 1,235,341
Members 474,524
Posts 29,219,277