Nyumba imejengwa juu ya kaburi la Abushiri bin Salim al Harith

Shukrani...Pia tukumbuke kua Pwani yetu iliwai kua na vita ya kidini kati ya Waislam na Wakristo kuanzia Waarabu na Wareno na mwisho. Wakristo wakiwa wanaongozwa na Wajeruman..huku makabila mengi ya pwani yakiwa tayari yameupokea Uislam kitu kilichowachukiza watubkutoka Ulaya...yaani Wareno na Wajerumani.
(CRUSH OF CIVILIZATION)
 
Kaka picha yako ya historia ni ya ajabu! na mbali na uhalisia. Wareno kufanya vita ya kidini? Mbona walikaribishwa na watawala wa Malindi ilhali walipigana pamoja nao dhidi ya Mombasa - hadi kujenga ngome kule shauri ya bandari bora?
Wajerumani walikuja na kuvamia Tanganyika kwa kutumia jeshi la Waislamu (soma juu #87: jeshi lao lilikuwa maafisa 21 na masajini 40 kutoka Ujerumani, askari mamluki Wasudan (wote Waislamu) 600 walioongezwa na Wazulu 150 kutoka Msumbij) - shule yao ya kiserikali ya kwanza walijenga Tanga ambako walimwajiri hata shehe kwa vipindi vya dini, maana walitegemea hasa Waislamu kwa utawala wao kama maakida na wasaidizi.
Hapakuwa na vita ya kidini.
 
Wahoo nashukuru sana kwakuliona ili kwa ukaribu sana...Bila shaka picha yako ya Historia kuna mambo aiwezi kukuonyesha mkuu...(CRUSH OF CIVILIZATION)
Wazungu hao walikua wajanja sasa bira Waarabu ( Waislam ) na Waafrika bila kujua. Waliwatumia hao hao kupigana vita hiyo na mwisho kusimika himaya zao..za Kireno ,Kijeruman na badae Kiingereza. Najua inawezekana ukufundishwa au ukusoma kinaga ubaga Historia ya Pwani,Vita ya Kidini na Kuja kwa Wageni...ndiyo maana huko mbeleni ili kutangaza ushindi wa Ukristo dhidi ya Uislam...ili motto IDD aende shule basi ilibidi aitwe Augustine au Jakaya etc
 
Samahani kaka hueleweki. Juu ulidai eti kulikuwa na vita ya kidini Tanzania ukitaja mifano ya wakoloni Wareno na Wajerumani. Nimejibu wote hawakupigania vita ya kidini, kinyume walishirikiana na mtu wa kila dini aliyepatikana kuwasaidia. Bila kutegemea (sehemu ya) Waislamu wasingeendelea.
Vita ya kidini ilipiganiwa mwaka gani, na wapi?? Abushiri 1888-89 haikuwa vita ya kidini: upande wake walikuwa Waislamu na Wapagani; Upande wa Wajerumani walikuwa Waislamu na pia Wapagani.
Vivyo hivyo Maji Maji 1905-07.
 
Mkuu bila shaka utakua mgeni wa Hidden Agenda ya kuwepo Wareno,Wajerumani na Waingereza na kupindua uwepo wa Waarabu katika pwani ya Afrika Mashariki... Tujifunze zaidi Historia...CRUSH OF CIVILIZATION. Au ndugu ulitaka wakuandikie Religious War..aaha the motive of Europeans at the E.African Coast ..Ibin Batuta et all..
 
Bado hueleweki. Sijali Hidden agenda. Nilikuomba utaje mwaka na mahali pa vita ya kidini katika Afrika ya Mashariki.
Hakika Ibn Battuta si mfano kwa hoja lako. Aliaga dunia mnamo 1377, wakati ule Wareno hawakuanza kusafiri Afrika ya Magharibi, wala upande wa Mashariki.
Wazungu walifika Afrika ya Mashariki kwanza ni Wareno waliotaka kufika Uhindi; walihitaji vituo vya kupumzika njiani kwa vyombo vyao; halafu wafaransa waliofika Kilwa kwa sababu waliweza kununua hapa watumwa kwa mashamba yao kwenye visiwa vya bahri hindi, lakini hawakujaribu kuwa na vituo vya kudumu. Walifika kama wateja wa wafanyabiashara ya watumwa kwenye pwani. Baadaye Waingereza walifika kutoka Uhindi (walikuwa na meli bora, hawakuhitaji vituo Afrika) kupambana na biashara ya watumwa.
Tangu kuingia kwa Wajerumani waliotafuta koloni, ambako walitegemea jeshi lao lililofanywa na mamluki Waislamu kutoka Sudani.
Wapi vita yako?? Ufichue hidden agenda!
 
Vita hii ilianza pale Wazungu kutoka Ulaya walipo wasili pwani ya mashariki ingawa ilianzia Kusini mwaafrika.
Yaani unashangaa Wazungu kuwatumia Nubian chini ya Emin Pasha ...mkuu.
Mbona ata waafrika walitumiwa na wazungu kupambana na waafrika kama Sangu,Bena,Baganda,Kahigi -Kihanja nk
Motive moja wapo ya Wazungu kuja Pwani ya Afrika ni dini na kudhibiti kuenea kwa Uislam barani Afrika asa Pwani ya Afrika..CRUSH OF CIVILIZATION.
Inawezekana ukachukua muda kunielewa mkuu
 
Kaka bado hueleweki. Umewahi kusikia kwamba wamisionari Wajerumani walilalamika kuwa jeshi la kikoloni lilisambaza Uislamu kote kwenye koloni??
Wareno walishirikiana na Waislamu wa Malindi kushambulia Mombasa. Wajerumani walishirikiana na Waislamu wa Zanzibar kupata utawala wa pwani.
Wajerumani walijenga utawala wao wa kikoloni katika Tanganyika kwa msaada wa sehemu kubwa ya Waislamu - ilahli Waislamu wengine waliwapinga.
Bado nasubiri tarehe na mahali pa vita yako ya kidini!
 
JUU YA KABURI LA BUSHIRI BIN SALIM PAMEJENGWA NYUMBA

Nimesoma historia ya Bushiri nikiwa shule ya msingi miaka ya 1960 pamoja na historia ya Vita Vya Maji Maji vilivyopewa jina la, "Maji Maji Rebellion."

Walioandika historia hii waliwaona Abushiri bin Salim, Abdulrauf Songea Mbano na Bi. Khadija Mkomanile, Mtwa Abdallah Mkwawa kwa kutoa mfano kutoka kundi la viongozi walioongoza vita dhidi ya Wajerumani si chochote ila waasi.

Kama waasi hukumu ya wao kunyongwa ilikuwa stahili yao.

Bushiri alitembezwa nusu uchi katika barabara za Pangani wakati anapelekwa kunyòngwa na huko alikotolewa alipokuwa amefungiwa Bushiri aliwekwa ndani ya chumba akiwa hana nguo.

Bushiri alikuwa kiongozi katika jamii yake aliyoishi na mtu aliyestahika kwa hiyo kumvua nguo hadharani kulikusudiwa kumwondolea heshima yake.

Kiasi cha miaka 20 iliyopita nilifika Pangani kwa nia ya kuzuru kaburi la Abushiri, kuutembelea msikiti ulioingizwa mbwa, kuona msikiti uliong'olewa mlango wa Kizanzibari uliokuwa na aya za Qur'an ukenda kufungwa bar panapouzwa ulevi na mwisho kutafuta baadhi ya nyumba walizoishi wazee wetu tuliopokea historia zao baada ya wao kufariki yapata miaka 100 nyuma.

Hakuna aliyekuwa anajua ni msikiti upi ulioingizwa mbwa enzi za Bushiri lakini nilionyeshwa na nilisali dhuhur katika msikiti uliong'olewa mlango.

Wala sikuwa na haja ya kuuliza kwani ule mlango mpya uliowekwa ulikuwa unachusha kama vile unasema, "Ning'oeni mahali hapa."

Nilifahamishwa na kiongozi mmoja mkuu wa serikali kuwa serikali ilikuwa ipo katika mchakato wa kulitafuta kaburi la Abushiri lakini bado hawajafanikiwa.

Kiongozi huyu wa serikali alinifahamisha kuwa serikali imeamua kulitafuta kaburi la Abushiri kwa sababu watu wengi kutoka nje ya Tanzania wamekuwa wakifika Pangani kwa nia ya kuliona kaburi lake.

Nilifahamishwa kuwa si mbali na Pangani sehemu inayoitwa Mahiwa kuna sehemu Bushiri alikuwa na makazi yake hapo na sehemu hiyo anaishi Mholanzi mmoja.

Nilikwenda hadi Mahiwa na nilipokelewa na huyo Mzungu.

Huyu Muholanzi alikuwa amejenga nyumba yake ya ghorofa moja pembeni ya Mto Pangani na aliniambia kuwa yeye amesikia kutoka kwa wenyeji kuwa Bushiri alipata kuishi hapo ambapo yeye alipojenga.

Sehemu hii imejitenga sana hakuna nyumba yeyote jirani.

Huyu Mzungu hakuwa anajua lolote kuhusu Abushiri ila hili la kunyongwa na Wajerumani.

Inawezekana hapa ndani msituni ndipo Bushiri alipojenga ngome yake na kuweka kambi wakati wa vita ile dhidi ya Wajerumani.

Lakini zipo taarifa kuwa hadi miaka ya 1960 wakati mimi nikiwa mwanafunzi wa shule ya msingi na nikifundishwa historia ya "uasi," wa Abushiri dhidi ya Wajerumani watu wa Pangani walikuwa wanajua wapi alipozikwa Bushiri.

Watu walikuwa wanajua sehemu kaburi la Abushiri lilipo ingawa kaburi lenyewe lilikuwa halionekani kwa kukosa matunzo.

Alipozikwa Abushiri kwa kwa wakati ule mwaka wa 1889 hapo palikuwa pori.

Wajerumani walimzika Abushiri porini pasipokuwa na watu wala makaburi akiwa kijana wa miaka 36.

Wajerumani walimzika Bushiri msituni kutokana na chuki waliyokuwa nayo dhidi yake na kwao wao walichukulia kitendo kile sawa na kufukia kitu kinachoudhi.

Wajerumani wakati wakimzika Bushiri porini, maiti za Wajerumani askari waliouawa na askari wa Bushiri zilizikwa katika viwanja makhsusi vya makaburi kwa heshima zote.

Makaburi haya ya Wajerumani yapo Pangani hadi leo na historia ya vifo vyao inafahamika.

Ukiingia Pangani kwa mara ya kwanza utapigwa na butwaa na utajiri wa historia iliyoko bayana mbele ya macho yako.

Halikadhalika utasikitishwa na magofu ya nyumba zilozojengwa zaidi ya karne mbili zikiachiwa zibomoke hadi zitoweke.

Watu niliowakuta Pangani miaka 20 iliyopita hakuna hata mmoja aliyekuwa anajua historia ya Bushiri kwa ukamilifu wake wala kujua katika nyumba zile zilizobaki magofu Bushiri alikuwa akiishi nyumba ipi.

Lakini nilifanikiwa kuona msikiti wa Ibadh ukiwa bado umesimama katika hali yake ile ilivyokuwa wakati Bushiri katika uhai akisali.

Nilifarajika sana mwenyeji wangu kutoka Tanga aliyenisindikiza Pangani aliponionyesha gofu la nyumba iliyokuwa ya Suleiman Nasr el Lemki aliyekuwa Liwali wa Pangani wakati Bushiri na jeshi lake walipoamua kunyanyua silaha dhidi ya Wajerumani.

Taarifa ni kuwa kaburi la Bushiri bin Salim Al Harith lipo Pangani na sasa kaburi hili halipo tena porini.

Palipimwa kiwanja na mnunuzi wa kiwanja hiki amejenga nyumba yake juu ya kaburi la Abushiri.

Mengi yameandikwa kuhusu Wajerumani walioshiriki katika vita hivi lakini hakuna chochote kilichoandikwa kuhusu askari Waafrika walioletwa Pangani na Hermann von Wissman kutoka Sudan na Mozambique.

Kama Kleist Sykes asingeandika maisha yake na kueleza historia ya baba yake Sykes Mbuwane aliyepigana vita vile Bagamoyo dhidi ya Bushiri historia hii kwa upande wa Waafrika ingekuwa imepunjika pakubww.

Kutokana na kalamu ya Kleist ndipo leo tumefahamu kuwa von Wissman alipoamua kushambulia kambi ya Bushiri iliyokuwa Nzole nje ya Bagamoyo pamojanae alikuwapo Chief Mohosh (Affande Plantan), Sykes Mbuwane Chakulan na Machakaomo kwa kuwataja Wazulu wachache katika Wazulu 400 waliokuwa askari mamluki.

Wissman alishambulia kambi ya Abushiri tarehe 8 May 1889.

Haya majina ya hawa Wazulu waliopigana vita vyao vya kwanza Bagamoyo yapo katika mswada wa kitabu alioandika Kleist kabla hajafa mwaka wa 1949.

Na historia hii yote Kleist aliisikia kutoka kwenye kinywa cha mlezi wake Affande Plantan baba yao Thomas Plantan, Schneider Plantan na Mashado Plantan akaiandika kabla hajafa mwaka wa 1949.

Sishangai kwa nini wanahistoria hawampi Abushiri hapewi heshima sawa na ile anayopewa Mtwa Mkwawa na wala sistaajabu kwa nini jina lake la Abdallah halitosis katika maandishi yao kama vile yalivyokwepwa majina ya Abdulrauf Songea Mbao na Khadija Mkomanile.

Baada vita dhidi ya Bushiri na Mkwawa kumalizika Chief Mohosh sasa akijulikana kama Affande Plantan akafanywa kuwa mkuu wa Germany Constabulary katika Tanganyika.

Affande Plantan alifariki 1914 Vita Vya Kwanza Vya Dunia vikiwa tayari vimeshaanza na majeshi ya Uingereza yapo ndani ya ardhi iliyokuja kujulikana baada ya vita kama Tanganyika.

Kila ninapokwenda kumsalimu Mwalimu Maunda Plantan mjukuu wa Chief Mohosh, bint ya Mwalimu Thomas Plantan huondoka na jipya ambalo sikupata kulijua kabla.

Picha: Picha ya kitabu kinachoeleza kwa ufupi hali ilivyokuwa Bagamoyo wakati wa mapambano, gofu la nyumba ya Suleiman Nasr el Lemki na mtaa wa biashara Pangani kama ulivyokuwa mwaka wa 1910.

View attachment 1931587

View attachment 1931593

View attachment 1931604
Historia nzuri sana hii.....

Natafuta sana kujua historia ya mji wa Kilwa...nawasilisha.

Pascal Mayalla JokaKuu zitto junior
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom