BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,088
Kusema la ukweli sisi wanawake huwa tunachangia waume zetu kwenda nyumba ndogo. Tukisha olewa na kuweka ndani ndio tunaona tumefika. Tunasahau wakati tukiwa wachumba tuliokuwa tunayafanya hata mkitoka kazini wote ile jioni mzee akiitaji kula matembele mbio unakwenda kuandaa, tena wafanya kumbembeleza " Honey leo njoo ule kwangu bwana.... akimaliza ugali na tembele unaachia viwili vya nguvu akha mtu anaende kwake kulala akiwa mweepeeesiii.
leo uko ndani akitaka unadai umechoka kwani mwanzoni ulikuwa huchoki ana hukujua unahitaji kuwahi kwenda kazini asubui. Wakati style zote ulikuwa unampatia uwe umechoka au hujachoka ulikuwa radhi kumtimizia ilimradi tu asiende nje kwa mrembo mwingine. Leo ati umechoka kilicho kuchosha ni nini?
Wanawake tubadilike. Tuliwazoeshe wenyewe hawa waumezetu kipindi cha kuchumbiana.!
Sio nawasema wanawake tu nanyi wanaume pia ukisha amua kuowa basi wale uliokuwa nao nyuma waache, eti mmnakamsemo kenu " PENZI LA HAWARA HALIFI" ukiwa unapewa huduma zote hadi kubebwa mgongoni kinachokupeleka nje kipi? Tulieni na wake zenu.
Kumbuka yale uliokuwa unamfanyia mkeo kipindi cha uchumba utakapo acha kumfanyia basi nae kwasababu anakosa ile huduma ya mwanzo ndipo anapokwenda kwa mlizi,shamba boy, dereva hata house boy pia. Utakuta mwanaume akisharudi mkewe yuko moto jamaa anagusa tu alafu anakoroma unategeme nini kama mkeo haendi kupindwana wafanyakazi wako.
Maneno mazuri sana kuhusiana na pande zote mbili ambayo yamejaa ukweli mtupu.