Nyoka ‘amtimua’ Waziri kanisani

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri, juzi
alitimua mbio kunusuru maisha yake na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Usharika wa Sanya Juu, mtaa wa Kilingi.

Hali hiyo ilitokea baada ya tukio la nyoka kutoka kusikojulikana kuingia kanisani humo huku Naibu Waziri akijiandaa kuendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa hilo. Tukio hilo lilitokea katika ibada ya saa nne iliyokuwa ikiongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao, ambayo pia ilikuwa ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo.

Mwanri aliyekuwa mgeni rasmi kwa ajili ya kuendesha harambee hiyo ya Kanisa la Kilingi, akiwa na mkewe meza kuu, aliwashangaza waumini alipokimbia akiwa amenyanyua mikono juu. Kutokana na kuibuka kwa nyoka huyo, waumini walikimbizana na kiumbe huyo kwa mawe na viti bila kujali kama walikuwa ibadani, huku Askofu na wachungaji wengine wakiendelea kusali na waumini kutakiwa kurejesha utulivu katika ibada.

Hata hivyo, jitihada za waumini za kumkimbiza nyoka huyo kutaka kumwua hazikufanikiwa, baada ya kutoweka asionekane tena, jambo lililoacha simulizi la ni kwa jinsi gani alifika mahali hapo. Awali mgeni rasmi wa harambee hiyo, alikuwa awe Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, lakini kutokana na kubanwa na shughuli za sherehe za maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa CCM, alishindwa kufika.

'Habarileo' lilishuhudia Mwanri ambaye pia ni Mbunge wa Siha akikimbia huku akitamka maneno ya “shindwa kwa Jina la Yesu wewe shetani, shetani shindwa kwa Jina la Yesu,” huku wageni wengine waalikwa wakianguka chini wakijiokoa.

Akizungumza na 'Habarileo', Mwanri alisema tukio hilo ni la kushangaza zaidi, kwani nyoka huyo alipita nyuma ya watu wote, lakini hakuonekana hadi katika meza yake huku akiwa amenyanyua kichwa chake na kutema sumu.

“Inashangaza sana kwani lazima ujiulize alifikafikaje hapo mbele, wakati nyuma yangu kulikuwa na watu wengi...alikuwa na hasira sana, kwani alikuwa tayari kung'ata, kwa kweli hadi sasa mimi sielewi ni mambo gani haya,” alisema Mwanri. Hata hivyo hakuna madhara makubwa yaliyotokea mbali na mhamaniko uliowapata waumini hao. Nyoka huyo hakuweza kutambuliwa aina yake kutokana na mtafaruku huo.
 
inamaana hata mlinzi wa mwanri alitimua mbio asiweze kumtambua huyo nyoka?
 
duh habari hiii imenichekesha kweli na kunifanya nionekane mwendawazimu , maana ni kichekesho toka kichwa cha habari mpaka mkiani duh hii kali....
 
hahahahahahahahahaa
kazzi kwelikweli
nimecheka kweli

sipati picha lile pande la mtu
likitoka nduki , huku likilalama
shinwa kwa jina la yesu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


pole mheshimiwa
 
Hii tabia ya mafisadi kukimbilia kujisafisha kwenye nyumba za ibaada imeshamchukiza Mungu naona ameamua awadhibu mlemle kanisani.
 
kweli hatari haina dini. Ni lazima kufa ili kuufikia ufalme wa mbinguni lakini hata waliopo kanisani wanapatwa na hofu ya kifo, je sisi watu wa mataifa itakuwaje?
 
Aha aha aha...NIGERIAZ ukishindwa kuwapa kitu kidogo chao wanakufata at kwenye nyumba za ibada...Haya ndo matatizo ya kuchanganya HAKI na BATILI.....By the way ilishanenenwa ya MUNGU mpeni yeye na YAWASHIRIKINA wenu wapeni wenyewe...USIKU kwa waganga wa kienyeji ASUBUHI kanisani kweli mheshimiwa sana?
 
Bwana Kombo kwenye habari wanasema nyoka alionekana ndio maana waumini wachache walinyanyua viti na mawe kutaka kumpomba ila akatokomea.
Mwanri ana matatizo yake mengine tu, huyo nyoka wa kuonekana nae tu nyoka gani huyo? Isije kuwa Mheshimiwa alikuwa anasinzia kanisani akaota mambo ya ajabu!
 
Back
Top Bottom