Django
JF-Expert Member
- Apr 15, 2013
- 354
- 147
KATIKA taifa letu leo hii kuna mgawanyiko mkubwa ambao unaweza kuwekwa kwenye makundi makubwa matatu.
Kuna kundi la wale ambao wako pembezoni mwa mafanikio lakini wakiwa ndio wenye kuhenyeka kila kukicha kujenga nchi lakini wakivuna mabua na upande mwingine wapo wale ambao kazi yao ni kula wasichopika na kuvuna wasichopanda.
Kundi la tatu lipo la wale ambao wanajiona hawana upande (neutral) na ambao wanaangalia ni upande gani unaonekana kufanikiwa ndio wajiunge nao.
Yawezekana kundi hili la watu ambao wanasema hawana upande ni wengi zaidi. Na inawezekana ndilo kundi la hatari zaidi kwani ndilo linachelewesha mabadiliko nchini.
Makundi yale mawili makubwa ndio yanagombania urithi wa taifa letu. Kikundi kidogo cha wenye nguvu ndicho kimeshikilia njia zote za kuufikia urithi huo na ndiyo hawa wenye nguvu ya kuchukua chochote, kutoka kwa mtu yeyote, wakati wowote bila kujali lolote! Kundi hili lina nguvu ya kisiasa na nguvu ya kiutawala. Ni kundi ambalo halijali chochote. Kuna msemo katika Kiingereza kuwa Abarger care about nothing! Yaani Kingo hajali lolote! Kingo kwa asili ni mnyama ambaye anaweza kula chochote akiwa na njaa. Japo chakula chake kikubwa ni asali, kingo hata hivyo haishii kwenye asali tu; ana kula chochote na anaweza kumnyanganya yeyote ili ale.
Kwa vile ni mnyama anayetumia nguvu nyingi sana, kingo basi muda wote ni mnyama mwenye njaa; atakula nyoka kama atakavyo kula ndege, na anaweza kumnyanganya simba chakula ikibidi!
Nyoka wenye sumu wamejaribu kuwagonga kingo na kingo wakazimia kwa muda lakini baadaye wanaamka na kuendelea kutafuta kula.
Kiboko ya Kingo ni nyuki waliodhamiria; ni wadudu wanaofanya kazi mno labda kuliko wadudu wengine wote kutengeneza mojawapo ya vitu vitamu kabisa duniani! Nyuki ni wadudu wenye nidhamu ambao wana utawala wao chini ya malkia wao.
Hata hivyo, nyuki mara nyingi wanajikuta wanatishiwa na uwepo wa kingo hasa kingo ambao wamedhamiria kupata asali.
Itakuwaje kama nyuki nao wanadhamiria kuzuia asali isitoke?
Makala yangu ya leo iko katika mtindo wa sheria; ni matumaini yangu utalifurahia na ndani yake utajikuta wewe mwenyewe unachagua upande katika mtanange huu wa demokrasia ambao mwisho wake bado haujawa dhahiri.
Nyuki wamechachamaa
Nyuki wamechachamaa, nyuki wameshacharuka,
Hasira kama kichaa, kichwani zimewashika,
Hawana cha msamaha, zamu yao imefika,
Nyuki wamechachamaa, kingo wamekasirika!
Hawa nyuki wa asali, nyuki wanaosifika,
Wanauliza maswali, yapo yasotamkika,
Si moja au mawili, ni mengi ya uhakika,

Asali twatengeneza, mbona bado maskini,
Na ngambo tunaiuza, inauzwa hata ndani,
Kingo ndio wapendeza, sisi tumekosa nini?
Nyuki wamechachamaa, Kingo wamekasirika!
Asali yetu ni bora, mfano wake hakuna,
Mtwara hadi Tabora, mizinga imejazana,
Kingo wanavyotupora, wanetu kula hakuna,

Wageni wanatujia, kuja kurina asali,
Wanakuja kwa mamia, toka masafa ya mbali,
Kingo wanatuambia, niwawekezaji mahili,

Mikataba waingia, kingo wanashangilia,
Mizinga wanagawina, nyuki tunaangalia,
Miaka inakimbia, mizinga yakaukia,

Mzinga ukiishia, mwingine wanahamia,
Wenyewe tunajifia, huku tunajililia,
Twafa tunaangalia, wapi tutakimbilia,
Nyuki wamechachamaa, Kingo wamekasirika
Kingo walishazoea, kula asali kwa zamu,
Hakuna wa kufokea, wanajilia kwa hamu,
Mabingwa wa kubobea, wamegeuka walimu,

Wanakula na masega, masega yenye asali!
Mizinga toka Nzega, kwa sahani na bakuli,
Wana kula na kumwaga, nyuki tunalikubali?
Nyuki Wamechachamaa, Kingo wamekasirika!
Sasa nyuki kimewaka, kingo wanataharuki!
Wamezindukazinduka, lahaullah hawa nyuki!
Kingo wanatetemeka, wamezidiwa mikiki!

Wanaleta na polisi, kupiga mkwara nyuki,
Nyuki wanazidi kasi, wala hawababaiki,
Wanapigwa na risasi, nyuki chini haanguki,

Toka Arusha na Mtwara, Tanga hadi Newala,
Na nyuki toka Tabora, wa Iringa, na Ukala
Utadhani Tora Bora, Kingo wanashindwa kula!

Nyuki wametuma neno, asali haitoki tena,
Haitoki kwa maneno, au vitisho vya jana,
Kingo wakosa unono, wageni waulizana,

Tushikamane nyuki, asali hiyo ni yetu,
Ya kwenu tena ya haki, yenu na ya wanetu!
Kingo wakae na nyuki, asali itufae petu!

Ninalo neno kwa kingo, kingo walamba asali,
Mmetawala kwa uongo, mkikimbia maswali,
Ahadi za mlolongo, mkipindisha kauli!

Kukasirika kwa kingo, hakuwasumbui nyuki!
Hata waje na magongo, huyu nyuki hatishiki,
Umeporomoka wongo, umekoma uzandiki!

Nyuki wameshaamka, kulala tena hakuna,
Na lindo wamelishika, hawatoachia tena,
Zamu yenu kugeuka, kingo ngondo mwaona,
Nyuki wamechachamaa, kingo wamekasirika
Beti zangu zinakoma, ninafunga kwa nukta,
Mwakijiji natuwama, heshima zangu wapata,
Nyuki wameshasimama, hawa kingo watajuta!