Nyumba ndogo Mbagala

Nyumba ndogo Mbagala

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,395
Reaction score
13,266
Jamaa mmoja alikwenda baa na mtoto wake mdogo mwenye umri wa miaka 4. Rafiki yake akaja na mazungumzo yakawa hivi:

RAFIKI: Habari za za leo rafiki yangu, siku hizi huonekani!
JAMAA: Ah, nipo rafiki yangu, si unajua tena mambo ya nyumba ndogo? Siku hizi kila nikitoka kazini lazima nipitie kwanza Mbagala kwa nyumba ndogo.

Baada ya wiki moja jamaa akapewa notisi na mwenye nyumba kutokana na kushindwa kulipa kodi. Wakiwa wamekaa wasijue pa kwenda na mkewe akilalamika mambo yalikuwa hivi

MKE: Unaona baba nanihii kila mara nilikuwa nakwambia tujenge hata kibanda kidogo unasema huna hela wakati wenzio mnaofanya nao kazi wameshahamia kwenye nyumba zao.

Kabla mume hajajibu mtoto akaingilia kati huku akimshika mkono baba yake kama namna ya kumkumbusha kitu,

MTOTO: Baba, siku ile tulipokuwa pale baa, rafiki yako Magumashi alikuuliza mbona huonekani, ukajibu kuwa kila siku ukitoka kazini huwa unapitia kwenye nyumba yako ndogo Mbagala. Sasa baba kwanini tusihamie tu huko hata kama nyumba ni ndogo mbona sisi wenyewe tupo watatu tu na hapa tunakaa chumba kimoja. Tena baba hata kama haijaisha, si utamalizia tukiwa humo humo kuliko kila siku huyu baba mwenyenyumba anakuja kukupigia kelele?
 
Hahahahahahahaha!! Madogo hawakopeshagiii! Baba lazima suruali ilimvuka! Hehe! So funy!!
 
Hivi aliona ni sifa kumpeleka mtoto wake nyumba ndogo? Watoto wa umri huo huwa wana photographic memories na wanaretrieve kama walivyoona.
 
Back
Top Bottom