Nyongeza ya mshahara ya mwaka

Nyongeza ya mshahara ya mwaka

kson m

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
6,682
Reaction score
3,066
Kwenye mikataba ya ajira suala la nyongeza ya mishahara kwa mwaka lipo wazi kabisa.

Mtumishi anatakiwa kubadilika toka kiwango kimoja kwenda kingine kila mwaka.

Mfano toka tgts c1 kwenda tgts c2 mwaka unaofuata.

Siku hizi jambo hili halifanyiki na matokeo yake hakuna tofauti ya mshahara kati ya mtumishi aliyeanza kazi mwaka juzi na aliyeanza leo.

Nini sababu za kuondoa hizo increaments? Katika mikataba imeelezwa kuwa mtumishi atanyimwa increament endapo amefanya makosa?

Je tunaonyimwa tumefanya makosa yapi?

Wadau naombeni ufafanuzi.
 
Kweli mkuu!,yaani kuna jamaa alinikuta kazini mimi nikiwa nimemtangulia miaka miwili lkn cha ajabu mpaka sasa tunalipwa sawa,sijui ni kwanini??.
 
Mbaya zaidi ndugu zangu hata madaraja kulingana na mikataba hiyo ni kwamba mtumishi atapanda daraja kila baada ya miaka mitatu.jambo hili nalo halifanyiki.zaidi sana mtu akikumbukwa hupandishwa baada ya miaka minne au mitano na zaidi.huu ni wizi na unyanyasaji pia.vyama vya wafanyakazi vinakata mishahara yetu kila leo lakini hatuoni wakifanya chochote kuhusu haya manyanyaso.wfanyakazi tufanyeje sasa?
 
kweli kabisa,MTU aliyeanza kazi 2011analipwa saw a na aliyeanza kazi 2015.hii ni aibu
 
increment huwa haipandi kama kutatokea mabadiliko ya mshahara (ongezeko la mshahara).. na toka 2010 kila incremental year kumekuwa na maboresho ya nyongeza ya mshahara... so hauwezi kupanda increment..
isipokuwa ikitimia miaka mitatu ya utumishi kazini hata kama bado uko mfano c1 utaruka hadi daraja d1.. hapo ndipo utakapompita huyo unayeona kaajiriwa juzi na mko sawa
...
isingetokea ongezeko/badiliko la mshahara mfano mwezi wa 7 mwakani lisipokuwepo hapo utapanda hichi kidaraja kidogo c1-c2 ...
 
Mbaya zaidi ndugu zangu hata madaraja kulingana na mikataba hiyo ni kwamba mtumishi atapanda daraja kila baada ya miaka mitatu.jambo hili nalo halifanyiki.zaidi sana mtu akikumbukwa hupandishwa baada ya miaka minne au mitano na zaidi.huu ni wizi na unyanyasaji pia.vyama vya wafanyakazi vinakata mishahara yetu kila leo lakini hatuoni wakifanya chochote kuhusu haya manyanyaso.wfanyakazi tufanyeje sasa?

Jambo la msingi ni kuhamasishana watumishi wa serikali wa kada zinazoitwa za chini! hasa walimu kuchukua maamuzi magumu ya kuhakikisha mfumo uliozeeka na kuchoka unabadilishwa kwa kuupigia kura mwaka huu. Ni ukweli mtupu kwa upande wa walimu walionza kazi mwaka 2011 na wale wa 2008 walitakiwa wapande madaraja tangu mwaka jana ambapo wale wa 2008 walitakiwa kuwa TGTS F na hawa wa 2011 walitakiwa waingie TGTS E! lakini hado mwez huu wa 8 hakuna kitu ni sarakasi tu ilhali majina ya waliostahili kupanda yalitoka tangu mwez januari mwaka huu 2015! Labda kama kuna maeneo wamepandishwa basi turekebishane lakini kiuharisia naona kuna masihara flan yanafanyika.
 
increment huwa haipandi kama kutatokea mabadiliko ya mshahara (ongezeko la mshahara).. na toka 2010 kila incremental year kumekuwa na maboresho ya nyongeza ya mshahara... so hauwezi kupanda increment..
isipokuwa ikitimia miaka mitatu ya utumishi kazini hata kama bado uko mfano c1 utaruka hadi daraja d1.. hapo ndipo utakapompita huyo unayeona kaajiriwa juzi na mko sawa
...
isingetokea ongezeko/badiliko la mshahara mfano mwezi wa 7 mwakani lisipokuwepo hapo utapanda hichi kidaraja kidogo c1-c2 ...

Miaka ya nyuma licha ya ongezeko la mishahara kila mwaka annual increament ilikuwepo .hivyo kuwepo ongezeko la mwaka sio sababu ya msingi zaidi ya kuwaibia wafanyakazi.nyaraka za mishahara zinaonesha uwepo wa annual increament lakini hawatekelezi.kuna sababu gani za kuonesha kuwa jambo hilo lipo wakati sio uhalisia.hata waraka wa mabadiliko ya mishahara 2015/2016 umeonesha uwepo huo.
 
kama waraka upo basi watakuwa wanakosea...
IKO HAJA KAMA WORKING CLASS KUFANYA KITU.. tatizo hawa wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi ni wabinafsi..wanafki na wachumia tumbo...
 
Back
Top Bottom