Nyololo: Kabla na baada ya kuuawa Mwangosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyololo: Kabla na baada ya kuuawa Mwangosi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nkisumuno, Sep 6, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asubuhi hapa kijijini kulikuwa na msiba,askari wakafika msibani na kuwataka wananyololo kufanya mazishi mapema ili kuepukana na dhahama au vurugu. Baada ya mazishi watu wote wakaambiwa watawanyike, wakati wote huo watu walikuwa wanashangaa na ujio wa polisi wengi defender sita zikiwa zimejaa polisi ambao walikuwa tayari kwa mapambano.

  Hizo defener zilikuwa zikizunguka hapa kijijini. Wakati wote huo kundi dogo la wafuasi wa CHADEMA walikuwa kwenye ofisi ya Tawi wakisubiri ujio wa viongozi wao wa kitaifa huku ofisi yao ya kata ikiwa imezingirwa na polisi wa FFU huku wengine wakirandaranda. Wakati huohuo polisi bila kujua kuwa kuna watu waliokuwa wanawasikia nyumba ya jirani walisikika wakisema leo lazima tuondoke na maiti kuanzia nne na wakapiga simu kwa jamaa zao wakisema wakae mkao wa kuangalia tv jioni.

  Majira ya saa sita na nusu polisi walienda kwenye ofisi ya Tawi na kuwaamuru wafuasi wa Chadema wazime mziki uliokuwa ukipigwa kwenye gari. Chadema wakatii.

  Majira ya saa nane kama na nusu ugeni wa Chadema uliwasili na kutoa ufafanuzi kuwa hawafanyi mkutano wa hadhara bali vikao vya ndani na ndipo polisi wakawaruhusu waende kwenye ofisi yao ya kata. Wakati wakielekea kwenye ofisi za kata polisi nao wakaenda eneo hilo na ndipo nilimwona Mwangosi akichukua picha za matukio na akiwa hana hata wasiwasi. Viongozi wa chadema wakatoa amri kuwa wale wote wasio wanachama waondoke kwani walikuwa na kikao cha ndani.

  Baada ya kauli hiyo polisi wakawambia wanachama tawanyikeni wote kabla hatujaanza kutumia nguvu. Viongozi wa chadema wakawaambia wanachama wakae chini, polisi wakaendelea kusema tawanyikeni, wakati wengine wamekaa chini na wengine wanapoanza kuondoka ikatolewa amri ya kuwakamata viongozi wa chadema na kuanza kuwapiga rungu na kupiga mabomu watu tulipotawanyika kufumba na kufumbua tunaambiwa Mwangosi kauawa na polisi.

  Muda mfupi baada ya mauaji hayo na kuwajeruhi wengine wakaondoka na defender zao zote utafikiri walilenga kumuua Mwangosi tu. na hapo watu waliendelea kujiuliza maswali mengi maana hakuna hata jiwe walilorushiiwa polisi isipokuwa wao ndiyo walikuwa chanzo cha vurugu

  Nawasilisha.
   
 2. M

  Mwera JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  je wewe uliwasikia polis wakisema lazima waondoke na maiti 4 au unaweka umbea wako tu hapa jukwaani?
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,679
  Trophy Points: 280
  Kama ni umbea basi wewe weka ukweli wa kile ulichokisikia hapo kijijini Nyololo.
   
 4. M

  Mundu JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Na wewe weka wa kwako pia kama umemuona nkisumuno anafaidi sana...
   
 5. k

  kwitega Senior Member

  #5
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmbea mwenyewe. Mtu anasema alisikia halafu unakejeli anachoripoti? Tuambie na wewe umbea wako.
   
 6. Joste

  Joste Senior Member

  #6
  Sep 6, 2012
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nkisumuno kweli wewe ni Kimeo na taahira hebu acha upumbavu wako hapa. Polisi waamue kuwa na maiti nne za nini. Hao jamaa walikuwa na kikao cha ndani kwenye kiofic kidogo wakati wao walikuwa kundi, hivi vikao vya ndani ni pamoja na speakers na shamra shamra? Acheni ujinga bwana
   
 7. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  magamba bwana
   
 8. m

  mamajack JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  lioine kwanza,roho inakuuma watu wakisema ukweli au nawewe ulikuwapo kutekeleza hayo mauaji.haya sema umbea uliovimbisha hilo domo lako.
   
 9. m

  mamajack JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wewe ndo tahira mkubwa,kwa hiyo kikao cha ndani ulitaka wawe wangapi????kwa hiyo kundi lilikuumiza roho ukaona bora kuua.nadahani madhara yake magamba mmeyaona na mtahaha sana kupinga ukweli na matamko yenu ya kifedhuli.shetani wakubwa nyie.
   
 10. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Majeruhi upande wa polisi walipatikanaje?
   
 11. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  wewe ndio taahira kabisa kwanini umtusi mwenzio anaroport yaliojili kwao wewe ulikuwepo?????unapenda kusifiwa tu ukikosolewa nongwa eee
   
 12. M

  Mwera JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mbona umefura kama hamira kwa mapresha?je una ushahidi na hilo alilosema mtoa mada kua askari walipanga kuondoka na maiti 4?ukiambiwa nawewe jiambie,yeye aliwasikia mda gani hao polisi wakati anadai walikua wamejitenga kikundi na raia wote wamekimbia???
   
 13. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  I will review the circumstancies under which hearsay evidence is admissible!
   
 14. K

  Kompis Member

  #14
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Magamba wooote lazima mwaka huu yatoke pendeni msipende. MV4C kazeni buti Mungu yupo nanyi coz mnapigania haki ya Watz walio wengi.
   
 15. p

  posa Member

  #15
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 25
  Kikao cha ndani kinaweza kuwa na idadi yoyote, for instance, magamba wakikutana pale chimwaga hata 3000, na kwaya za kina komba, kile kakao ni cha ndani. Nadhani hapo nyororo pangekuwa na ofisi ya ku-accomodate wanachama basi wangekuwa ndani, lakini kwa vile hapakuwapo ndio maana ilibidi wakae nje.
   
 16. m

  mamajack JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wewe unataka shahidi awe nani???huyo aliyeriport ndiyo shahidi wa kweli.kama hutaki nenda mabwepande.kama kufura unapenda fura na wewe tukuone na roho mbaya yako.
   
 17. Blessed

  Blessed JF-Expert Member

  #17
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 2,488
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
 18. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,737
  Trophy Points: 280
  Mbona unashindwa kufikiri kwa kina kabla ya kujibu hoja!

   
 19. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,737
  Trophy Points: 280
  Hoja ujibiwa kwa hoja si matusi!
  Ukiona mtu anatumia matusi kukabili hoja ujue hiyo hoja imemzidi uzito!

  Jaribu kubadilika si lazima uandike unaweza kusoma tu!

  Mchana mwema!

   
 20. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,192
  Likes Received: 997
  Trophy Points: 280
  Haina haja ya kuumiza vichwa bandugu. Iissue yenyewe ni kwamba polisi walikuwa wakitekeleza amri kutoka kwa uongozi wa juu wa sisiemu. Kulikuwa na mkakati wa kuua watu ikiwa ni pamoja na kuwajumuisha na baadhi ya polisi wasiojua siri. Lengo ni kuhusisha mauaji hayo na chadema kwamba mfuasi wa chadema kavaa bomu na kujitoa muhanga kwa kuua polisi. Halafu Tendwa angejitokeza na kusema kuwa chedema kimepoteza uhalali wa kuwa chama cha kisiasa na hivyo kutangaza kukifuta. Tangazo hilo la kukifuta lingeenda sambamba na tangazo la polisi la kupiga marufuku mikusanyiko yote ya kisiasa mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo. Kwa mujibu wa mtoaji wa siri hii iliyopangwa na waandamizi wa sisiemu kisiri, mikutano ya kisiasa ingelikuja kuruhusiwa mwaka 2014 baada ya bunge la budget kwa ajili ya kampeni za uchaguzi huku chadema kikiwa hakipo.
  Kwa kweli kilichozuia mkakati huu usifanikiwe kwa mujibu wa mtonyaji ni Mungu mwenyewe ambae kwa siku za karibuni amejidhihirisha akiwakwamisha viongozi waovu ndani ya serikali ya sisiemu katika utekelezaji wa mipango yao miovu. Kwa mujibu wa mtonyaji ni mengi mauvu waliisha panga lakini yamewaathiri wao kuliko waliyemkusudia. Mtoa habari alinimalizia kwa kusema, hukuona ya Arumeru?, Ulimboka? Sms za kichina? Na sasa Mwangosi? Na bado akaendelea kudai yapo mengi ila anahisi huenda wakabadili mbinu ya kuwakilisha na wawakilishaji maana tathmini ya madhara ya yaliyotangulia yamekiathiri sisiemu na kukifanya kichukiwe kuliko wakati mwingine wowote. Hili nimekuwa mwiba mchungu kwao maana ni kinyume na matarajio yao. Hebu tusubiri picha litakalofuata baada ya hii ya Mwangosi.
  .
   
Loading...