Wanaume wengi wanaojikuta wameangukia ktk nyumba ndogo,tena wakaishi na amani sana huko zaidi ya nyumba kubwa nadhani wanawake wa nyumba kubwa mnahusika kwa kumsababishia mume kutafuta kajumba kadogo, haya dada zangu nambieni ni kweli? Msije mkaanza kuniambia eti ooh! Wanaume wanatamaa,mie naamini sio tamaa ila kuna tu cheche twa mapenzi ya zamani mmetupunguza ati! Zamani neno honey,baby,dear, na mengine kibao yalikua yapo katika ncha ya ulimi,ukipita utasikia honey,uone gari utasema kama la sweet wangu,ukijikwaa utasikia ooh! My love kanisema huko aliko.lakini baadae yoooote mnayafuta,nyie Nyumba kubwa ndio mnasababisha mume awe na bi mdogo.