'Nyumba ndogo' huimarisha 'nyumba kubwa'

Nyumba ndogo ni kama gari bovu. Ina gharama kubwa za ukarabati, mafuta, spea, kusukumwa, kuvutwa, kuchaji, na hasa kuchomelewa chini mara kwa mara. Iepuke.
 
Hizo ni type za Umalaya na Malaya ndio wanaozijua sana. Mimi najua huwa hakuna nyumba ndogo zilikuwepo enzi za mababu tu na zilikuwa zinajulikana kwa nyumba kubwa. hayo unayoongelea wewe ni aina za umalaya, na jinsi unavyoweza kuwa Malaya zaidi bila mkeo kujua. Period !
 
Hakuna nyumba NDOGO yoyote inayoimarisha nyumba kubwa. Huo ni UZINZI na kukosa maarifa! ZAB 6-32 '' Mtu azinie na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza mwenyewe''
 
Hizo ni type za Umalaya na Malaya ndio wanaozijua sana. Mimi najua huwa hakuna nyumba ndogo zilikuwepo enzi za mababu tu na zilikuwa zinajulikana kwa nyumba kubwa. hayo unayoongelea wewe ni aina za umalaya, na jinsi unavyoweza kuwa Malaya zaidi bila mkeo kujua. Period !


Mzee Taratibo.. Punguzo ukalo wa maneno! Tafadhalo!
 
Kuna aina kuu 2 za nyumba ndogo

1. Type I; Ambayo mwanaume akiwa nayo humnyanyasa mkewe, huchelewa kurudi home bila maelezo, humpiga mkewe endapo akimuuliza au kumfumania, hatoi matumiz ya kutosha home, mostly anapeleka kwa nyumba ndogo n.k. Mara nyingi nyumba ndogo hizi huzaa na huyo mwanaume.

2. Type II. Ambayo mwanaume anakuwa nayo kwa siri sana, hapendi mkewe hata ashuku, mapenzi huwa ya siri kubwa na nyumba ndogo yenyewe inaambiwa kabisa i-'behave' ikijua kuwa kuna mwenye mali yake.

huwa kuna intermediate kati ya hizo mbili pia...


Mi naongelea type II. Hii, KIMSINGI huimarisha mapenzi ya mwanaume kwa mkewe (au GF, au mchumba).

Kwa nini
- Mwanaume akiwa na nyumba ndogo kwa siri, hujitahidi sana mkewe asishtuke. Katika kufanya hivi, mambo anayofanya kwa kiasi kikubwa huongeza upendo kwa wife. Kwa mfano kama anajua kesho anatoka na small house, basi leo atarudi hom mapema, sometimes ataleta zawadi, atakuwa mnyenyekevu ili baadae akitoa taarifa kuwa 'wife kesho nitakuwa na ka-kikao Kibaha, may be nitachelewa kidogo kurudi' bas wife anakuwa mpole na hahis kitu. Tena siku hiyo atajitahidi hata kama ni gem akamue kwa juhudi na utaalam wote, ili wife kesho yake asiwe saaana na apetite.

All in all ni kuwa katika kuficha madhambi yake kwa wife, mwanaume mwenye nyumba ndogo type II, hufanya mambo mazuri kwa mke ambayo asingeyafanya tu katika hali ya kawaida...

Nawakilisha...

TYPE II... umepiga ikulu... hapo hata babzetu huenda waliangukia humo!!! nway, boora nushu shari kuliko shari kamili!!
 
Mapenzi ni ya wawili. Hata kama nitakuvumilia urudi kwa mkeo, bado utakumbuka penzi langu na utarudi, mbona watu wanapiga simu usiku wa manane na wako na wake zao. Halafu ukigundua mie ndio nayekupenda kweli, nakwambia hata hilo neno la nyumba ndogo utaliacha maana ni kama kumdhalilisha anayekupenda ati unamwita nyumba ndogo. Na hapo mtu kila kitu najitegemea nina biashara zangu sichukui hata senti yako, ni penzi tu, sikubanii hata ukiwa na shida inahusu hela nakupa, lazima mwanaume utaona haya kidogo wanadamu tumeumbwa na haya, kama sijawa mwangalifu utahamia tu. Halafu kumbuka pia mwanamke anahitaji zaidi ya penzi anahitaji mtoto, unafikiri itakuwaje hapo. Umeshazaa nae, bado utasema nyumba ndogo sijui nini? Huwezi kuita nyumba ndogo mtu ambaye humtunzi, hapo ni kukoseana heshima.
 
Mimi naona hizi nyumba ndogo ni source of problems ndani ya familia zetu,imagine baba anamnyima mwanae pesa ya ada then mtoto wa huyo nyumba ndogo ambaye huyo baba wala si mwanae anapewa ada na kila kiti eti kisa baba kadata na penzi la mama mtu hii ni nini kama si ulimbukeni.Mwisho wa siku mwanao wa kumzaa anakua kibaka kwa kukosa elimu bora then mtoto wa mwenzio anakua na maisha bora.
 
mmmh na walaaniwe wanaume wote wenye nyumba ndogo hapo naona kama hoja tu inatetewa:mad2:
 
Wanaume wengi wanaojikuta wameangukia ktk nyumba ndogo,tena wakaishi na amani sana huko zaidi ya nyumba kubwa nadhani wanawake wa nyumba kubwa mnahusika kwa kumsababishia mume kutafuta kajumba kadogo, haya dada zangu nambieni ni kweli? Msije mkaanza kuniambia eti ooh! Wanaume wanatamaa,mie naamini sio tamaa ila kuna tu cheche twa mapenzi ya zamani mmetupunguza ati! Zamani neno honey,baby,dear, na mengine kibao yalikua yapo katika ncha ya ulimi,ukipita utasikia honey,uone gari utasema kama la sweet wangu,ukijikwaa utasikia ooh! My love kanisema huko aliko.lakini baadae yoooote mnayafuta,nyie Nyumba kubwa ndio mnasababisha mume awe na bi mdogo.
 
Kwa taharifa wengi hawaamii huko nyumba ndogo wanaenda kuchungulia tu. Wanaoamia wala hawaishi kwa amani. Juzi kati tumetoka kumzika mmoja just a year baada ya kuhama nyumba kubwa.

samahani mzee,nahisi unajua mengi zaidi ya hapo tafadhari funguka japo kidogo, jina lako tu linatosha kabisa kutuonyesha kuwa ulikuwa na maana.
 
Kwa taharifa wengi hawaamii huko nyumba ndogo wanaenda kuchungulia tu. Wanaoamia wala hawaishi kwa amani. Juzi kati tumetoka kumzika mmoja just a year baada ya kuhama nyumba kubwa.

inawezekana kitendo cha kuhamia nyumba ndogo ndo kime m-cost?
 
ubazazi tu wa mwanadamu!kazi ya kuboresha ndoa si ya mwanamke peke yake!
kabla hujaenda nyumba ndogo jiulize umefanya mangapi kuifanya ndoa yako iwe mpya!
we mwanaume tu ubaki na likitambi lako mchakato wa kueleweka hutoi,.hutoi pesa ya kumpendezesha huyo mke,dada zako wanamkera mkeo na uchimvi kila uchao,huna mawasiliano sahihi na mkeo kila siku maagizo tu ka yuko na babake mzazi au mkwewe,umemzalisha mkeo watoto kama kumbi kumbi,pesa ya matumizi unahesabia kweny mfuko,humuamini mkeo,hujali jitihada zake,humkuzi kifikra ili ajiamini unapata wapi guts za kusema nyumba kubwa imekusababishia nyumba ndogo?!JUSTIFICATION TU HIZO!
 
Lakini ni kweli kwani katika mapenzi vitu vidogo vidogo vinasababisha wanandoa kutofautiana. Mwanamke akishaolewa tu anaanza insecurities zake na kuhisi vitu vya hajabu hajabu kiasi kwamba kila muda anamuhisi mumewe yuko na house girl ama secretary. Mume akichelewa kidogo tu kurudi nyumbani anatupiwa maneno ya kashfa. Sasa kwa mpango huu mwanamme gani atakuwa na furaha ya kuishi na vuvuzela la namna hii? Solution inakuja kwenye nyumba ndogo na nyumba ndogo akiwa mshirikina ndo unasahau kabisa kurudi kwa nyumba kubwa.
 
ubazazi tu wa mwanadamu!kazi ya kuboresha ndoa si ya mwanamke peke yake!
kabla hujaenda nyumba ndogo jiulize umefanya mangapi kuifanya ndoa yako iwe mpya!
we mwanaume tu ubaki na likitambi lako mchakato wa kueleweka hutoi,.hutoi pesa ya kumpendezesha huyo mke,dada zako wanamkera mkeo na uchimvi kila uchao,huna mawasiliano sahihi na mkeo kila siku maagizo tu ka yuko na babake mzazi au mkwewe,umemzalisha mkeo watoto kama kumbi kumbi,pesa ya matumizi unahesabia kweny mfuko,humuamini mkeo,hujali jitihada zake,humkuzi kifikra ili ajiamini unapata wapi guts za kusema nyumba kubwa imekusababishia nyumba ndogo?!JUSTIFICATION TU HIZO!

unajua ndio maana ukawa mwl...........i love that. ngoja niongezee hapa

wewe ni mwanaume hujali hisia za mkeo wala fikra zako na kama hana kipato ndo kabisa mateso na masimamngo kazi moja. huendi outing na mkeo, hulali kwa amani na mkeo ukienda bar unacheka hadi jino la mwisho ukirudi home umenuna kama umelisha flagyl. watoto hawajui upendo wa baba mkeo kazoea kubakwa kila siku wamrudia saa saba nane uko kikomba zaid kisha unambaka hakuna kuoga wala kupiga mswaki binti wa watu anavumilia tu kisa ni mume. siku akikuuliza kipigo kinatembea eti unautendea haki uanaume wako sasa wategemea nini?

haya umeipata utaish huko, yeye atalea wanae kwa tabu na raha wale wa chumvi ama wabure alimradi maisha yasonge, anajitahd akijua watoto si mawe useme hawatakuwa wala si gogo useme litaliwa na mchwa wanakuwa wanafika mbali wanaanza kumlea mama kwa mapenzi ya dhati hali wakikumbuka kwamba baba uliwatesa, hadi wengine wakawa na chuki nafsin mwao. wewe kuona nyumba kubwa kwa sasa iko paradiso unarudisha miguu na kwa aibu kama vile ulifukuzwa.shame on you.

kwa upande wa pili

wewe mama Mungu kakubariki kwa ndoa njema ambayo mumeo anakuthamini na kukupenda basi jitahd na wewe kuonyesha upendo wako. usibweteke eti ni wangu huyu hatoki utalia mchana wa jua kali. jua kwamba hiyo ndoa ni amana inatakiwa izae so kila siku kama mumeo ni mstaarabu na wewe ongeza ustaarabu zaid yake na kama sio basi wewe usiondoe ustaarabu wako. hakikisha bidhaa yako unaipathamani kila siku ili mteja wako nae aipende kila siku.

ngoja naingia pindi baada ya dk 80 narudi tena.
 
Ki ukweli kuna baadhi ya ndoa ambazo vituko na mwenendo wa mke ndani ya ndoa unachangia kwa kiasi kikubwa mwanaume kutafuta nyumba ndogo kwa minajri ya kujiburudisha. Kwa mfano kuna wale wadada wanaotumia kigezo cha kumnyima unyumba mumewe hata kwa miezi 3 kwa sababu ndogo tu ya kutofautiana kauli au misimamo. Kuna wale wengine unakuta haongei na mume, kila kitu anafanya kwa vitendo au kumtuma housegel, kuna wengine nyumbani ni ukali tu na kupayuka nk unafikiri mwanaume gani ataweza kuvumilia?

Ila nakubali pia wamo wanaume ambao wanatabia za kuwa na nyumba ndogo hata kama mke atajitahidi vipi! Hawa kwa kweli wanahitaji maombi, LOL!
 
nyumba ndogo ni matokeo ya uzinzi na umalaya tu wa wanaume......

Kama ups n downs za mahusiano wote wanawake na wanaume yaani mke na mume hupitia ila mke anastick kujenga ndoa wanaume kwa tamaa zao hutoka nje......
 
Back
Top Bottom