Nyumba imejengwa juu ya kaburi la Abushiri bin Salim al Harith

Shukrani...Pia tukumbuke kua Pwani yetu iliwai kua na vita ya kidini kati ya Waislam na Wakristo kuanzia Waarabu na Wareno na mwisho. Wakristo wakiwa wanaongozwa na Wajeruman..huku makabila mengi ya pwani yakiwa tayari yameupokea Uislam kitu kilichowachukiza watubkutoka Ulaya...yaani Wareno na Wajerumani.
(CRUSH OF CIVILIZATION)
 
Kaka picha yako ya historia ni ya ajabu! na mbali na uhalisia. Wareno kufanya vita ya kidini? Mbona walikaribishwa na watawala wa Malindi ilhali walipigana pamoja nao dhidi ya Mombasa - hadi kujenga ngome kule shauri ya bandari bora?
Wajerumani walikuja na kuvamia Tanganyika kwa kutumia jeshi la Waislamu (soma juu #87: jeshi lao lilikuwa maafisa 21 na masajini 40 kutoka Ujerumani, askari mamluki Wasudan (wote Waislamu) 600 walioongezwa na Wazulu 150 kutoka Msumbij) - shule yao ya kiserikali ya kwanza walijenga Tanga ambako walimwajiri hata shehe kwa vipindi vya dini, maana walitegemea hasa Waislamu kwa utawala wao kama maakida na wasaidizi.
Hapakuwa na vita ya kidini.
 
Wahoo nashukuru sana kwakuliona ili kwa ukaribu sana...Bila shaka picha yako ya Historia kuna mambo aiwezi kukuonyesha mkuu...(CRUSH OF CIVILIZATION)
Wazungu hao walikua wajanja sasa bira Waarabu ( Waislam ) na Waafrika bila kujua. Waliwatumia hao hao kupigana vita hiyo na mwisho kusimika himaya zao..za Kireno ,Kijeruman na badae Kiingereza. Najua inawezekana ukufundishwa au ukusoma kinaga ubaga Historia ya Pwani,Vita ya Kidini na Kuja kwa Wageni...ndiyo maana huko mbeleni ili kutangaza ushindi wa Ukristo dhidi ya Uislam...ili motto IDD aende shule basi ilibidi aitwe Augustine au Jakaya etc
 
Samahani kaka hueleweki. Juu ulidai eti kulikuwa na vita ya kidini Tanzania ukitaja mifano ya wakoloni Wareno na Wajerumani. Nimejibu wote hawakupigania vita ya kidini, kinyume walishirikiana na mtu wa kila dini aliyepatikana kuwasaidia. Bila kutegemea (sehemu ya) Waislamu wasingeendelea.
Vita ya kidini ilipiganiwa mwaka gani, na wapi?? Abushiri 1888-89 haikuwa vita ya kidini: upande wake walikuwa Waislamu na Wapagani; Upande wa Wajerumani walikuwa Waislamu na pia Wapagani.
Vivyo hivyo Maji Maji 1905-07.
 
Mkuu bila shaka utakua mgeni wa Hidden Agenda ya kuwepo Wareno,Wajerumani na Waingereza na kupindua uwepo wa Waarabu katika pwani ya Afrika Mashariki... Tujifunze zaidi Historia...CRUSH OF CIVILIZATION. Au ndugu ulitaka wakuandikie Religious War..aaha the motive of Europeans at the E.African Coast ..Ibin Batuta et all..
 
Bado hueleweki. Sijali Hidden agenda. Nilikuomba utaje mwaka na mahali pa vita ya kidini katika Afrika ya Mashariki.
Hakika Ibn Battuta si mfano kwa hoja lako. Aliaga dunia mnamo 1377, wakati ule Wareno hawakuanza kusafiri Afrika ya Magharibi, wala upande wa Mashariki.
Wazungu walifika Afrika ya Mashariki kwanza ni Wareno waliotaka kufika Uhindi; walihitaji vituo vya kupumzika njiani kwa vyombo vyao; halafu wafaransa waliofika Kilwa kwa sababu waliweza kununua hapa watumwa kwa mashamba yao kwenye visiwa vya bahri hindi, lakini hawakujaribu kuwa na vituo vya kudumu. Walifika kama wateja wa wafanyabiashara ya watumwa kwenye pwani. Baadaye Waingereza walifika kutoka Uhindi (walikuwa na meli bora, hawakuhitaji vituo Afrika) kupambana na biashara ya watumwa.
Tangu kuingia kwa Wajerumani waliotafuta koloni, ambako walitegemea jeshi lao lililofanywa na mamluki Waislamu kutoka Sudani.
Wapi vita yako?? Ufichue hidden agenda!
 
Vita hii ilianza pale Wazungu kutoka Ulaya walipo wasili pwani ya mashariki ingawa ilianzia Kusini mwaafrika.
Yaani unashangaa Wazungu kuwatumia Nubian chini ya Emin Pasha ...mkuu.
Mbona ata waafrika walitumiwa na wazungu kupambana na waafrika kama Sangu,Bena,Baganda,Kahigi -Kihanja nk
Motive moja wapo ya Wazungu kuja Pwani ya Afrika ni dini na kudhibiti kuenea kwa Uislam barani Afrika asa Pwani ya Afrika..CRUSH OF CIVILIZATION.
Inawezekana ukachukua muda kunielewa mkuu
 
Kaka bado hueleweki. Umewahi kusikia kwamba wamisionari Wajerumani walilalamika kuwa jeshi la kikoloni lilisambaza Uislamu kote kwenye koloni??
Wareno walishirikiana na Waislamu wa Malindi kushambulia Mombasa. Wajerumani walishirikiana na Waislamu wa Zanzibar kupata utawala wa pwani.
Wajerumani walijenga utawala wao wa kikoloni katika Tanganyika kwa msaada wa sehemu kubwa ya Waislamu - ilahli Waislamu wengine waliwapinga.
Bado nasubiri tarehe na mahali pa vita yako ya kidini!
 
Historia nzuri sana hii.....

Natafuta sana kujua historia ya mji wa Kilwa...nawasilisha.

Pascal Mayalla JokaKuu zitto junior
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…