Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,174
Yapo makundi mawili ndani ya Chadema kundi moja laongozwa na Tundu Lissu na la pili liko chini ya Aikael Mbowe.
Ugomvi wa haya makundi mawili ni nani awe mpeperusha bendera ya Urais ujao yaani 2025.
Kundi la Tundu Lissu linaamini mgombea wao ndiye mwenye mvuto na wanaamini alishinda uchaguzi wa 2020 wakati kundi la Mbowe lina mtazamo tofauti na huo wao wanaona ni zamu ya Mwenyekiti wa chama apewe fursa stahiki kama Mwenyekiti wa chama.
Katika hiyo mivutano, kundi la Tundu Lissu limekuwa likibeza jitihada ya Mwenyekiti wao kufikia mwafaka na CCM kwa kudai CCM hawana dhamira ya kweli ya kuwatendea haki wapigakura wa nchi hii.
Pia, Tundu Lissu na kundi lake hawana imani na wajumbe wa hiyo kamati ya mwafaka wakihoji walivyopatikana na wana mwakilisha nani.
Mbowe na wenzake ambao wengi wao ni wachaga wanaona mwafaka na CCM utasaidia kuleta katiba mpya ambayo inabeba matarajio ya wengi ya kufanyika uchaguzi wa huru na haki ukisimamiwa na Tume huru.
Ni dhahiri kwa sasa wamepata gundi ya kufukia hizi tofauti lakini swala tata la bandari haliwezi kuendelea bila ukomo. Tunatarajia mwafaka wa utata na kizungumkuti wa bandari umiliki, uendeshaji wake na mgawanyo wa mapato utapata ufumbuzi kabla ya mwisho wa mwakani na baada ya hapo Chadema itabidi ivalie njuga migawanyiko tajwa kwenye chama chao.