Nyota za bahati zipoje?

Nyota za bahati zipoje?

Habari wana Jamvi, naombeni msaada kwa wale wanaojua mambo ya nyota.
Nna rafiki yangu ameanza kusali kanisa fulani maarufu hapa mjini, alipoenda kanisani mchungaji akamuombea akamwambia kuna ndugu zake wamechukua nyota yake na kuiuza Kampuni ya TOYOTA Japani. Yani amechanganyikiwa anahisi toyota wanauza magari kwa nyota yake. Eti hiii uongo f kitu inawezekana kweli? Mi naona kama ni uongo fulani wa kumfanya aende kanisa hilo daily....je inawezekana kwa nyota ya mtu kuuzwa? Tena kwa kampuni kubwa ivo kutoka kwa mtanzania wa kawaida hajulikani hata mtaani kwao?
Mnaojua habari za nyota tafadhali nisaidieni kulifumbua hil.

Sent using Jamii Forums mobile app
Akili za kuambiwa changanya na zako
 
Kwani kampuni ya toyota na huyo aliyeibiwa nyota kipi kilianza?

Huyo aliyeibiwa nyota yake ana umri mkubwa kuizidi kampuni ya toyota?

Mauzo ya toyota kabla ya kuuziwa hiyo nyota yalikuwaje na sasa yakoje?
 
Habari wana Jamvi,

Naombeni msaada kwa wale wanaojua mambo ya nyota.

Nina rafiki yangu ameanza kusali kanisa fulani maarufu hapa mjini, alipoenda kanisani mchungaji akamuombea akamwambia kuna ndugu zake wamechukua nyota yake na kuiuza kampuni ya Toyota Japani.

Yani amechanganyikiwa anahisi toyota wanauza magari kwa nyota yake. Eti hii uongo kitu inawezekana kweli? Mi naona kama ni uongo fulani wa kumfanya aende kanisa hilo daily je inawezekana kwa nyota ya mtu kuuzwa?

Tena kwa kampuni kubwa ivo kutoka kwa mtanzania wa kawaida hajulikani hata mtaani kwao? Mnaojua habari za nyota tafadhali nisaidieni kulifumbua hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungemwambia akamkate vibao huyo mchungaji, haiwezekani amfanyie utoto wa namna hiyo!

Kesho atamwambia apeleke kiasi fulani cha pesa ampe maji ya kurudisha nyota!
 
Kuhama hama makanisa mtasali mpk Kwenye nyumba za ibada za mashetani, si mtuliege hamkomi. Bora niende kwa mganga sio makanisa haya ya wasakatonge
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom