Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,834
- 155,782
Hebu fikiria, umekaa na msichana wako kwa zaidi ya miaka saba, tangu mkiwa shule hadi mnamaliza chuo, mnafunga pingu za maisha na kubahatika kupata watoto wawili.
Mkeo ana umbo zuri, licha ya kuwa ni mzazi wa watoto wawili lakini anaonekana kama bado hajawahi kuzaa.
Muda unaenda, tabia zake nyumbani zinaanza kubadilika, unafanya uchunguzi, unagundua kuwa anatembea na meneja wa mradi fulani unaodhaminiwa na wahisani kwa mamilioni ya dola za kimarekani.
unaendelea na uchunguzi lakini huoati uthibitisho wa mapenzi yao.
siku moja jioni, mkeo anakuja anakuambia kuwa amegundua kuwa nyota zenu haziendani ndio maana hata mama yake (ambaye ni mama mkwe wako) alikufa kwa kansa, halafu kwa sababu nyota zenu haziendani ndio maana hata ng'ombe wenu kule shambani alikufa baada ya kumeza mfuko wa nailoni, hivyo basi anaomba muachane kwani utamletea mabalaa mengine makubwa.
Je ukiwa kama wewe utafanyeje? kisa hiki kimemkumba mfanyakazi mwenzetu na leo ameshindwa kabisa kufanya kazi.
Naomba majibu yenu ya hekima niyatumie kama dawa ya kumliwaza na kumtia moyo ndugu yetu huyu