Nyuma ya Pazia; TFF -AZAM TV Haki ya Matangazo

Mk54

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
1,988
2,000
Mosi, MKATABA umetolewa kwa muktadha wa UZOEFU na sio katika TARATIBU za Manunuzi ya Umma. Mathalani, tukiangalia Ligi ya South Africa, duration ya MKATABA inakuwa ni kati ya miaka miwili hadi mitatu tu. Kila timu inapokea Bil 4 kwa mwaka huku mshindi wa PSL akipokea Bil 6 ikiwa ni jumla ya shilingi Bil 10.

Pili, Kuna viashiria vyote ya kwamba TFF na Wizara ya Habari na Michezo imeshawishika kwenye MOTIVE ya AZAM TV. CAG na TAKUKURU inashauriwa juu ya UCHUNGUZI Kuanzia Wizara ya Habari na Michezo mpaka viongozi wa TFF ili kuweza kujua COMPLIANCE na ETHICS za MKATABA kwa minajili ya Value for Money pamoja na contract duration ya miaka 10.

Tatu. Halikadhalika tafiti zinaonesha ya kwamba endapo kama kungekuwa na COMPETITION ya WAZABUNI yaani Open Tendering basi the highest BIDDER angefika kati Bil 800 hadi 1 Trilioni kwa kipindi hicho cha miaka 10.

TAKUKURU na CAG,
1. Special AUDIT kwenye mlolongo mzima wa MKATABA huu ufanyike kuanzia ngazi ya Wizara hadi TFF
2. MKATABA kati ya miaka 2 na 3 ungekuwa na TIJA katika THAMANI ya FEDHA na kuongeza ushindani kwa WAZABUNI wengine. Mkataba tajwa umekiuka VFM.

Mwisho, mada hii haina any personal issues, ni katika kutoa FURSA ya kuhoji mambo ya msingi na kuangalia mambo yetu katika jicho la tatu; There is no FREE LUNCH , NEVER!
 

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
10,951
2,000
Neema imepatikana kuanzia TFF mpaka vilabu, funika kombe mwanaharamu apite, mambo mengine ni kuyaacha tu, kuna sheria, kanuni na taratibu nyingi kwenye mambo mengi tofauti tofauti zimevunjwa kwenye hii nchi, hili la TFF na Azam isiwe ajabu bana.
 

Mk54

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
1,988
2,000
Neema imepatikana kuanzia tff mpaka vilabu,funika kombe mwanaharamu apite,mambo mengine ni kuyaacha tu,kuna sheria,kanuni na taratibu nyingi kwenye mambo mengi tofauti tofauti zimevunjwa kwenye hii nchi,hili la ftt na Azam isiwe ajabu bana.

Mkuu Badili Mtazamo wa Maisha yako.

Wewe kuwa maskini haitoi UHALALI kwa mke wako kutoka nje kwa kigezo cha kutafuta hela ya kula. Think big.

Wacha TAKUKURU ifanye kazi yake. What is Value for Money, Mjomba? How old are you? and after 10 years from now utakuwa na umri gani.

There is no such a thing Mwanaharamu apite, maneno hayo ni kuruhusu utumwa wa akili, sheria na miongozo imewekwa
Ili iwe ni Guidance kwetu ; chochote nje ya hapo ni RUSHWA
 

wakali ndondo

JF-Expert Member
Jun 12, 2017
310
500
Una miaka mingapi dogo!?? Miaka 5 nyuma hii ligi lin okiwa haielewek mdogo Angu tulikuwa tunafatilia mpira kwa redio
Azam, katusaidia sana DSTV tuliwabembeleza sana watusaidie kuonyesha ligi lakini waligoma walikuwa wanataka mechi za watani tu.

So usiwabeze Azam mdogo wangu kisa umeikuta ligi inaonyeshwa unashinda kibanda umiza jamaa wamewekeza sana ni muda wao wa kula matunda sasa.

Wanachonifurahisha azam wako tayari kukuza soka letu, watasapot timu zetu pia.
 

Mk54

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
1,988
2,000
Una miaka mingapi dogo !?? Miaka 5 nyuma hii livbi lin okiwa haielewek mdogo Angu tulikuwa tunafatilia mpira kwa redio
Azam katusaidia sana DSTV tuliwabembeleza sana watusaidie kuonyesha lig lakin waligoma walikuwa wanatakan mechi za watan tu
So usiwabeze Azam mdogo angu kisa umeikuta lig inaonyeshwa unashinda kibanda umiza jamaa wamewekeza sana ni muda wao wa kula matunda sasa
Wanachonifirahisha azam wako tayar kukuza soka letu watasapot timu zetu pia

Next time jifunze KUANDIKA vyema.

Hoja ya msingi hapa sio habari za miaka 5 iliyopita. Hoja ya msingi Bil 225 kwa miaka 10 ni akili MUFILISI katika Karne hii.

Wewe unadhani kwanini yeye ame PIN muda mrefu hivo. Kumbuka huyu ana UZOEFU na ameshaona kuna madini kiasi gani Kwenye INVESTMENT hiyo.

Je unayo taarifa kwamba kuna kampuni nyingi sana zilianza kumendea hiyo FURSA baada ya kufanya financial analysis zao . Na walikuwa tayari kuweka mara 2 ya mzigo huo tena for less that 10 years.

Wewe unadhani hiyo PIN ya 10 years ni BAHATI mbaya ? Unadhani AZAM anashindwa kutoa 2 Bil kwa Wizara husika na TFF kuharakisha hiyo dili.

Je unajua sheria ya Restricted Tendering ? Je unajua kipengele chochote ndani ya mkataba huo. Unaimbishwa nyimbo ya hovyo na wewe unacheza.

Tafadhali, open your eyes and learn how to be skeptic.
 

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
10,951
2,000
Mkuu Badili Mtazamo wa Maisha yako.

Wewe kuwa maskini haitoi UHALALI kwa mke wako kutokana nje kwa kigezo cha kutafuta hela ya kula. Think big.

Wacha TAKUKURU ifanye kazi yake. Do you know what is Value for Money , Mjomba? How old are you ? and after 10 years from now utakuwa na umri gani.

There is no such a thing Mwanaharamu apite, maneno hayo ni kuruhusu utumwa wa akili, sheria na miongozo imewekwa
Ili iwe ni Guidance kwetu ; chochote nje ya hapo ni RUSHWA
Kwa hili wala sibadili mtazamo wangu, Azam Mungu awabariki kwa kutupatia huduma bora, baada ya miaka mitano waongeze tena mkataba juu ya mkataba kabla ya mkataba huu wa juzi haujaisha.

Viva Azam, Viva TFF.
 

Megalodon

Senior Member
Apr 9, 2021
186
500
Mosi , Napinga HOJA ya kwamba AZAM TV imekuza soka letu na kuboresha ubora VPL.
Ukweli ni kwamba VPL na SOKA letu limekuwa kulingana na NYAKATI kama ilivyo katika Muziki kwa sasa.

Pili, katika MKATABA huo, hakuna dalili yoyote ya kwamba TARATIBU za manunuzi ya Umma zilifuatwa ikiwa ni pamoja na kuwashindanisha WAZABUNI . MKATABA umetolewa kwa muktadha wa UZOEFU na sio katika TARATIBU za Manunuzi ya Umma.
View attachment 1801626

Mathalani, tukiangalia Ligi ya South Africa, WAZABUNI hushindanishwa PUBLICLY na kumpata COMPETITIVE BIDDER mwenye thamani kubwa. Aidha, MKATABA unakuwa ni kati ya miaka miwili hadi mitatu tu. Kila timu inapokea Bil 4 kwa mwaka huku mshindi wa PSL akipokea Bil 6 ikiwa ni jumla ya shilingi Bil 10.

Tatu, Kuna viashiria vyote ya kwamba TFF na Wizara ya Habari na Michezo imeshawishika kwa namna moja au nyingine kwenye MOTIVE ya AZAM TV. Hivyo basi, CAG na TAKUKURU hii ni KAZI yenu . Kuanzia Wizara ya Habari na Michezo mpaka viongozi wa TFF WACHUNGUZWE kwa kusaini MKATABA wenye thamani ya Bil 225 tu kwa miaka 10 mfululizo huku other factors are not constant. Tafiti zinaonesha ya kwamba hakuna TV sponsor katika MATAIFA mengine imepewa haki ya matangazo kwa miaka 10 mfululizo bila ya KUSHINDANISHWA na WAZABUNI wengine. Je, hawa wenzetu wameyatoa wapi kwa mantiki ya Value for Money( VFM).

Nne. Halikadhalika tafiti zinaonesha ya kwamba endapo kama kungekuwa na COMPETITION ya WAZABUNI yaani Open Tendering basi the highest BIDDER angefika kati Bil 800 hadi 1 Trilioni kwa kipindi hicho cha miaka 10.

TAKUKURU na CAG,
1. Special AUDIT kwenye mlolongo mzima wa MKATABA huu ufanyike kuanzia ngazi ya Wizara hadi TFF
2. Muda wa miaka 10 bila ya kushindanisha wazabuni wengine, ni ANGAMIZO na MANUFAA ya watu wachache; MKATABA kati ya miaka 2 na 3 ungekuwa na TIJA katika THAMANI ya FEDHA na kuongeza ushindani katika other interested bidders in the near future.
3. Je Financial Intelligence kubaini MAKUSANYO ya AZAM katika haki ya matangazo kwa mwaka unaoishia inasemaje?

CAG na TAKUKURU fanyeni kazi yenu kudadavua huo UKAKASI.... kuna KAHARUFU kuanzia WIZARA husika hadi TFF.
Mwisho, mada hii haina any personal issues, ni katika kutoa FURSA ya kuhoji mambo ya msingi na kuangalia mambo yetu katika jicho la tatu; There is no FREE LUNCH , NEVER!

Waze wa sistimu mshaanza kuchokonoa.
Mwenda zake mwenda zake. Watu walibanwa sana
 

Megalodon

Senior Member
Apr 9, 2021
186
500
Una miaka mingapi dogo !?? Miaka 5 nyuma hii livbi lin okiwa haielewek mdogo Angu tulikuwa tunafatilia mpira kwa redio
Azam katusaidia sana DSTV tuliwabembeleza sana watusaidie kuonyesha lig lakin waligoma walikuwa wanatakan mechi za watan tu
So usiwabeze Azam mdogo angu kisa umeikuta lig inaonyeshwa unashinda kibanda umiza jamaa wamewekeza sana ni muda wao wa kula matunda sasa
Wanachonifirahisha azam wako tayar kukuza soka letu watasapot timu zetu pia

Biashara za inshallah inshallah
 

Bukali

JF-Expert Member
May 7, 2018
854
1,000
Una miaka mingapi dogo !?? Miaka 5 nyuma hii livbi lin okiwa haielewek mdogo Angu tulikuwa tunafatilia mpira kwa redio
Azam katusaidia sana DSTV tuliwabembeleza sana watusaidie kuonyesha lig lakin waligoma walikuwa wanatakan mechi za watan tu
So usiwabeze Azam mdogo angu kisa umeikuta lig inaonyeshwa unashinda kibanda umiza jamaa wamewekeza sana ni muda wao wa kula matunda sasa
Wanachonifirahisha azam wako tayar kukuza soka letu watasapot timu zetu pia
Hapana hatuwezi enda hivihivi, eti ligi ilikuwa haijulikani.
Sasa ishajulikana si kwamba Azam hajafaidika, kapata faida ndio maana kaja kijanja na miaka 10.
 

mtanzania1989

JF-Expert Member
May 20, 2010
3,819
2,000
Hela aliyotoa Azam Media si DSTV wala media yoyote ingeweze kutoa kwa soka la bongo. DSTV Kenya walikuwa wanatoa 7bn Tsh kwa mwaka, wakati Azam wamekubali kutoa 22bn Tsh kwa mwaka kwa Tanzania, pili bei za vifurushu vya DSTV si rafiki kwa uchumi wa watanzania wengi, wakati Azam 20k tu unaona VPL kama yote.
 

Katomlb

Member
Apr 9, 2021
37
125
Akili ndogo kama zako ndo huwa wanajadili matukio na hawawezi kamwe kusababisha matukio. Azam kaweka pesa yake unaona nongwa eti? Wapuuzi kama wewe washawahi mchefua vodacom najua klabu zilikiona cha moto. Unadhani azam asingeliweka pesa ni nani angeliweka au ndo ungekuja na uzi wa kuponda TFF tena kwa kufukuza wawekezaji?

Nina imani kupitia hiki walichokifanya azam huenda ligi ikaongeza ushindani kwa bonas zile sio kila upuuzi uuoneshe kwa watu au ndo unatufuta kazi ya uchambuzi ndugu?
 

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,225
2,000
Pili, katika MKATABA huo, hakuna dalili yoyote ya kwamba TARATIBU za manunuzi ya Umma zilifuatwa ikiwa ni pamoja na kuwashindanisha WAZABUNI . MKATABA umetolewa kwa muktadha wa UZOEFU na sio katika TARATIBU za Manunuzi ya Umma.
Boss vyema kama hujui ukauliza...tenda ilikuwa wazi na wazabuni waliojitokeza kuomba ni pamoja na TBC 1 kupitia Startimes, Startv kupitia continental decoda na ATN kupitia TING ...so you see..watu waliojitokeza kuweka mzigo mezani..hoja za Azam TV zikwap shawishi zaidi kuliko hao wengine...

Na kingine watu mnalia Sana na DSTV Ila kiukweli DSTV asingeweza kutoa pesa hata robo ya aliyotoa Azam TV.. zingatia alichotoa kwenye ligi za Zambia na Ethiopia ambapo huko ana soko kubwa pia Kama hapa TZ.

Utasema mbona Katoa mzigo mkubwa Afrika kusini, jibu ni simple tu kule Afrika kusini DStv ni kama Azam TV kwa hapa bongo..wana wateja wengi na uhakika mkubwa wa return ..the same na Azam TV hapa ..ingekuwa Azam TV anadhamini ligi ya Kenya asingetia pesa nyingi hivi..simple kwa kuwa hana return kule.

Ukijumlisha dau ambalo angetoa washindaji wote hao.. kwa miaka kumi ijayo..isingeweza kufika dau aliloweka Azam TV..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom