'Nyumba ndogo' huimarisha 'nyumba kubwa' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Nyumba ndogo' huimarisha 'nyumba kubwa'

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tuko, Aug 26, 2010.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kuna aina kuu 2 za nyumba ndogo

  1. Type I; Ambayo mwanaume akiwa nayo humnyanyasa mkewe, huchelewa kurudi home bila maelezo, humpiga mkewe endapo akimuuliza au kumfumania, hatoi matumiz ya kutosha home, mostly anapeleka kwa nyumba ndogo n.k. Mara nyingi nyumba ndogo hizi huzaa na huyo mwanaume.

  2. Type II. Ambayo mwanaume anakuwa nayo kwa siri sana, hapendi mkewe hata ashuku, mapenzi huwa ya siri kubwa na nyumba ndogo yenyewe inaambiwa kabisa i-'behave' ikijua kuwa kuna mwenye mali yake.

  huwa kuna intermediate kati ya hizo mbili pia...


  Mi naongelea type II. Hii, KIMSINGI huimarisha mapenzi ya mwanaume kwa mkewe (au GF, au mchumba).

  Kwa nini
  - Mwanaume akiwa na nyumba ndogo kwa siri, hujitahidi sana mkewe asishtuke. Katika kufanya hivi, mambo anayofanya kwa kiasi kikubwa huongeza upendo kwa wife. Kwa mfano kama anajua kesho anatoka na small house, basi leo atarudi hom mapema, sometimes ataleta zawadi, atakuwa mnyenyekevu ili baadae akitoa taarifa kuwa 'wife kesho nitakuwa na ka-kikao Kibaha, may be nitachelewa kidogo kurudi' bas wife anakuwa mpole na hahis kitu. Tena siku hiyo atajitahidi hata kama ni gem akamue kwa juhudi na utaalam wote, ili wife kesho yake asiwe saaana na apetite.

  All in all ni kuwa katika kuficha madhambi yake kwa wife, mwanaume mwenye nyumba ndogo type II, hufanya mambo mazuri kwa mke ambayo asingeyafanya tu katika hali ya kawaida...

  Nawakilisha...
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ....Nakubaliana na hizo aina mbili za small house lakini sikubaliana na the fact kuwa zinaimairisha ndoa kwa namna yoyote ile......! vinginevyo sijui maana ya ndoa imara hapa......! kutembea na mke nje ya ndoa kwa namna yoyote ile ni kuivunja ndoa, ni kuisaliti ndoa ni kubomoa ndoa...!
   
 3. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,481
  Likes Received: 2,072
  Trophy Points: 280
  nyumba ndogo mara nyingi uwa zinavuruga sana ratiba ya kuwa na familia pamoja na pia inaharibu bajeti na mipango ya maendeleo hivyo huwezi kusema kuwa zinaimarisha nyumba

  Hiyo type II ni nzuri kwa mtu mstaarabu na mwenye mapenzi ya kweli na mkewe so at least inapunguza maumivu. Mimi nimepitia kidogo kwenye hizi nyumba ndogo tofauti tofauti ingawa kwa sasa nimeacha karibia unafika mwaka sijawa na small house

  Nyumba ndogo ni wajanja sana na uwa wana-act kutokana na wewe ulivyo kwa mfano kama wewe unampenda sana mkeo kuliko yeye na yeye analijua ilo basi na yeye atakupa muda mrefu na mkeo na ataheshimu unachomwambia juu ya mkeo na hata kukukumbusha muda wa kurudi nyumbani ili usije kuaharibu maana anajua wazi kuwa ukiharibu nyumbani inaweza kuwa sababu tosha kumtosa yeye na hawa mara nyingi (type II) uwa wako money oriented kuliko type I wana malengo ya kukuchuna zaidi hivyo ingawa mkeo hawajui ila bajeti upungua sana nyumbani kwa visingizio mbalimbali

  Type I mara nyingi uwatokea watu ambao hawajali kuachana na mke wake yaani wamekolea zaidi kwa nyumba ndogo kuliko kwa mkewe na hawana mapenzi ya dhati kwa wake zao. Hawa wako radhi hata kurudi asubuhi na akiulizwa uwa mbogo na mara nyingine wakidatishwa sana wanaweza hata kumpa small house simu apokee pindi mkeo anapopiga

  Ushauri kwa wana nyumba ndogo ni kwamba:
  Jitahidi sana kutojiachia 100% kwa nyumba ndogo inabidi uwe akili kichwani sana tune akili yako kuwa pale unapita tu na kuwa muwazi kuhusu uhusiano wako na mkeo kuwa ueshimike na weka mipaka mapema na pia jua kabisa yule si mkeo ni wakupita tu na uwe makini sana kwa hilo ukibweteka tu umekwisha na utaterekeza familia

  Najua kuna watu watanimind kuwa napenda nyumba ndogo ila hapana kuna mara moja moja mtu unatereza ila kwa sasa nimeachana na hivyo vitu ingawa siweki guarentee kuwa sitarudia tena maana ubinadamu kazi
   
 4. t

  tumwe273us Member

  #4
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli kuwa type2 inaimarisha uhusiano wa mme na mke.but sioni km ni kitu chema hata kidogo.km umeamua kuoa na umeamua kuishi na mke au mchumba au vyovyote utakavyoamua kuita,why nyumba ndogo!
  Nawashukia sn wanaovaa suruali km mwanaume lijali thn wanakuwa na nyumba ndogo na haishali whc type but all in all ni kupoteza ela tu.
  WAHENGA WALISEMA,MPENDA VYOTE HUKOSA VYOTE.
   
 5. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,481
  Likes Received: 2,072
  Trophy Points: 280
  usije kuapa kabisa kuwa sitakuwa na nyumba ndogo au kuona wenye nyumba ndogo kama ni vichaa tema mate chini kabisa haya mambo ya mapenzi ni ya ajabu sana unatakiwa kumuomba Mungu tu ila usijiapize

  halafu piga hodi kwanza na ujitambulishe sio unaingia tu kama ******
   
 6. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Zote hizi zinaashiria kutokuwa na mapenzi mema na mwenzio...! Na zote ni sumu ya maendeleo ya familia, hata hivyo ni udhalilishaji wa mwenzio...! Lakini pia sio njia ya kulipiza kisasi kwa mwenzio (kama yeye anakuwa na mume mdogo)....! Kama imekulazimu ni bora ukamleta nyumbani awe nyumba ya pili, lakini sio nyumba ndogo....! Kama unaamini hivi, basi uamini pia kuwa kuna wakati mkeo akitoka nje ya ndoa itasaidia ile ndoa yenu kudumu na kuimarika zaidi....! (kitu ambacho unaniuma mimi kama mwanume). La msingi ni kujiuluza, "Je, wewe mwenyewe ungependa kushuhudia hayo yakikutokea?".

  Aidha, uwelewe tu kuwa kwa kila mwanaume mwenye nyumba ndogo mbili, basi anao wanaume wenzie si chini ya wawili....! Na kwa kila mwanamke mwenye wanaume wawili, naye anaye mke menzie mmoja au zaidi....!
   
 7. D

  Dick JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aina ulizotaja au zaidi zipo, lakini hujaeleza hiyo ya II inaimarshaje nyumba kubwa. Vinginevyo withdraw hoja yako.:playball:
   
 8. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Ni upuuzi mtupu. Hakuna kuimarisha ndoa (nyumba kubwa) hapa. Ndoa iliyoimarika haina nafasi kwa nyumba ndogo kwa namna yoyote ile. Unaweza ukawa unaishi na jambazi kwenye nyumba au mtaa mmoja lakini ujambazi wake anauficha sana watu hawajui na kwenye nyumba za ibada hakosi na shughuli za kijamii anashiriki sana lakini hii hamfanyi kuwa si jambazi.

  Kwa vigezo vyovyote vile nyumba ndogo hubomoa ndoa (nyumba kubwa) - Penzi haligawanyiki hata kidogo that's it.
   
 9. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #9
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Jibaba bonge, pamoja na Dick..

  Sio kwamba nahubiri kuwa nyumba ndogo ni kitu kizuri. Najaribu kufanya retrospective analysis...

  Hata kama sio wewe, lakini kama unaishi katika jamii ya KITANZANIA, (kwa herufi kubwa), basi utakuwa unaweza kukadiria ni asilimia ngapi ya waliooa wana nyumba ndogo. Katika mazingira ninayoishi mimi ni zaidi ya 50% pengine. Inaweza kuwa wa kudumu au wa muda, mtaani au ofisini n.k. Observation zangu zinaonyesha kuwa wanaume wenye nyumba ndogo type II, wako makini zaidi kuhakikisha hawawaudhi wake zao ili kuondoa shaka yoyote ya kushtukiwa. Wapo wengi ambao hawana nyumba ndogo lakini ni amkini kwa wake zao sikatai, lakini kwa ninavyojua mimi mara nyingi wanaume wanajisahau.
   
 10. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Basi change hiyo heading ya thread yako otherwise my post still holds
   
 11. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #11
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,726
  Likes Received: 3,144
  Trophy Points: 280
  Type I hutokana zaidi na mwanaume married a woman by chance not love of his life. Type II ni tamaa.
   
 12. p

  pori Member

  #12
  Aug 27, 2010
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nyumba ndogo ni upuuzi mtupu! cha tofauti unachopata huko usichoweza kukirekebisha kwa mkeo ni nini katika dunia hii ya maradhi kibao? pia ya nini kuishi maisha ya shida ya kujifichaficha? siku nikigundua wa kwangu ana nyumba ndogo nami natafuta nyumba ndogo pia ili nae a=feel the pinch
   
 13. m

  mpangwa1 JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 279
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  vipi umewahi kula mahindi ya kuchoma watu utaonawanachangua yale mahindi mateke hivi hata kwa nyumba dogo tupo laini nyumba kubwa imeshakoma meno hayanachoka haraka
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Aug 27, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Kama ametafuta nyumba ndogo ni kutafuta chanzo kilichosababisha mwenzio akawa na hiyo nyumba
   
 15. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  :nono::nono:
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Haswa, We are on the same track
   
 17. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #17
  Aug 27, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hamna lolote ni ukosefu wa maadili tu, mtu anafiri anasolve one problem kumbe ana create other problem.
   
 18. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  "Lakini kwa sababu ya ZINAA kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe, mume ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; na vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu." (1 Wakorontho 7:2-5)
   
 19. Ngomo

  Ngomo Senior Member

  #19
  Aug 27, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 199
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45

  kama unanyumba fifkiri mke wako naye anka serengeti boy
  je unaweza kumvumilia?
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  "Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka….. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, UASHERATI, uchafu, ufisadi…… na mambo yanayofanana na hayo; katika hayo nawaambia mapema kama nilivyokwisha, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu." (Wagalatia 5:16-21)


  "Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili, bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kutii. Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili, bali mwaifuata roho." (Warumi 8:5-9).
   
Loading...