White party
JF-Expert Member
- May 5, 2015
- 1,037
- 1,179
Ulikuwa na njaa,.OVER!
Yaani mkuu nimecheka mpaka basiNimejikuta nacheka peke yangu. Mkuu angalia isije ikawa unataka kupata malaria kweli, unajua ungeuliza ndoto ina maana gani ningekuelewa, ila unapouliza wewe ni nani ndio hapo umeniacha hoi. Wewe si binadamu au? ungekuwa nyoka ungeweza kweli hata kuja humu JF?
Duu hii sasa kibokoHakuna nyoka wa ajabu wala sungura au kunguru,hizo ni njozi.UNUSUAL DREAMS mara nyingi huwapata watu wanaotumia aina fulani ya madawa.Watu wanaotumia dawa za kupunguza makali (ARV) Hasa dawa ya EFAVIRENZ huwaletea njozi mbaya za kutisha.Huenda mtoa mada yuko kwenye dose za ARV au dawa zingine.Kwa wale wanaotumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu mara nyingi hua wanapatwa na tatizo la HALLUCINATION.Mwathirika ataanza kuona vitu au viumbe mbele yake wakati ninyi wazima hamuoni chochote.Madereva walioathirika huweza kumwona mtu,mnyama,nyoka nk wakikatisha k atikati ya barabara na anapojaribu kukwepa anapinduka.Akinusurika kufa yeye hudai eneo la mahali pale kuna wachawi.
Jimena, kwani husomi nilichokueleza hapo juu? Sababu sio kulala mchana bila kula mimi ni daktari zingatia sababu nilizokutajia.Hakuna sababu zingine labda ziwe za kienyeji.![]()
![]()
sawa mkuu, sitarudia tena kulala mchana kabla sijala
Sasa mi situmii ARV wala drugs ndio maana sikufatilia ushauri wako.Jimena, kwani husomi nilichokueleza hapo juu? Sababu sio kulala mchana bila kula mimi ni daktari zingatia sababu nilizokutajia.Hakuna sababu zingine labda ziwe za kienyeji.
mmmmh. ....Hakuna nyoka wa ajabu wala sungura au kunguru,hizo ni njozi.UNUSUAL DREAMS mara nyingi huwapata watu wanaotumia aina fulani ya madawa.Watu wanaotumia dawa za kupunguza makali (ARV) Hasa dawa ya EFAVIRENZ huwaletea njozi mbaya za kutisha.Huenda mtoa mada yuko kwenye dose za ARV au dawa zingine.Kwa wale wanaotumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu mara nyingi hua wanapatwa na tatizo la HALLUCINATION.Mwathirika ataanza kuona vitu au viumbe mbele yake wakati ninyi wazima hamuoni chochote.Madereva walioathirika huweza kumwona mtu,mnyama,nyoka nk wakikatisha k atikati ya barabara na anapojaribu kukwepa anapinduka.Akinusurika kufa yeye hudai eneo la mahali pale kuna wachawi.
Habari za mda huu wana JF
Siku ya leo mapema tuu mchana kwenye saa saba wakati napitia posts mbali mbali hapa jamvini nilijikuta nimepitiwa na usingizi wa ghafla.
Na kujikuta nipo mazingira ambayo sijawahi kuyaona, na nilikuwa katika umbo la nyoka kimwili na mawazo pia, hilo halikunishangaza sana kwa sababu nilijiona kuwa mimi ni nyoka na niliona hayo ndio maisha yangu ya siku zote kama nyoka wengine,
Lakini ghafla kulitokea na njiwa wawili waliotua mbele yangu juu ya mti ulio mfano wa miti ile ya Crismass, nami nikaanza kuupanda ule mti kwa taratibu na busara kwa lengo la kuwakamata wale njiwa ili niwale...
Cha ajabu nilipofika juu na kuwakaribia nikagundua kuwa wale sio njiwa ila ni kunguru, na mimi kama nyoka nilikuwa sina tabia ya kula kunguru hivyo niliamua kushuka chini bila kuwabugudhi niendelee na mambo mengine lakini nilipofika chini na kutazama tena juu ya ule mti niliwaona kuwa ni njiwa na wala si kunguru kama nilivyofikiri hapo mwanzo, kwa mara ya pili niliamua kurudi tena juu ya mti ili niwakamate, ila nilipofika juu niliwaona ni kunguru na wala sio njiwa, hichi kitu kilinishangaza sana, maana nikiwa chini nawaona kama njiwa lakini nikiwa juu nawaona kama kunguru...
Wakati nipo katika dimbi la mawazo nisijue nini cha kufanya mara ghafla chini ya ule mti alipita sungura...
Hapo sasa nikaachana na habari ya wale njiwa/kunguru na kuanza kumfukuza yule sungura,
Ghafla nikashituka maana nilikuwa naamshwa ili nile chakula cha mchana na nilipongalia saa ilikuwa ni saa saba na dakika ishirini na tano mchana
Shida yangu hapa sio tu kutaka kujua hii ndoto inamaanisha nini Ila nikukutaka kujua mimi ni nani?
Je mimi ni binadamu ambaye nawaza/kuota kuwa nyoka au ni nyoka ambaye anawaza/kuota kuwa binadamu???
Na je maisha yangu na ufahamu wangu kwa sasa upo wapi?
Ni kwa nyoka au binadamu?
Na ni yapi ni maisha yangu ya kweli ninayoishi sasa kati ya nyoka au binadamu?
Cc Appolo Annael Bennie 369 Mkuu wa chuo aretasludovick pamoja na wengine wote ambao mna ufahamu kuhusu haya maswala naomba ufafanuzi wenu maana naona muda unapita bila mimi kupata ufumbuzi kwenye hili
Asante sana KirangaWewe ni Mtanzania. Kupitia post mbalimbali ni maisha. Kusinzia ni kupoteza umakini.
Njiwa wawili walio juu ya mti wa Krismasi ni uongozi mzuri wa chama na serikali kuongoza nchi.
Wewe kutaka kuwala njiwa wale wawili ni wananchi kutaka uongozi mzuri wa chama na serikali uwasaidie kutatua matatizo yao, ikiwamo njaa na mengine.
Nyoka kugundua kwamba wale waliodhaniwa ni njiwa juu ya mti wa Krismasi si njiwa ni kunguru, ni wananchi kugundua kwamba uongozi wa chama na serikali si mzuri, ni mbaya na haufai. Wamehadaa wananchi kwa ahadi za uongo wakaonekana wazuri, walivyofika kwenye uongozi wanaonekana tofauti.
Sungura waliopita chini ya ule mti ni vyama vya upinzani.
Hii ndiyo tafsiri ya ndoto yako.
Ila huyu shetani kama angekuwepo kweli siku moja angewajibu mana kila kitu anabebeshwa yeye.Dah pole sana kaka iyo ni ishara mbaya sana kwako,unatakiwa ujitafakali mwenendo wako sio mzuri kuna mapepo au mashetani au unaroho ya uasi,maana yake shetani anakutumia kwa kukutamanisha ni iv ww ni nyoka ni mambo yako ya kishetan tena shetani kakuvaa sanaa na ananutumia kwa nguvu nyingi sana anakutamanisha na unatamani unafata matamanio yako lkn upate unachokitamani,na ukikata shauri unatamanishwa zaidi