Nyota wa filamu Bollywood aachiwa

explicity

JF-Expert Member
Oct 9, 2015
207
140
Nyota wa filamu za Bollywood Sanjay Dutt amewachiliwa kutoka jela katika mji wa magharibi wa Pune nchini India.

Dutt mwenye umri wa miaka 56 alihukumiwa kifungo jela kufuatia makosa ya kumiliki silaha inayohusishwa na mlipuko wa 1993 mjini Mumbai ambapo takriban watu 257 waliuawa na wengine 713 kujeruhiwa.

Alipatikana na hatia ya kununua silaha hiyo kutoka kwa walipuaji ,lakini akasema kwamba silaha hizo zilikuwa muhimu kwa lengo la kuilinda familia yake wakati wa ghasia za Waislamu dhidi ya Hindu.

Nyota huyo baadaye alipelekwa hadi katika jela ya Pune mwaka 2013 ili kukamilisha kipindi chake cha miaka mitano.

Hatahivyo alipewa msahama wa siku 144 baada ya kuonekana kuwa na tabia njema na vitendo kama vile kusimamia kipindi cha redio.
 
Huyu na Salman Khan wakorofi sana!!!

Wangeiga mfano wa mwenzao Sharukh Khan, ana pesa sana lakini hana makuu & ni balozi mzuri wa UN kupitia mashirika kama UNICEF.

Ninampenda sana Sharukh Khan, hana makuu na mtu na ni mtoaji. Nakumbuka Ra.One ilipofanikiwa aliwanunulia team members wake Bmw Series 7 Sedan cars za maana. Ni halali kwake kuwa anaingiza mapene akikimbizana na akina Tom Cruise.
Salman Khan kama sio rushwa angekua anakula kifungo cha maisha mpaka sasa.
 
huyo kiboko yaan akiigiza na Yale macho yake akilia ,nyimbo zake balaa hakunagaa
 
Mna picha zao labda........?.....
2145b6815f4528ddf7a8d9acdd4fc84a.jpg
sanjay datt
 
Back
Top Bottom