undefine
JF-Expert Member
- Nov 17, 2016
- 442
- 1,011
Mwanamke mmoja astuka baada ya kugundua nyoka aina ya Black mamba yupo pembeni ya kitanda chake
Wiki 2 zilizopita nilitoa uzi kuelezea namna nyoka aina ya black mamba alivyoingia kwenye moja ya nyumba ya mwanamke iliyopo westville nchini Afrika kusini na kupanda kitandani na kulala bega kwa bega mubashara na mwanamke huyo na alipostuka yule mwanamke alishuka kitaratibu kitandani na kumpigia simu Nick Evans mtaalamu wa nyoka aje kumtoa black mamba yule .
Tukio lingine limetokea tena katika moja ya familia nchini Afrika kusini ambapo waligundua uwepo wa black mamba juu ya dirisha akitafuta mahali apate joto.
Nick Evans kutoka KwaZulu Natal Amphibian and reptile conservation aliitwa na familia hiyo kwenda kumkamata nyoka Huyo na kumpeleka sehemu salama.
"Mamba hakuwa mkubwa sana ila kiasi alikuwa mkubwa-Evans
" kusema kweli nilikuwa na shauku sababu black mamba yule alikuwa na faida ya kuwa na urefu mkubwa.
"Lakini black mamba huyu amethibitisha kuwa sifa wanayopewa ya kuwa wakali sana na kushambulia hovyo zimeongezwa chumvi.Utaona kwenye video kwamba alikuwa anataka mimi nimuache pekee yake atulie zake na kunipa tahadhari kwa kufungua mdomo wake mweusi niondoke lakini nisingeondoka sababu ilibidi nyoka huyo aondolewe. -Evans
" ilibidi niwe muangalifu ili nisimuumize mamba na pia nisijiumize mwenyewe -Evans
Nick Evans akimkamata black mamba katika nyumba aliyoingia.
NB:ndani ya wiki 3 Nick Evans amepigiwa simu Mara 2 kwenda kuwatoa black mamba walioingia nyumba za watu.Jambo la kujifundisha tunapowaona nyoka wameingia majumbani kwetu haswa venomous snakes kama mamba tusijichukulie sheria mkononi kwa kuwaua kikatili bali tuwapigie simu TANAPA waje kuwatoa bila ya kuwaumiza,.hizi familia 2 huko south wamefanya jambo ambalo sisi waTanzania tujifunze.Nyoka anapoingia kwetu tusianze kupiga mayowe na kuita watu na kuanza kushambulia sababu kufanya hivyo utahatarisha maisha yako kwa kumfanya mamba a-panic na kushambulia hovyo wakati ni mpole ,pia ni kinyume cha sharia kuua nyoka waliochini ya maliasili.
Huu ni msimu wa nyoka kuonekana sana haswa maeneo ya chunya ,tukuyu ,mbeya ,iringa ,Tabora nk ,ndugu zanguni pindi mkiwaona wapigieni simu TANAPA.