MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,563
Mara nyingi nimeshasikia watu wakishangaa kwa bwana fulani kutembea (sex) nje ya ndoa yake na mwanamke ambaye pengine havutii kihiiiivyo kama mkewe wa ndoa. Au mwanamke kutembea na kijibwana ambacho hakina A wala B compared na Mr wake.
Na mara nyingi wote ukiwauliza wanatoa sababu nzuri tu za kuwafanya wao wakubaliwe huo udhaifu wao. Utasikia mume akidai kuwa the woman -anajua mapenzi, ananifanya nijisikie mwanaume, has more time for me, ananiheshimu e.t.c.
Na mke akiulizwa vipi mbona unatembea na kibarua wenu atajibu either Ananifanya nijisikie vizuri, ananifanya nijisikie wa maana, anajua pa kunigusa n.k

Na wakati mwingine tunaambiwa kuwa nyumba ndogo zina ufahamu wa hali ya juu kuhusu kile ambacho tunakikosa majumbani mwetu kwa wenzi wetu so tunakimbilia kwao ili tuvipate either kama ni feelings /hisia ambazo sisi kama wanandoa hukosa kwa wenzi wetu na kuamua kwenda kutafuta sehemu kwao.
Sijui lakini hawa watu tunaotembea nao nje ya ndoa (nyumba ndogo, ving'asti e.t.c) wanaonekana wako smart sana kujua tunachokikosa ndani ya ndoa zetu.
Swali langu ni je wanajuaje kuwa tunamiss hiki na kile katika ndoa zetu? Tunawaambia wenyewe au?