Nyumba ndogo sasa basi

Nyumba ndogo sasa basi

mmmh dhana ya kujiheshimu napingana nayo kabisa kwa sababu angekuwa anajiheshimu asingetembea na mume wa mtu angetafuta wa kwake labda kama unamaanisha heshima nyingine sio ninayoijua mimi.

Asnam, mwongozo tafadhari? Hapo kwenye Bold hivi mwanamke anatafutaje mwanaume?
 
huyu bi mdogo naona kama ananifaa sana.. plz natafuta mke kama huyu
Habari wana MMU.

Kwa kweli nimeamua mwenyewe kwa dhati kabisa naachana na mambo ya nyumba ndogo. Kwa zaidi ya miaka sita sasa sijawahi hata siku moja kuhisiwa na wife kwamba na-cheat ila nimeamua kumrudishia haki yake ya msingi ya kuwa na mimi wakati wowote.

Nimekuwa nikiamini hizi nyumba ndogo zina umuhimu mkubwa sana katika kujenga nyumba zetu, wamekuwa wakijaza pale palipopungua kwa mke, nimekuwa na bahati kubwa ya kukutana na nyumba ndogo zenye amani, wenye furaha, wanaomheshim mke wangu, sio wasumbufu, wasio tegemezi lakini pamoja nahayo yote leo nasema IMETOSHA.

Lakini wakati naelekea maamuzi haya niliwaza changamoto zilizo mbele yangu (hapa ndipo michango yenu na uzoefu wenu unapohitajika zaidi):

1. Hii nyumba ndogo nilienae sasa ana upendo wa dhati (nionavyo mimi), ni mwanamke anestahili kuwa mke wa mtu (namfaham kwa mwaka sasa), ana haiba, anajua kusamehe bila kuombwa msamaha, anajiheshim, ananiheshim na mke wangu pia, anadai anawapenda hadi wanangu (sina hakika). Najua ataumia kuachana na mm, je, nitakuwa na tofauti gani na wanaume wengine wanaowaumiza wanawake waliowapenda kwa dhati??? Nitakuwa nimetenda wema kwa wife, lakini hisia za huyu ninaemwacha hazipaswi kufikiriwa/kuheshimiwa ikiwa hajanitenda ubaya wowote?

2. Je, ni busara kumwacha kwa kumwambia nia yangu ya dhati? Sijawahi kuacha mwanamke kwa kumwambia hapo kabla (hili linanipa mashaka utekelezaji wake)

Mwisho: Niwashukuru wote mliochangia kunifikisha kwenye uamuzi huu kutokana na post zenu, Mtambuzi, watu8, MadameX, HorsePower, Heaven on earth, Mentor, Evelyn Salt, Fixed Point, ......... list ni ndefu sana natamani niwataje wote ila mda wenyewe ndio hivyo hautoshi.

Nitapokea mawazo yenu (unaruhusiwa kushauri, kuponda, kukatisha tamaa, kupongeza .......).

Thanks MMU members.
 
Mie nashangaa mwanaume unaweza iba nje sasa ulimtongozaje kama haujui kujichomoa, eti unafikiria au hujui kuwa na maneno unayomwambia ndio utajuta?

Kwanza nikuambie wewe ni mmoja wa wanaume mnaotia aibu hapa duniani, na ninaomba mungu sasa, leo au kesho mkeo ajue kuwa ulikuwa unatembea nje.

Mie sipendi wanaume wa aina yako, halafu hauna aibu kuja hapa kusema haya na kuomba ushauri kwetu eti tukusaidie mtu mzima hata uamuzi huwezi fanya mwenyewe ila unajua kwenda kuingia kitandani na wanawake wengine wasio wake zako bila kujali afya na maish aya wanenu.

Unashangaza sna, nakusikitikia kuwa hauna nguvu za kujiita muiba nje as haujui nini unataka duniani, na kukuakikishia leo huwezi kuacha maana ungekuwa kweli unataka kuacha basi ungeongea maneno tofauti ya kwanini unataka, umeshasema mkeo ana mapungufu basi hayo kama bado hayajaisha utaiba tu nje.

wanaume wengi huenda nje kwa mchezo na kuwa kama vijitoto ambavyo havijawahi kuona mwanamke sasa wewe mmmh sijui nini kilikupeleka nje.

n.b. nimeona wanawake wengine wanaumia na watu kama nyie wanaume msiojua kufunga suruali huko nje.

acha hiyo tabia na usali Mungu akusamehe, au mkeo atajua tu hata ya zamani ataambiwa na utakomaje.

hizo pesa unazotoa huko nje unajua zingesaidiaje nyumbani kwako? hata kama unazo vi extra vingefanya kitu kama ungempa mkeo awaendeleze pia.

Aisee una jazba ile mbaya. Huyo wako siku ukimkamata!!!!!
 
Hongera sana mkuu! Mi
mwenyewe ni nyumba ndogo ya mtu, namwambiaga hivo hivo lakini simaanishi
hata chembe, napoteza nae muda tu coz ni kijana mwenzangu na sijaolewa,
wala sijawahi kumwomba pesa wala kumsumbua mke wake. Ila hata akiamua
kuniacha sitaumia coz sina future nae. Tunakaribia mwaka sasa

usije ukawa ndio wewe anayekuzungumzia,maana maelezo yenu yanafana.
sema tu hamjuani kama wote mpo jf kutokana na ID zenu fake
 
Hivi huwa kuna nini huko nyumba ndogo kisichopatikana nyumba kubwa? Nina miaka 15 na wife na sijawahi kufikiria kuwa na hiyo nyumba ndogo. Jamaa anadai amekuwa na nyumba ndogo nyingi bila wife kumshitukia na it seems kwake ni kama kutimiza wajibu vile mpaka anaona huruma kwa nyumba ndogo anayokusudia kuiacha. Napata picha kuwa ndoa si kama tunavyoifahamu bali ni kila mtu anavyotaka kuimaanisha!
 
Men are very selfish!!complicated,------ and crayz!(some of),

women are very complicated,we dont knw what they want,and stupid in a weird way!(some of)

human beings are complicated!
anyway what happened happened, kama umeamua,mwambie mkeo kajua so mstopishe kidogo,then from there uanze kumshutdown taratibu.
After sometime mtaachana.
 
Mwambie tu kuwa unarudi kwa mkeo mazima! Atakuwa wa ajabu kama katika mahusiano yenu yote hakutegemea hilo kutokea.
 
Asante sana, nimefurahi kwa niaba ya mkeo. ingekuwa kanisani tungesema injili imetema!kumbe tuseme jamii forum imesaidia ndoa. sasa huyo wife material kwa nini hajaolewa?
 
Namshukuru Mungu sijawahi kufikiria kuwa nyumba ndogo maana naelewa iko siku tuu huyo jamaa atarudi kwa mke wake halafu nianze kumanga manga.! Mmmh...!
 
Back
Top Bottom