Nyota za bahati zipoje?

Nyota za bahati zipoje?

uajekundu

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2016
Posts
541
Reaction score
461
Habari wana Jamvi,

Naombeni msaada kwa wale wanaojua mambo ya nyota.

Nina rafiki yangu ameanza kusali kanisa fulani maarufu hapa mjini, alipoenda kanisani mchungaji akamuombea akamwambia kuna ndugu zake wamechukua nyota yake na kuiuza kampuni ya Toyota Japani.

Yani amechanganyikiwa anahisi toyota wanauza magari kwa nyota yake. Eti hii uongo kitu inawezekana kweli? Mi naona kama ni uongo fulani wa kumfanya aende kanisa hilo daily je inawezekana kwa nyota ya mtu kuuzwa?

Tena kwa kampuni kubwa ivo kutoka kwa mtanzania wa kawaida hajulikani hata mtaani kwao? Mnaojua habari za nyota tafadhali nisaidieni kulifumbua hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi thimgs znaukweli.. Kiiman zaidi zipo

Carpe diem.....
Ni mambo ya kiroho nyota ya mtu inaweza kuchafuliwa au kuchukuliwa na kutumiwa kwa faida ya mtu mwingine na mhanga mambo yake yakawa yanakwama sana lakini hilo la kuuziwa Toyota halijakaa vizuri nadhani si kweli ni kumtisha tu ili waendelee kula sadaka zake
 
Habari wana Jamvi, naombeni msaada kwa wale wanaojua mambo ya nyota.
Nna rafiki yangu ameanza kusali kanisa fulani maarufu hapa mjini, alipoenda kanisani mchungaji akamuombea akamwambia kuna ndugu zake wamechukua nyota yake na kuiuza Kampuni ya TOYOTA Japani. Yani amechanganyikiwa anahisi toyota wanauza magari kwa nyota yake. Eti hiii uongo f kitu inawezekana kweli? Mi naona kama ni uongo fulani wa kumfanya aende kanisa hilo daily....je inawezekana kwa nyota ya mtu kuuzwa? Tena kwa kampuni kubwa ivo kutoka kwa mtanzania wa kawaida hajulikani hata mtaani kwao?
Mnaojua habari za nyota tafadhali nisaidieni kulifumbua hil.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizi hesabu ngumu sana aisee,
Kwa hiyo kama Toyota wasingechukua Nyota ya Jamaa basi angekua tajiri kama walivyo Toyota sasa??
 
Ni mambo ya kiroho nyota ya mtu inaweza kuchafuliwa au kuchukuliwa na kutumiwa kwa faida ya mtu mwingine na mhanga mambo yake yakawa yanakwama sana lakini hilo la kuuziwa Toyota halijakaa vizuri nadhani si kweli ni kumtisha tu ili waendelee kula sadaka zake

Eti Toyota mkuu kweli
 
aaaaah amwambie awaunganishe nao ili awauzie mwezi na mbalamwezi kama wanazihitaji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom