Nyota zenu HAZIFANANI

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,030
156,526
Hebu fikiria, umekaa na msichana wako kwa zaidi ya miaka saba, tangu mkiwa shule hadi mnamaliza chuo, mnafunga pingu za maisha na kubahatika kupata watoto wawili.
Mkeo ana umbo zuri, licha ya kuwa ni mzazi wa watoto wawili lakini anaonekana kama bado hajawahi kuzaa.
Muda unaenda, tabia zake nyumbani zinaanza kubadilika, unafanya uchunguzi, unagundua kuwa anatembea na meneja wa mradi fulani unaodhaminiwa na wahisani kwa mamilioni ya dola za kimarekani.
unaendelea na uchunguzi lakini huoati uthibitisho wa mapenzi yao.
siku moja jioni, mkeo anakuja anakuambia kuwa amegundua kuwa nyota zenu haziendani ndio maana hata mama yake (ambaye ni mama mkwe wako) alikufa kwa kansa, halafu kwa sababu nyota zenu haziendani ndio maana hata ng'ombe wenu kule shambani alikufa baada ya kumeza mfuko wa nailoni, hivyo basi anaomba muachane kwani utamletea mabalaa mengine makubwa.
Je ukiwa kama wewe utafanyeje? kisa hiki kimemkumba mfanyakazi mwenzetu na leo ameshindwa kabisa kufanya kazi.
Naomba majibu yenu ya hekima niyatumie kama dawa ya kumliwaza na kumtia moyo ndugu yetu huyu
 
nyota aziendan ndo mana mamake akafa kwa kansa?ndo mana ng'ombe alikufa kwa kumeza nilon shambaban....kwa iyo tuachane?
ahh apo kakangu HAUITAJI KUTIA NENO CZ KUONGEA UJINGA /UPUMBAVU NA WEWE UTAKUWA MJINGA /MPUMBAVU ( as long as unajua anachoongea ni ujinga ,upuuzi wa mwsho cz kansa sjui ng'ombe kufa haiwez kusababishwa na nyota )

amwambie mkewake unatakaje?atasema tuachanae amwambie poa waachane...(najua haitakuwa kuachana cz wthn miez miwil uyo mdada atarudi na kuomba msamaha..

uyo dada ni limbukeni na kuna kitu kinamsumbua kutokana na uyo mwanaume mwenye pesa na akishaachana na mmewe uyo mwizi pia atasepa na uyo dada akili itamrudi...

kaka hana kosa ni uelewa mdg na ujinga wa dada ndo tatizo
atarudi mwenyewe ni wehu tu na macho juu ndo pbm...

ni wimbi tu litapita bt asimkataze kufanya ananchotaka kufanya ili aelewe somo vzr (iwe practical zaid)
 
ngoja nicheke kwanza yaarab yaani ng'ombe kameza lailoni ni kwa ajili nyota haziendani,,,,he,,,kaazi kweli kweli,,,, i will b back men,,,
 
Hii kali kwa kweli, heri kujikwaa kidole kuliko kujikwaa akili.
Huyo binti amerogwa bila ya shaka.
sipati picha, mtu una watoto wawili halafu unataka kuivunja ndoa yako, wewe ni mwehu au punguani?
 
hapo mbona mambo yako wazi.yani hata kama hujui kusoma lazima picha utazielewa.hapo huyo bibie hana time tena na mume wake.tena akilazimisha kuendelea kuishi nae atajikuta anaishi maisha magumu ya majonzi kuliko!!hapo apige chini mzigo tu na tena ajifanye hata hamjui.kwa kumsaidie mtafutie tu king'amuzi cha kumliwaza.
 
kweli huyo dada amechemka...

Lakini atakapoachana na mume wake, ajue kuwa hata huyo meneja atampiga kibuti.... kwa sababu na yeye inawezekana ana mke na hawezi kukubali mzigo mwingine....

Mpe nafasi, kampumzishe kwao kwa muda usiojulikana, kama atarudi kwa huyo bwana utajua... lakini mwisho wa siku, atarudi kukuangukia na kuomba msamaha kwa madai kuwa shetani alimpitia...
 
nyota aziendan ndo mana mamake akafa kwa kansa?ndo mana ng'ombe alikufa kwa kumeza nilon shambaban....kwa iyo tuachane?
ahh apo kakangu HAUITAJI KUTIA NENO CZ KUONGEA UJINGA /UPUMBAVU NA WEWE UTAKUWA MJINGA /MPUMBAVU ( as long as unajua anachoongea ni ujinga ,upuuzi wa mwsho cz kansa sjui ng'ombe kufa haiwez kusababishwa na nyota )

amwambie mkewake unatakaje?atasema tuachanae amwambie poa waachane...(najua haitakuwa kuachana cz wthn miez miwil uyo mdada atarudi na kuomba msamaha..

uyo dada ni limbukeni na kuna kitu kinamsumbua kutokana na uyo mwanaume mwenye pesa na akishaachana na mmewe uyo mwizi pia atasepa na uyo dada akili itamrudi...

kaka hana kosa ni uelewa mdg na ujinga wa dada ndo tatizo
atarudi mwenyewe ni wehu tu na macho juu ndo pbm...

ni wimbi tu litapita bt asimkataze kufanya ananchotaka kufanya ili aelewe somo vzr (iwe practical zaid)

jamani watu wana dharau mbaya mwe!! hivi mtu umezaa nae watoto wawili unamwambia hivyo kweli lol nashindwa hata cha kuchangia
 
funga kwa maombi
ni mawimb kwenye maisha ya ndoa..

Ni kweli kabisa unachosema Rose, maana hii inashangaza nyota haziendani kwa vile mama mkwe kafariki kwa cancer!! ng'ombe naye duh! huyu anatafuta visingizio vya kuachika. Ikiwezekana muache tu kwani kuna usemi kuwa 'U will never know the value / importance of something / someone until u loss it / him/her hakika atakurudia kwa msaaha baadae baada ya kurealize her mistake. Unakumbuka lile song la Dube babe??. anyway lile gauni lako la mauamaua lipo tayari na zile sandals! so kaa mkao wa kutembea kandokando ya mto jioni ya Christmass!!
 
huyo dada atakuwa ameshajiingiza kwenye masuala ya nguvu za giza ( yaani anakwenda kwa waganga wa kienyeji) nasikia ndo wenye kutoa ushauri wa mambo ya Nyota ambayo ni uzushi mtupu!!!!!
Ushauri wangu ni kwamba kama mwanamke keshasema tuachane, jamaa asitake kulazimisha maana siku zote raha ya ndoa huletwa na upendo wa kweli.....najua jamaa ataumia sana but apige moyo konde asikilize maamuzi ya mkewe ambaye nina uhakika atasema muachane!
 
Maisha yenyewe mafupi....Open the door and give her a goodbye kiss as simple as that!
 
hatari tupu ...
huyu dada kashanusa $$$$$$$$$ halafu anasigizia nyota..
nyota gani kwanza hizo anaongelea zile za kwenye magazine ni unafki mtupu...

namwonea huruma sana huyo kaka na watoto wake.....
kwa kweli saa nyingine $$$ ni ibilisi mkubwa sana.....

kwa kweli huyu kaka anatakiwa awaze nini cha kufanya na wanawe ka mama
ndo ameanza kuongea nmna hiyo....
 
wanawake wengine huwa wana confidence za ajabu cjui wanatoa wapi..
Huyu si bure kuna linalomsumbua baada ya muda atajuitia matendo yake machafu
 
Kama kweli yeye ni mtaalam au anaamini nyota, kwa nini nyota hakuzitumia ili kujua kama yule ni mwanamme anayeweza kuishi nae kabla ya ndoa? Kwa nini nyota zije baada ya kuona mda mrefu? Kanogewa tu huyo inje, na akiachika tu huku, tha same na upande wa pili (ziliko kubali nyota), na hapo ndipo majuto anapokuwa mjukuu.
 
hatari tupu ...
huyu dada kashanusa $$$$$$$$$ halafu anasigizia nyota..
nyota gani kwanza hizo anaongelea zile za kwenye magazine ni unafki mtupu...

namwonea huruma sana huyo kaka na watoto wake.....
kwa kweli saa nyingine $$$ ni ibilisi mkubwa sana.....

kwa kweli huyu kaka anatakiwa awaze nini cha kufanya na wanawe ka mama
ndo ameanza kuongea nmna hiyo....

nadhani ana undugu na shekhe Yahya
 
nadhani ana undugu na shekhe Yahya

Hapo umenena vyema, huyu mzee anachangia sana kuharibu mahusiano na ndoa za watu. Hebu tuishi kama zamani mbona ndoa zilidumu sana tu bila nyota. Skafu nazo eti zinahusika katika mapenzi kweli?
 
Back
Top Bottom