Nyoka wa maajabu apatikana

Aventus

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
2,011
2,165
Jana katika taasisi ya wanyama pori ya Nat Geo ilitangazwa kuwa ametokea nyoka hatari
sana ambaye hajawahi kutokea duniani wanadai kwamba nyoka huyo anaongezeka urefu wa 0.5sm kila kila chakula na huwa anakula chakula kuanzia sekunde 30 kurudi
nyuma.

Mpaka sasa hakuna silaha ya kuweza kumuua nyoka huyo isipokuwa akijiuma mwenye ndo anaweza kufa, wanasayansi hao walieleza japo uchungu zaidi bado
unaendelea huyu ni nyoka anayeua kuliko nyoka wote waliowaho kutokea katika historia
ya maisha ya mwanadamu nyoka huyu hupatikana katika simu pekee za NOKIA TOCHI katika sehemu ya game inaitwa snake Xenzia.
 
Hehe!ha
Mkuu umekosea sasa
Title ilitakwa iwe ya kutisha kidogo kama hivi
DUNIA KUANGAMIA;JOKA LA KUTISHA ZAIDI LIMETOROKA MAABARA
Halafu badala ya 'Geo' ungeweka kitu kama NGSS-Anaconda-Academy yaani ilimradi tu,kutisha watu
Au anaongezeka urefu wa kM 5 kila sekunde

Mbona ungewapata vichaa wenzako..!
 
Ukitaka uongo wako upendeze na ufanane na ukweli ungesema, nyoka huyu ni hatari sana hata kwa Simba, chui na jamii zote za tai wanaokula Nyama na samaki. Maana kama risasi, kemikali na mabomu hayawezi kumuua hapo lazima watu wote tungeamini.
 
YAANI INIMECHEKA SANA NIMETUMIA NGUVU KUBWA KUFUATILIA HII HABARI NIKITARAJIA NA PICHA KUMBE DUH....NIENDE TU HOME NIKAMWANGALIE KWENYE TOCHI NOKIA YA H/BOY WANGU
 
Hehe!ha
Mkuu umekosea sasa
Title ilitakwa iwe ya kutisha kidogo kama hivi
DUNIA KUANGAMIA;JOKA LA KUTISHA ZAIDI LIMETOROKA MAABARA
Halafu badala ya 'Geo' ungeweka kitu kama NGSS-Anaconda-Academy yaani ilimradi tu,kutisha watu
Au anaongezeka urefu wa kM 5 kila sekunde

Mbona ungewapata vichaa wenzako..!
Hahaha nmefrah
 
Ukitaka uongo wako upendeze na ufanane na ukweli ungesema, nyoka huyu ni hatari sana hata kwa Simba, chui na jamii zote za tai wanaokula Nyama na samaki. Maana kama risasi, kemikali na mabomu hayawezi kumuua hapo lazima watu wote tungeamini.
Hapo ss ntakua nmezidisha chumvi
 
Back
Top Bottom