Nyumba 5,600 kubomolewa Dar

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Nyumba 5,600 Dar es Salaam zipo katika mpango wa kubomolewa katika mpango wa bomoabomoa unaoendelea sasa hivi.

Mpaka sasa nyumba zilizokwisha bomolewa ni nyumba 200 ambayo ni sawa na 3% ya lengo.
 
Yawezekana watawala wetu wamefuata sheria, lakini hawakutumia busara na hekima. Nawatakia kila la kheri katika kazi yao nzuri ya kuwabomolea nyumba wananchi wao, nayo yaweza kuwa ni ubunifu.
 
chanzo ni gazeti la mwananchi, nimesahau kuweka
 
Nyumba 5,600 Dar es Salaam zipo katika mpango wa kubomolewa katika mpango wa bomoabomoa unaoendelea sasa hivi.

Mpaka sasa nyumba zilizokwisha bomolewa ni nyumba 200 ambayo ni sawa na 3% ya lengo.

Chanzo chako cha uhakika ni kipi kwa topic hii
 
Tukishamaliza kubomoa hizo nyumba tufukuze kazi wale wote waliokuwa wanaangalia tu wakati nyumbq zina jengwa hapo ndo tutakuwa tumeweka mambo sawa
 
Kwahiyo unatenda kosa,ukiona huzuiwi unaendelea?

ukitafakari kwa busara hapa, utaona hao waliokua na jukumu la kusimamia mipango miji walikua hawafanyi kazi yao au walihongwa, nyumba 5,600 kubomolewa is not good for anyone,kwa serikali inaonekana inanyanyasa na kwa wananchi ni hasara kubwa sana, hadi nyumba nyingi kiasi hiki zijengwe walikua wapi?
 
Nyumba 5,600 Dar es Salaam zipo katika mpango wa kubomolewa katika mpango wa bomoabomoa unaoendelea sasa hivi.

Mpaka sasa nyumba zilizokwisha bomolewa ni nyumba 200 ambayo ni sawa na 3% ya lengo.
Vip kwenye hiyo orodha Jumba la Mama Rwakatare wa CCM lionmo??
 
Wakimaliza kubomoa serikali watunze hayo maeneo, kama ni open space pawekwe bustani na sio kuwacha liwe pori tena.
 
1967 Mwl Nyerere alivunja Nyumba Ilala, Temeke, Magomeni na maeneo mengi nchini. Alitumia busara sana. Watawala waige busara iliyotumika miaka huyo kwa kuwezesha kila mtu anapata Nyumba walau ya kujisitiri. Serikal as Mitaa zifutwe mitaani maana mtu anauziwa eneo kwny ofisi za serikal, TRA wanakusanya mapato toka chanzo kisicho halali kwa kuwa hizi nyumba hazitambulki. Serikal itafute namna ya kuwasaidia hawa mahohe hahe walalahoi
 
Hivi Na Zile Office Za DARTS Pale Jangwani Jirani Na Kajima, Magodauni Yaliopo Bonde La Msimbazi Tokea SUKITA Ya CCM Hadi Mandera Road Na Matumbi Na Buguruni Ally Hamza!! Yatuvunjwa Au Watayaacha Tu!? Huku Wakibomoa Vibanda Vya Makabwela Tu!!!!!?? Mi Nasubiria Kuona Hilo, Hapo Ndio Nitawapongeza NEMC, JIJI Na Wakurugenzi Kwa KAZI Nzuri!! Lkn Wakiyaruka Hayo Magodauni, Magereji, Mayadi Na Maofisi!!! Sitaweza Kuikubali Hiyo Operesheni Yao!!! Nasubiria Kuona!!!
 
1967 Mwl Nyerere alivunja Nyumba Ilala, Temeke, Magomeni na maeneo mengi nchini. Alitumia busara sana. Watawala waige busara iliyotumika miaka huyo kwa kuwezesha kila mtu anapata Nyumba walau ya kujisitiri. Serikal as Mitaa zifutwe mitaani maana mtu anauziwa eneo kwny ofisi za serikal, TRA wanakusanya mapato toka chanzo kisicho halali kwa kuwa hizi nyumba hazitambulki. Serikal itafute namna ya kuwasaidia hawa mahohe hahe walalahoi

kweli mkuu, yaani hawa wanabomolewa wengine kwa kushtukizwa hata vitu unakuta hawawezi kutoa vyote
 
Mi nadhani kwa busara ya kawaida idadi ya nyuma 5,600 ni kubwa sana. Ikiwezekana wabomoe zile zilizoko kwenye maeneo hatarishi, kwenye miundombinu muhimu na viwanja vya wazi. Nyinginezo kama sio hatarishi wabadili ramani na kuzirasimisha tu. Ila usimamizi uimarishwe ili mtu asijenge nyumba bila kuwa na vibali toka mamlaka husika
 
kweli mkuu, yaani hawa wanabomolewa wengine kwa kushtukizwa hata vitu unakuta hawawezi kutoa vyote

Haitii huruma kwani ni shida yao wenyewe kwa sababu hawa wote walishapewa notice ya kuhama miaka kibao iliyopita na hela wakalipwa lakini hawakuhama kutokana na srikali ya kipindi kile kuwa bize na massage na safari za hajabu nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom