Nyoka weusi wamuondoa Rais ofisini, wapotea

Nyoka weusi wamuondoa Rais ofisini, wapotea

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,421
Nyoka wawili weusi wamekutwa ndani ya ofisi ya Rais wa Liberia, George Weah hali iliyomlazimu kuhama ofisi yake kwa muda.

George.jpg

Mkurugenzi wa Masuala ya Habari wa Ikulu, Smith Toby amekaririwa na BBC akieleza kuwa nyoka hao wawili walikutwa Jumatano katika ofisi za mkuu huyo wa nchi ambazo ziko kwenye jengo la Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje.

Kutokana na hali hiyo, wafanyakazi wote waliokuwa wanatumia jengo hilo wametakiwa kutoenda tena kazini hadi Aprili 22, kupisha shughuli za kuwaondoa nyoka hao pamoja na wadudu/wanyama wengine wasiohitajika.

“Lengo ni kuhakikisha kuwa wanyama na wadudu wote wanaotambaa au wanaoruka wanaondolewa kwa kupuliza dawa za kuua wadudu (fumigation),” alisema Tody.

“Wizara ya Mambo ya Nje ndiyo yenye ofisi za Rais, kwahiyo imetoa tangazo la ndani kwa wafanyakazi wake kubaki nyumbani wakati ambapo kazi ya kupuliza dawa maalum za kuwaondoa wadudu na wanyama ikiendelea,” aliongeza.

Tody alisema kuwa nyoka hao wawili walioonekana hawakuuawa, walifanikiwa kupata upenyo kwenye tundu moja na kutokomea kusikojulikana.

Ofisi ya Rais imekuwa ndani ya jengo la Wizara ya Mambo ya Nje tangu mwaka 2006 baada ya moto mkubwa kuteketeza moja kati majumba ya makazi ya Rais.

Polisi na kikosi maalum cha ulinzi wa Rais walionekana wakiwa wameongeza ulinzi kwenye eneo la makazi ya Rais katika Mji Mkuu wa Monrovia.

Source
 
Hio nyumba ina mashimo ya nyoka kutorokea??

Nyoka aingie ndani ya ofisi apotee hapo hapo ndani bila kutoka njepaka waamue kupuliza dawa za kuua wadudu kweli.
 
Kwanini wasitie Timu pale Cuf Buguruni ingependeza.
Hahaaaaaaa........

Unataka Mkuu Imhotep "utaalam" huo uhamishiwe CUF Buguruni kwa nia ya kumtoa nduki La Profeseri Lipumbaaaa??
 
Ushirikina tu wa kiafrika bado kuna watu wanawaza ushirikina mpaka kesho"
 
Nyoka mweusi kama ni wale "Black mamba" ni nyoka hatari wanauma na sumu yao uponi. Inasambaa haraka mwilini na inauwa moyo haraka na uhai unaishia hapo. George Weah, pole sana, puuzia habari za kishirikina. Fanya utafiti wakina taarifa zimejaa mashaka sana, kuwa makini.
 
Black mamba ana rang ya kijivu lakini mdomo wake kwa ndani ndio mweusi. Hiyo rangi nyeusi ndio sumu yake. Nawasilisha
Nyoka mweusi kama ni wale "Black mamba" ni nyoka hatari wanauma na sumu yao uponi. Inasambaa haraka mwilini na inauwa moyo haraka na uhai unaishia hapo. George Weah, pole sana, puuzia habari za kishirikina. Fanya utafiti wakina taarifa zimejaa mashaka sana, kuwa makini.
 
Eti puuzia habari za kishirikina....unaandika ivi utafikiri wew ni mgeni na africa

Back
Top Bottom